Hizi habari tuulize sisi Wanaume wenye dhakari. Nani amekwambia kukojoa kwa kusimama ni urijali ? Urijali haupimwi kwa kukojoa, kuna makhanithi wengi wanakojoa kwa kusimama.
Mimi mara nyingi nakojoa kwa kuchuchumaa kuliko kukojoa kwa kusimama na nikimaliza lazima nioshe Dhakari yangu,ikitokea sina maji basi nitatumia udongo, au mchanga, au majani au jiwe. Hii hutegemeana na mazingira ila kwetu sisi wanaume kukojoa kwa kuchuchumaa ni bora na kunapendeza zaidi kutokana na msingi wa kuepuka kupatikana mabaki ya mkojo katika nguo, sababu mkojo ni najisi.
Ukikojoa kwa kuchuchumaa dhakari inakuwa free sana ina kuwa ime relax mno, na mkojo unatoka katika hali tulivu na murua, kuliko ukiwa umesimama, ukiwa umesimama dhiki inakuwa kubwa na usipo kuwa makini unaweza kuubakiza mkojo.
Wote walio unga mkono kukojoa kwa kuchuchumaa, wanajua wanamaanisha nini na wako sahihi.
Mkojo ni uchafu na hutakwii ubaki nao. Kama huna maji basi tumia udogo, majani au jiwe, yaani kuosha dhakari baada ya kukojoa ni lazima.
Shukrani.