Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Wapi kwenye hivyo vyombo vya habari wamesema Papa kabariki ndoa za jinsia moja?Taarifa iliyotafsiriwa na hivyo vyombo kuwa inapingana na Papa?
Kama Papa angeagiza ndoa za jinsia moja zibarikiwe basi mimi ningekuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa kupinga. Ninachojua hakuna fundisho wala agizo la namna hiyo.
Hayo Mabaraza yalichoeleza ni msimamo wa Kanisa, ambapo hata kwenye agizo la Papa lipo. Sasa wanapoelezea msimamo wa Kanisa ambao ni kinyume ya kile walichokitengeneza (vyombo vya habari) kutokana na agizo la Papa ni lazima ionekane kuwa wanampinga, wakati kiuhalisia wanafafanua na kuongelea kilekile alichokiongea.
Wapi kwenye matamko ya hayo mabaraza wamesema hawatabariki ndoa za jinsia moja?
Alichokisema Papa na Vatican katika waraka wao ni kuruhusu kanisa katoliki kubariki mashoga (na nyinyi mnasema Papa ameruhusu kubariki mali/vitu vya mashoga tu na sio kuwabariki mashoga wenyewe, lakini hapo hapo mnakiri kuwa Mashoga wasitengwe na kanisa katoliki bali watendewe sawa sawa na wakatoliki wengine). Na vyombo vya habari vikaripoti tamko la Papa kuwabariki mashoga katika mtazamo huo. Na hayo mabaraza yakatoa tamko la kusema hawatabariki mashoga kwa namna yoyote ile kwa kuwa mashoga hawana nafasi ndani ya kanisa katoliki.