Rebeca 83
JF-Expert Member
- Jun 4, 2016
- 15,136
- 32,268
Ngoja niongelee sababu ya mimi kutojali.
Mwanzoni nilikuwa sipendi kabisa kuwasikia mashoga wala hata kuwaona na nilikuwa nawaona kwenye mitandao hii ya kijamii.Nilipofika chuo mwaka wa kwanza hostel nikapangwa na lesbians wawili kwenye chumba cha watu wanne.Mmoja alikuwa ni wale waongeaji wachekeshaji sana kwa hiyo baada ya week tu akasema kabisa mimi napenda wasichana wenzangu.Kusema kweli nilishtuka kwa sababu huwezi kumdhania ni msichana mzuri sana na wala hana viashiria vya kupenda labda sijui nguo za kiume wala nini ila sisi mule tukapotezea,huyu wa pili alikuwa sio muwazi kama mwenzake na ilichukua kama miezi mitatu hivi ndio akaniambia mimi na mwingine aliyejua ni yule lesbian mwenzie.Room mate mwenzetu mpaka tunaondoka hakujua na hakumwambia.
-Sasa hawa watu ndio walikuwa na marafiki zao wa kiume ambao wengi walikuwa ni hao gays na walikuwa wakija pale room kwetu.Mimi nilikuwa naongea nao kawaida tunapiga stori,tunacheka,tunashare interest za movies na series,tunawaponda wanaume tunadate nao ilikuwa ni kama ni extended female circle.Sasa mtu akikuta room anakusalimia kwa heshima,hajawai kukudharau wala kukuonyesha lolote baya kwako nianze kumchukia ghafla kisa ya uchaguzi wa raha zake uko faragha kwani mimi ni malaika hapa duniani sina dhambi.
-Hii ndio sababu nimekaa kimya nachukulia kawaida kwa sababu mwisho wa siku na wao ni watu kama mimi wenye mazuri na mabaya yao.Sisemi kama naungana nao kwamba wanachokifanya ni sahihi ila huwezi nikuta nawatukana kwa sababu eti ni shoga au ni lesbian
Ni kweli..personal/private matters..should remain private...sasa kuna watu wanataka kuchukulia private matters za watu kama zina national interest vile, kwamba ushoga ni oxygen,ikikosekana jamii ita suffocate.. very wrong..sasa mtu hakuboi, yuko dependable anakusaidia mambo mengi ,you share laughter..he/she is making you happy.,and you can trust her/him and call her/him a friend...then uwe source ya matatizo kwake, kisa tu una beliefs/values zako ambazo unaona unaweza ukam force nazo... very unfair!...nimependa post yako mkuu...