Ni ubabaifu mwanaume kulilia mali za mwanamke katika talaka. Kesi ya talaka ya Fatma Karume ina masomo muhimu sana

Ni ubabaifu mwanaume kulilia mali za mwanamke katika talaka. Kesi ya talaka ya Fatma Karume ina masomo muhimu sana

Katika maisha yangu siwezi kuoa mwanasheria ni washenzi sana.
Woga tu.....

Jamaa yangu kamuoa mmoja ambaye alikuwa KISOI mno....leo amekuwa chini ya nyayo ya mwamba....nilimpeleka mwamba kule Mwamgongo Kigoma....hiyo ndiyo DAWA yao ha ha ha
 
Kusonga ugali kwani sio kazi?
Mbona mnalipa hela kwa mama ntilie
Kwahiyo akiachika atasonga ugali ajenge ghorofa si ndio.
Asingeolewa angekua pia anapika ale ila sasa anapika bila kutafuta anachopika.

Kazi za nyumbani haziwezi ingiza kipato ndio maana mkiacha kazi mkakaa nyumbani wote hizo kazi za nyumbani hazitawaingizia chochote na njaa itataradadi.

Na hata usipooa au kuolewa hauwezi kufa njaa hivyo hauwezi kusema wewe ulikua unapika ugali.

Kila mmoja haya maisha achakarike asimtegemee yoyote awe mwanamke au mwanaume dunia ya sasa haina huruma utakuja kukuta mali kaandikwa mama wa mmeo ulie kilio kikuu.
 
Woga tu.....

Jamaa yangu kamuoa mmoja ambaye alikuwa KISOI mno....leo amekuwa chini ya nyayo ya mwamba....nilimpeleka mwamba kule Mwamgongo Kigoma....hiyo ndiyo DAWA yao ha ha ha
Siku dawa ikiisha atakiona cha mtema kuni.
 
Nashangaa sana ujue hakuna kazi ngumu kama kazi za nyumbani nashangaa watu wanachukuliaga poa sana hii sekta.. kuwafanyia maandalizi watoto na baba wanaokwenda shule na wanaokwenda kazini waende wakiwa smart..na bado wengine ubaki nao na kazi za nyumbani upambane nazo warudi wakute mambo yako fresh si jambo rahisi na ukute hana hata msaidizi wa nyumbani so ni kila kitu anafanya mtu mmoja tena kwa ukamilifu na bado anachukuliwa poa mwanamke hiyu..wanahaki na kupata 50 50 acha mfumo uwabebe
Katika mambo yote hayo jioni anakua ameingiza shilingi ngapi kama shares zake kwenye mgao wa 50/50..?
 
Huwa nawaaprisheti sana wanaume wanaowarecognise wake zao japo kwa pesa kidogo motisha kwao..sa mijanaume mingine haijali wala nn si kwa losheni ,nguo za ndani za mkewe wala pesa za kusuka ..kazi za nyumbani zinachosha usipokuwa makini unachakaa utashinda bila kuoga au mazingira ya nyumbani yatakuwa safi ila wewe mama mchafu utakosa muda wa kuoga hekaheka hadi jioni inakukuta unaogea kitanda unalala hoiii..
Mbona hawarudi kwao kama majukumu yake yamemshinda, kwenye maofisi ya watu tunafanya kazi hadi overtime, mambo yakimzidi apishe aje muajiriwa mwingine
 
Kuna funzo hapa.

Wanandoa tarajali kusainiana Mikataba ya Kusajili Mali zao (Pre-nuptial Contract) ni muhimu sana katika maisha ya Sasa.
Pre-nuptial Contract will help to avoid the problem of the Marriage Conemanship in case of divorce like this.

Ukichunguza kwa umakini Sana utagundua kwamba kiuhalisia Wanaume wenyewe huwa wanakuwa chanzo cha matatizo yote haya ya wao kutapeliwa au kudhulumiwa mali zao kwenye masuala haya ya talaka.

Kwa kawaida mgawanyo wa mali kwenye talaka huwa unagusa mali zile tu ambazo ni 'Chumo la Ndoa,'(Matrimonial Property). Kama Mwanandoa wa kike naye alichangia kwenye suala la upatikanaji wa mali husika, sioni tatizo lolote lile na yeye akipewa Haki yake katika mchakato mzima wa mgawanyo wa mali wakati wa talaka.
Nakaa ukimya kwa sasa
 
Back
Top Bottom