Kwa mara nyingine tena, Rais wetu huyu Chifu Hangaya amefanya mahojiano na chombo cha habari.
Nimeangalia vipande vipande kadhaa vya mahojiano hayo na sijaona swali lolote lile lililo gumu aliloulizwa huyu chifu wetu.
Anaulizwa vi softballs tu. Naye anatoa majibu mepesi mepesi tu. Sijui mara anaingia mitandaoni, mara anacheza na wajukuu, mara sijui kusikiliza Taarab, yaani mambo mepesi mepesi tu.
Alisema[ga] Le Mutuz, viongozi wetu ni akisi yetu sisi wenyewe wananchi.
Nchi hii ina changamoto kibao. Ina viongozi waongo. Tena waongo wasio hata na haya.
Waandishi wa habari wanapata fursa ya kumhoji Rais aliyeshiriki kudanganya, hawamuulizi kwa nini yeye na wenzake huwa wanatudanganya.
Ni kwenye vijamhuri vya midizi tu kama Tanzania ambako viongozi waandamizi wa kiserikali chao wanawadanganya watu wao kuwa Rais wao ni mzima ilhali si mzima. Ni mgonjwa mahututi au ni marehemu tayari.
Halafu hakuna anayejali [ukinitoa mimi] kuwa kuwa amedanganywa na hakuna anayejali kuona kuwa kunakuwepo na uwajibikaji.
Kama Ayoub Rioba angekuwa yule aliekuwa anafanya vipindi kupitia ITV, bila shaka angekuwa na maswali yenye kutaka kujua Rais anawaza nini ana anatupeleka wapi.
Au kama ni Tido Mhando wa sasa Azam au Tido wa BBC sio Tido wa TBC, hapo napo tungeweza kuwa na maswali magumu kwa mepesi yanayowakilisha mahitaji na hisia za umma.
Au hata angekuwa Masoud Kipanya wa Clouds mmoja wa watangazaji wa Power Breakfast, napo tungepata kujua madam SSH anaposheherekea miaka 62 na takribani anaelekea kutimia mwaka mmoja akiwa CinC, tungekuwa na bonge ya session.
Ila waajiriwa wa serikali, magari yao STK/STJ/STL ambao uteuzi wa nafasi ya DG ni mamlaka ya kiserikali, kutakuwa na sense ya uwoga "kumbana" boss.
Ila kama kurugenzi ya mawasiliano ingekaa na madam ili kutengeneza sense ya kuandaa session ambayo legends kama Tido wanaweza kualikwa, bila shaka ingekuwa session nzuri zaidi ya hii ya leo.
JPM alijaribu mara moja pale IKULU kuwa na wanahabari wote, akawepo Tido; kuna swali zuri sana toka kwa Paskali Mayala kuhusu separation of power, majibu yalileta mjadala ila ujasiri wa Mayala kuuliza swali gumu na mhusika kujibu na mjadala ukaendelea, hiyo inakuwa bonge ya session.
Tutafika. Watu bado wanaogopa maisha ya kitaa kama nafasi zao wakipewa watu wengine.
Tido atabaki moja wa watangazaji mahiri ambae kuna wakati alipitia mawimbi makali, ila alisimama kulinda heshima ya kazi ambayo kaifanya kwa weledi na skills za hali ya juu akiwa BBC mpaka sasa.