Kwa uamuzi huu wa Spika kuhusu kuendelea kwa Halima na wenzake 18 kuwa wabunge ni dhahiri dhahiri Samia na serikali yake hawaheshimu kabisa katiba iliyopo. Tumeshudia na kusikia Jaji Mkuu Prof. Juma akiamuru mahakama kutopingana na serikali vilevile tumemsikia Spika wa Bunge akisisitiza utiifu wake hoja zote za serikali, hivyo tusitegemee hata mara moja vyombo hivi viwili vya dola kutenda haki pindi serikali inapovunja katiba na sheria.
Bunge na Mahakama kwa sasa ni vyombo vya serikali kwa manufaa ya serikali. Hakuna tena mihimili mitatu ya dola bali kuna muhimili mmoja wa serikali.
Kwa hiyo nashauri Mbowe kuachana kabisa na mazungumzo na Samia na serikali yake kwa sababu hakuna kitakachoafikiwa kutekelezwa. Kinachofanywa na Rais kwa sasa ni kuonyesha unafiki wake kuwa ana nia njema ili serikali yake iendelee kupata uungwaji mkono na kupata misaada ya kimataifa katika kuiendesha. Mbowe atambue kwamba hata kufutiwa kwake mashtaka ya ugaidi ni mbinu ya Samia kujikosha mbele ya mataifa ya kigeni.
Samia anapenda sana kutalii nje ya nchi hivyo ili kupunguza kelele za madai ya utawala wa sheria, demokrasia na katiba mpya awapo kwenye utalii wake ambapo amepanga kutembelea nchi nyingi, kete yake kubwa ilikuwa kumwachia huru Mbowe.
Serikali ya Samia bado inaendeleza udikteta na kamwe haitaacha sera za ukandamizaji za mtangulizi wake Dikteta Magufuli!