Ni usafi mwanaume kukojoa kwa kuchuchumaa na kisha kutawadha baada kumaliza

Ni usafi mwanaume kukojoa kwa kuchuchumaa na kisha kutawadha baada kumaliza

Msichukulie utani, wako serious.

Kuna siku nilibanwa barabarani nikakimbilia choo cha msikitini. Nikaingia hata mlango sijafunga nikaanza kumwaga oil. Jamaa mmoja aliingia akaanza kuongea kwamba mambo gani haya mtu anakojoa amesimama, nadhani na viatu niliingia navyo wenzangu wanaaacha nje. Nilstaajabu mno!

Ukitanga kuingia msalani msikitini jipange, uchuchumae.
 
Ng'ombe asimame
Mbuzi asimame
Mbwa asimame
Mweha asimame
Afu mm nichuchumae?
 
Unless unakojoa polini kwenye majani, sehemu yene mchanga mwingi au vile vyoo special vya juu hasa vinavyokuaga stand za mabasi au vyoo vya kulipia au vile vya shimo la moja kwa moja unaweza ukasimama, ila hivi vyoo vya sink na kwengineko ni uchafu mwanaume kukojoa umesemama.

Ukikojoa kwa kusimama Mkojo unaruka na kuingia kwenye nguo, ukutani na chombo cha karibu cha kuhifadhia maji au kunawia.

Pia ni vizuri kuosha zakali yako baada ya kukojoa, sio baada ya kukojoa unaiingiza tu kwenye suluali na kufunga zipu.

Pia hakikisha umemaliza kila kitu ndio unawe na kuiingiza ndani vinginevyo kuna vidogo vidogo vinavyobakia vinakua vinakuja taratibu mwishoni na unaweza usifahamu.

Naomba kuwasilisha
Sasa tofauti ya mwanaume na mwanamke iko wapi?acheni masihara kwa mambo sirious.
 
Kojoa ukiwa umelenga tundu la choo.

Hakikisha unaingiza dushe ndani ikiwa tayari umemaliza mkojo wote.
Kwasababu kuna vimkojo huwa vinabakia mwishoni pale, hivyo haviepukiki hata ukichuchumamaa kama mnavotaka wewe na mleta uzi.
Simple kihivyo tu, labda uwe huna akili nzuri ndo huo mkojo utakurukia wakati tundu unaliona.
Kwasababu kuna vimkojo huwa vinabakia mwishoni pale, hivyo haviepukiki hata ukichuchumamaa kama mnavotaka wewe na mleta uzi.

Hivyo vimkojo huwa havibaki ukiwa utavikamua kwa kujikohoza kohoza.
 
Hayo hata kwa mwanamke pia, Si mwanamme tu.

Mijanajike na mijana dume mingi haielewi usafi huo, wao ni kukojoa kwa kusimama tu na hawajioshi kabisa kwa maji, si wanawake wala wanaume. Hawana ustaarabu huo. Wana ustaarabu wa paka kunya mavi kujipaka.
Mwanaume kukojoa huku amechuchumaa ni utamaduni wa kiarabu kutokana na aina ya mavazi waliyovaa enzi hizo, ila kama suruali ina zipu huwezi kuchuchumaa eti unakojoa tu.
 
Kwenye vyoo vya bar siwaoni hao waislamu Safi wakikojoga kwa kuchuchumaa au wakiosha ninihii zao baada ya kukojoa ?
Muislamu safi halewi wala hazini.
Ukimuona huyo mtu ujue tu kwa wakati huo huyo mtu si Muislamu. Uislamu hua unavuka kama zinavyo vuka NGUO, wakati wa kufanya mambo hayo mpaka atakapo maliza.
Na ndio maana kifo kikikukuta umo ndani ya mambo hayo wewe ni Fiinaari huna msamaha.
 
Mara ya kwanza kuona mwanamme MTU mzima anakojoa amechuchumaa ni kipindi nasafiri na magari ya Tanga wakati wa kuchimba dawa porini.
Kuna mwingine alienda mbele zaidi badala ya kutingisha kengele yeye alimuosha abdala kichwa wazi.
Seriously watu wa Tanga hii ndio kitu gani mwanamme anakojoa amechuchumaa?
Basi sio huyo tu, rafiki yangu nae aliniadithia kwa mara ya kwanza aliwaona wanaume wanakojoa kwa kuchuchumaa na kuosha mali njia ya dsm kuelekea Dodoma .
 
Mwanaume kukojoa huku amechuchumaa ni utamaduni wa kiarabu kutokana na aina ya mavazi waliyovaa enzi hizo, ila kama suruali ina zipu huwezi kuchuchumaa eti unakojoa tu.
Wewe sio mstaarabu? Hivi unakojoa umesimama huku mikojo inakurukia halafu unasema ndio utamaduni mwema? Dah!
 
Back
Top Bottom