Ni uoga au ni uwezo duni wa waandishi wetu wa habari?

Ni uoga au ni uwezo duni wa waandishi wetu wa habari?

Mkuu wakati Nyerere anataka Dodoma iwe mji mkuu, imechukua muda mrefu sana mpaka kaingia Mkapa ndipo shughuli nyingi zikahamia Idodomya na karimjee ikawa basi tena.
Nyerere alitaka kujenga bwala la umeme, mpaka anaondoka hapakuwa hata na dalili, leo hii linajengwa na tunasubiri crane toka ughaibuni kuja kuziba magati ya maji.
Nyerere alitamani kujenga daraja kati ya kagamboni na kivukoni, JK akaja akawa sehemu ya ndoto hiyo.
JPM kwa kukoswakoswa kuzama kwa mtumbwi kigongo busisi akiwa na pikipiki yake aina ya Honda, years later kawa mkulu ameacha ujenzi wa darala la kigongo busisi ili kurahisisha usafiri.

Yote hayo yamechukua muda ila yamefanyika.

Inawezekana kuna siku mwanao akaja kuwa mtu mwenye ushawishi nchi hii na kukawa na freedom of media to the extent ya kumweka "Mhe. Rais wa nchi Kitimoto".

Nihitimishe kwa kusema US ilipata uhuru 1776, Presidential debate ya kwanza ilikuwa 1960 kati ya alikuwa Senator John F. Kennedy na aliekuwa VP Richard Nixon.

Ipo siku, kama sio mie, kuna atakae kuamsha. Kama sio dunia hii basi ile ijayo.

F
Debates Marekani mbona zimeanza siku nyingi tu.

Lincoln - Douglas debates zimefanyika mwaka 1858.

Unaijua significance ya hizo debates?

1858 ni miaka 102 kabla ya 1960….
 
Kwa mara nyingine tena, Rais wetu huyu Chifu Hangaya amefanya mahojiano na chombo cha habari.

Nimeangalia vipande vipande kadhaa vya mahojiano hayo na sijaona swali lolote lile lililo gumu aliloulizwa huyu chifu wetu.

Anaulizwa vi softballs tu. Naye anatoa majibu mepesi mepesi tu. Sijui mara anaingia mitandaoni, mara anacheza na wajukuu, mara sijui kusikiliza Taarab, yaani mambo mepesi mepesi tu.

Alisema[ga] Le Mutuz, viongozi wetu ni akisi yetu sisi wenyewe wananchi.

Nchi hii ina changamoto kibao. Ina viongozi waongo. Tena waongo wasio hata na haya.

Waandishi wa habari wanapata fursa ya kumhoji Rais aliyeshiriki kudanganya, hawamuulizi kwa nini yeye na wenzake huwa wanatudanganya.

Ni kwenye vijamhuri vya midizi tu kama Tanzania ambako viongozi waandamizi wa kiserikali chao wanawadanganya watu wao kuwa Rais wao ni mzima ilhali si mzima. Ni mgonjwa mahututi au ni marehemu tayari.

Halafu hakuna anayejali [ukinitoa mimi] kuwa kuwa amedanganywa na hakuna anayejali kuona kuwa kunakuwepo na uwajibikaji.

Kuna mwanahabari mwenye akili akafanya kazi TBC??
Wengi pale wanatema mate kwenye microphones wakisubiri teuzi!
Like really, unamuuliza Rais kuhusu "mdako"??
 
Kuna mwanahabari mwenye akili akafanya kazi TBC??
Wengi pale wanatema mate kwenye microphones wakisubiri teuzi!
Like really, unamuuliza Rais kuhusu "mdako"??
Go figure 🤣🤣🤣
 
Rais anapenda kuingia mitandaoni (kwa kauli yake mwenyewe).
 
Unalaumu Mwanahabari ? Kama tu Spika wa Bunge alichambwa na kudhalilishwa na mwishowe “kujiuzulu“ kwa kuhoji tu ije kuwa huyo Mwanahabari ?
Kwa hiyo unamtaka Job Ndugai aendelee kuwa Spika pamoja na udhalimu aliofanya dhidi ya uhuru wa Bunge na Demokrasia?

Kweli Watanzania hatujui tunachotaka
 
Nimeshangaa yani kama alikosa maswali kabisa angemuuliza anaonaje au kuzungumzia vitu na bidhaa na huduma kupanda bei kila kukicha?

Basi hata mwandishi alishindwa kuigilizia maswali ya Kikeke akamuuliza? Waandishi wanahangaika kujipendekeza hadi wanasahau kuuliza maswali ya msingi!

Yani watu wameona kujipendekeza kunalipa sana ...na ni kweli wanaogopa kufukuzwa kazi kwa kuuliza maswali magumu
Mnapoona maswali hamna mkubali tu kuwa nchi inakwenda vizuri.

Tusitmegemee Rais Samia aulizwe maswali kama Rais Abiy Ahmed wa Ethiopia ambaye nchi yake iko vitani na watu wanaotaka kujitenga wa Tigray.
 
Azori Azori, ngabu kwa umakini wako wote hujui kwamba ukiuliza swali gumu watatokea watu sebuleni kwako bila kuwafungulia milango. Tuweni makini basi wazee nyakati nyingine.
 
Kwa hiyo unamtaka Job Ndugai aendelee kuwa Spika pamoja na udhalimu aliofanya dhidi ya uhuru wa Bunge na Demokrasia?

Kweli Watanzania hatujui tunachotaka

Aliyedhalilishwa na kudhihakiwa siyo Ndugai boyfriend bali ni Spika wa Bunge la JMTZ, do you get the picture?
 
Nyie wenye majigambo ya uelewa na uwezo mkubwa wa kufanya mambo mbona hatuoni impact yenu kwenye jamii? Mara nyingi ni porojo tu na majigambo yasiyokuwa na tija!
 
Debates Marekani mbona zimeanza siku nyingi tu.

Lincoln - Douglas debates zimefanyika mwaka 1858.

Unaijua significance ya hizo debates?

1858 ni miaka 102 kabla ya 1960….
Oh, you have a point boss wangu.

Pengine tusema national televised Presidential debate ndio ilianza na Kennedy na Nixon, hii niliweka kwa muktadha wa televised Tz Presidential birthday cake cutting which went after a talk with TBC Journalist.

Waingereza na ujanja wao wote na demokrasia na uhuru wa habari, 2015 ndio kukawa na televised debates.

Kiufupi, bado tuna safari ila tutafika siku moja.
 
Kwa mara nyingine tena, Rais wetu huyu Chifu Hangaya amefanya mahojiano na chombo cha habari.

Nimeangalia vipande vipande kadhaa vya mahojiano hayo na sijaona swali lolote lile lililo gumu aliloulizwa huyu chifu wetu.

Anaulizwa vi softballs tu. Naye anatoa majibu mepesi mepesi tu. Sijui mara anaingia mitandaoni, mara anacheza na wajukuu, mara sijui kusikiliza Taarab, yaani mambo mepesi mepesi tu.

Alisema[ga] Le Mutuz, viongozi wetu ni akisi yetu sisi wenyewe wananchi.

Nchi hii ina changamoto kibao. Ina viongozi waongo. Tena waongo wasio hata na haya.

Waandishi wa habari wanapata fursa ya kumhoji Rais aliyeshiriki kudanganya, hawamuulizi kwa nini yeye na wenzake huwa wanatudanganya.

Ni kwenye vijamhuri vya midizi tu kama Tanzania ambako viongozi waandamizi wa kiserikali chao wanawadanganya watu wao kuwa Rais wao ni mzima ilhali si mzima. Ni mgonjwa mahututi au ni marehemu tayari.

Halafu hakuna anayejali [ukinitoa mimi] kuwa kuwa amedanganywa na hakuna anayejali kuona kuwa kunakuwepo na uwajibikaji.

Bro naona umemiss a point hapo,
Hio ilikuwa ni hafla ya birthday ya Mheshimiwa Mama Rais, so kuanza kuuliza maswali yasiyohusiana na mnasaba wa tukio ni kuivunjia heshima taaluma.. Hafla ya Birthday inahusiana na maisha binafsi ya mtu , hivyo wananchi watataka kusikia yahusuyo hayo maisha yake na si vinginevyo.. Maswali mengine ya kitaifa yana mahali pake mnasaba na sio pale.
 
Back
Top Bottom