Ni wakati muafaka sasa Mbowe kuachana na mikutano ya Rais Samia

Ni wakati muafaka sasa Mbowe kuachana na mikutano ya Rais Samia

Izia maji

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
2,997
Reaction score
5,385
Kwa uamuzi huu wa Spika kuhusu kuendelea kwa Halima na wenzake 18 kuwa wabunge ni dhahiri dhahiri Samia na serikali yake hawaheshimu kabisa katiba iliyopo. Tumeshudia na kusikia Jaji Mkuu Prof. Juma akiamuru mahakama kutopingana na serikali vilevile tumemsikia Spika wa Bunge akisisitiza utiifu wake hoja zote za serikali, hivyo tusitegemee hata mara moja vyombo hivi viwili vya dola kutenda haki pindi serikali inapovunja katiba na sheria.

Bunge na Mahakama kwa sasa ni vyombo vya serikali kwa manufaa ya serikali. Hakuna tena mihimili mitatu ya dola bali kuna muhimili mmoja wa serikali.

Kwa hiyo nashauri Mbowe kuachana kabisa na mazungumzo na Samia na serikali yake kwa sababu hakuna kitakachoafikiwa kutekelezwa. Kinachofanywa na Rais kwa sasa ni kuonyesha unafiki wake kuwa ana nia njema ili serikali yake iendelee kupata uungwaji mkono na kupata misaada ya kimataifa katika kuiendesha. Mbowe atambue kwamba hata kufutiwa kwake mashtaka ya ugaidi ni mbinu ya Samia kujikosha mbele ya mataifa ya kigeni.

Samia anapenda sana kutalii nje ya nchi hivyo ili kupunguza kelele za madai ya utawala wa sheria, demokrasia na katiba mpya awapo kwenye utalii wake ambapo amepanga kutembelea nchi nyingi, kete yake kubwa ilikuwa kumwachia huru Mbowe.

Serikali ya Samia bado inaendeleza udikteta na kamwe haitaacha sera za ukandamizaji za mtangulizi wake Dikteta Magufuli!
 
Kwa uamuzi huu wa Spika kuhusu kuendelea kwa Halima na wenzake 18 kuwa wabunge ni dhahiri dhahiri Samia na serikali yake hawaheshimu kabisa katiba iliyopo. Tumeshudia na kusikia Jaji Mkuu ...
Kama maridhiano yanayoimbwa kuridhiwa ni yahila kiwango hiki na yenye kukosa uadilifu ni Bora kutokuwepo maridhiano hayo,pia yafaa watanzania Kwa umoja wetu tukemee tabia za ukosefu wa maadili ,zinazo ratibiwa Kwa manufaa ya makundi ya wachache katika Chama na serikali.
 
covid 19 wanahitajika kwa sababu mbili..ule msaada wa european union WA EUROS ZA KUTOSHA BUNGENI unaohitaji idadi fulani ya wapinzani kwenye kamati zabunge wakati huo kuna watu waliiiba kura kupitiliza na kukosesha idadi

Pili inadhaniwa kwamba hii situation italeta mgawanyiko chadema kumbe IMEWAGEUZA WATU WENYE"HESHIMA ZAO" KUWA VITUKO
 
Katika diplomasia za watu wanaojua mambo ya itifaki za mikutano, mikutano ya wakuu huwa inaandaliwa na watu wa chini kabisa, wanaandaa ajenda.

Halafu inapanda kwa watu wa kati, wanaipitia ajenda na kuiongeza, au kuipunguza.

Halafu inakwenda kwa watu wa juu, wanaihakiki tena ajenda na vifungu vyake. Wanafikia makubaliano.

Halafu ndiyo wanakutana viongozi wenyewe, kusaini tu makubaliano.

Ukisikia Reagan kakutana na Gorbachev, ujue kuna mikutano mingi sana ishafanyika awali hapo. Ndiyo maana mkutano huu unaitwa "summit", kilele cha mlima. Maana yake huko chini kuna mlima mrefu sana.

Mfumo huu unatoa nafasi sehemu kukitokea kukosa kuelewana kuwepo na namna ya kuhusisha wakubwa zaidi, na kupata muafaka.

Mikutano ya Mbowe na Rais Hassan haikufuata mfumo huu wa summit.

Mikutano hii imefuata mfumo wa mikutano ya Trump na Kim Jong Un.

Yani, mikutano imeanza kwa viongozi wakuu, bila kuanzia kwa watu wa chini.

Maana yake, viongozi wakuu wakikosa makubaliano, hakuna namna ya ku appeal kwa wakubwa wao kutafuta muafaka.

Hii ni moja ya tofauti kubwa iliyofanya mikutano ya Reagan na Gorbachev ifanikiwe, na mikutano ya Trump na Kim Jong Un isifanikiwe.
 
Katika watu ambao hawakufurahishwa wala kuunga mkono ziara za Mbowe ikulu, mimi ni mmojawapo. Nilijua fika Samia anamtumia Mbowe kama kinga ya utawala wake wa kihuni.

Nilifika mahali pa kusema kuwa Mbowe hastahili tena kuwa mwenyekiti wa cdm kwani ameshachoka. Ccm hawataki muafaka, bali wanataka kuogopwa kwa kukaa madarakani bila ridhaa ya umma. CDM kuendelea kumtegemea Mbowe kama mwenyekiti wa chama ni kosa kubwa la kiufundi.
 
Shida ni kwamba viongozi wa chadema wana watu wao wanaotaka wawe wabunge, mmoja wa huyo mtu ni Joyce Mukya
Ni ujinga wa kiwango cha 4G kudhani kuwa kuna mwanasiasa anapigania maslahi yangu, wote wapo hapo kupigania matumbo yao, ya wake na watoto zao, ya vimada zao, ndugu zao, marafiki zao kimpango wao,… watuache na shida zetu.
 
Kwa uamuzi huu wa Spika kuhusu kuendelea kwa Halima na wenzake 18 kuwa wabunge ni dhahiri dhahiri Samia na serikali yake hawaheshimu kabisa katiba iliyopo. Tumeshudia na kusikia Jaji Mkuu Prof...
shida ni ubunge tuu ama ni nini
 
Katika watu ambao hawakufurahishwa wala kuunga mkono ziara za Mbowe ikulu, mimi ni mmojawapo. Nilijua fika Samia anamtumia Mbowe kama kinga ya utawala wake wa kihuni. Nilifika mahali pa kusema kuwa Mbowe hastahili tena kuwa mwenyekiti wa cdm kwani ameshachoka. Ccm hawataki muafaka, bali wanataka kuogopwa kwa kukaa madarakani bila ridhaa ya umma. CDM kuendelea kumtegemea Mbowe kama mwenyekiti wa chama ni kosa kubwa la kiufundi.
Birds of the same feathers flock together, not less or more but precisely.
 
Ikumbukwe kuwa mbowe anawasilina na muhimili mmoja tu bunge na mahakama Ni mihimili mingine tu afanye namna alutane na mhimili bunge na mahakama
 
Nakumbuka juzi kati nilikwenda kwa rafiki yangu kufika kwake nikashangaa kukuta mbwa wa rafiki yang akijaribu kumdhibiti mwenye mbwa ambae ndio rafiki angu 😂😂😂🤣, oh samahani nipo nje ya mada. Sasa mleta mada unatakiwa uelewe kuwa mwenyekiti wa chama ndio mwenye maamuzi ya mwisho, hakuna chawa wala mtu yeyote mwenye uwezo au mamlaka ya kumpangia. Mleta mada kama unaona mambo yako hayakuendei huku chamani basi kaanzishe chako au ujiunge na act wazalendo.
 
Nakumbuka juzi kati nilikwenda kwa rafiki yangu kufika kwake nikashangaa kukuta mbwa wa rafiki yang akijaribu kumdhibiti mwenye mbwa ambae ndio rafiki angu 😂😂😂🤣, oh samahani nipo nje ya mada. Sasa mleta mada unatakiwa uelewe kuwa mwenyekiti wa chama ndio mwenye maamuzi ya mwisho, hakuna chawa wala mtu yeyote mwenye uwezo au mamlaka ya kumpangia. Mleta mada kama unaona mambo yako hayakuendei huku chamani basi kaanzishe chako au ujiunge na act wazalendo.
Akili za mpumbavu utaziona bila chenga!
 
Back
Top Bottom