Ni wakati wa kutoa ultimatum kwa watawala, bila Katiba Mpya ya wananchi hakuna uchaguzi

Nikajua utasema bila ofs mpya ufipa Mwenyekiti aondoke
Mkigoma uchaguzi tutaendelea nao kwa mjibu wa katiba
 
Usitishe watu. Tutayasema haya usiku na mchana, kwenye vyombo vya habari na hata sehemu za wazi kama barabarani au majukwaani.

Kama umezoea kutisha watu, umepitwa na wakati. Ulimwengu wa leo siyo wa kumtisha yeyote.

Nani amekutisha.?

Nimetaka utoke hadharani na sio unajificha kwenye keyboard
 
Bams upo sahihi ✔️ Je uvccm watakuelewa?
 
Kama tunakubaliana kila baya na jema lina watu wake, basi hapo moja kwa moja tumeshakubaliana pia kwamba, hata wale wananchi ambao watakuwa wagumu kuiunga mkono hiyo ultimatum nao watakuwa na haki, bila kujali kama kwa mtazamo wa wengine wako sawa, au hapana, ndivyo haki ya kuchagua ilivyo.

Baada ya kusema hayo, sasa hebu tuoneshe hapa, ni njia gani itakayotumika kuyaunganisha hayo makundi uliyoyataja hapo juu, mbaya zaidi pale ulivyotolea mfano vyama vya wafanyakazi, ambavyo kimsingi ni mali ya serikali ya CCM, na mengine kwenye kufanikisha hilo?

Nauliza hivyo kwasababu moja ya kimazingira, kwamba imeshathibitika, kuna kasumba ya kuogopa kuliunga mkono jambo lolote litakaloonekana kwenda kinyume na watawala, hii inasababishwa na adhabu (mazingira magumu), wanayotengenezewa wale wanaoonekana kuunga mkono uelekeo wa upinzani, hasa kwenye utekelezaji wajukumu yao.

Sasa kwa hii ultimatum uliyotuletea na unayopendekeza hapa, na kwa kuzingatia ugumu wa mazingira kama nilivyokuonesha hapo juu, niambie utayaunganisha vipi hayo makundi ili yasiogope vitisho vya CCM na athari zake kwao? kwasababu nionavyo kiuhalisia na mazingira hapa tulipo, hii ultimatum yako haitekelezeki..
 
Kasoro Marekani (USA); lakini hata wao, kuna mambo mengi sana waliyolazimishwa na matakwa ya wananchi, na serkali ikatii. Hapa kwetu ni serikali( hapana Rais) ndiyo inayotuamrisha tufanye nini!
Hapakwetu ni mwendo wa kutii maagizo tu
 
Mkuu 'Sandinista', safari hii tumefika kwenye 'tipping point'; mabadiliko haywezekani kuzuiwa tena kwa njia yoyote.

Samia kajaribu kutumia hadaa, lakini watu tayari wameona ulaghai unaofanyika waziwazi, kwa hiyo wataukataa.

Wewe uliamini huko mwanzo kwamba Samia ni mtu wa "maono"? Kwa alama zipi alizoonyesha hadi ukazolewa akili kiasi hicho?

Tokea mwanzo, huyu rais amekuwa ni mtu mwenye kuyumbayumba tu. Historia yake, hata katika lile Baraza la Katiba lililoshindikana, yeye akiwa na Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo, ukiangalia utaona kwamba yeye alikuwa ni mmoja wa hao wasiotaka mabadiliko huko ndani ya katiba mpya. Kwa hiyo siyo sahihi kudhani kuwa wakati huu anayumbishwa na yeyote kuhusu swala hilo.
 
Najiuliza tu, hivi kila Mtanzania akianza kupiga mawe mbunge wake na mawaziri wezi huku mitaani CCM hawatakubali kweli kutuletea katiba Mpya? Naona tuanzie hapa.
 
😆😆😆 Kuongea hayo mambo ukiwa umejificha Kwenye keyboard ni very easy

Toka nje, simama pale kariakoo then sema hayo uliyoandika, hapo ndio tutajua kweli Una maanisha

Lazima ajifiche maana anaweza kuuwawa, hivyo ni lazima atangeneze hamasa kwanza. Kwani hao wanaofanya mabadiliko ya kimifumo yasiyotakiwa na walioko madarakani huwa wanajitokeza hadharani kuhubiri hayo?
 
Samahani kama naingilia hoja zenu, mkuu 'denoo J', lakini ningependa kujua maoni yako kuhusu nini kifanyike badala ya hayo anayopendekeza Bams.

Kwa maoni yangu, kazi ya kuzuia uchaguzi usifanyike hauhitaji watu wote washiriki katika kuzuia zoezi hilo. Vile vile, kama sote tunavyojua, kuzuia uchaguzi usifanyike kunaweza kuwa kwa njia mbalimbali.

Nadhani jambo ambalo mkuu 'Bams' hakuligusia katika mada yake ya "wananchi kutoa 'ultimatum...' ni swala la nani hasa atakuwa anaongoza juhudi hizo na kuwaunganisha wananchi watimize lengo hilo la kuzuia uchaguzi. Ni dhahiri bila ya uwepo uongozi wa wananchi hao, kamwe haiwezekani wafikie lengo hilo, kwanza halitakuwa lengo, kwa sababu hapatakuwepo na walioliasisi lengo lenyewe.

Ndiyo maana, baada ya kusoma kichwa cha mada aliyotumia kabla sijasoma aliyokuwa amewasilisha ndani ya mada yenyewe, nikadhani kachukua yale yale waliyokwishayaamua CHADEMA, kama chama kuhusu hiyo Katiba Mpya; na mchango wangu wa kwanza kwenye mada hii utaona iliegemea huko, kuwa wananchi hawa watakuwa wanatimiza adhma ile ile waliyokwisha idhamiria CHADEMA kuitimiza.

Kwa hiyo, kwa maana hiyo, nikachukulia kwamba itakuwa ni kazi ya chama hicho, na wengine wote watakaopenda kuungana kulisimamia jambo hilo na kulifikisha kwa wananchi na kuwaongoza, na kuwaunganisha pamoja wakisimamia zoezi hilo lifanyike kwa ufanisi.
Nina hakika CHADEMA na wengieo wakipenda kuifanya kazi hiyo vizuri na kuifikisha kwa wananchi, safari hii inawezekana kabisa kuzima hizi njama za kila mara zinazofanywa na CCM

Kuzuia uchaguzi usifanyike ni zoezi linalohitaji kufanyiwa kazi tu kwa mipango inayoeleweka. Hapahitajiwi zaidi ya watu milioni moja kutimiza zoezi hilo kwa ufanisi mkubwa, kama wananchi walisha elimishwa vya kutosha wasishiriki kwenye uchaguzi batili.
Kubaki tu nyumbani bila kwenda kwenye kituo cha kupigia kura, hiyo ni sehemu moja tu ya kuzuia uchaguzi usifanyike. Watu wanaoelewa maana ya kufanya hivyo ni nini, hawataweza kusita kuunga mkono hatua hiyo ndogo wanayotakiwa kushiriki ili kuleta mabadiliko ndani ya nchi yao.
 
Najiuliza tu, hivi kila Mtanzania akianza kupiga mawe mbunge wake na mawaziri wezi huku mitaani CCM hawatakubali kweli kutuletea katiba Mpya? Naona tuanzie hapa.
EEEeeeHEEEE!

Wewe jamaa siyo 'Mbishi', tu, bali una la ziada! Hili wazo lako hapa, huoni kwamba unataka kwenda kulipiza tu kisasi kwa yule Jamaa wa V8 aliyekupora mpenzi wako kweli?
 
LOoooh!

Unayo aina yako maalum ya kuwasilisha ujumbe.

Hapa umetoa 'HINT, sijui kama wengi wataelewa ulichokusudia kukifikisha.'
 
LOoooh!

Unayo aina yako maalum ya kuwasilisha ujumbe.

Hapa umetoa 'HINT, sijui kama wengi wataelewa ulichokusudia kukifikisha.'
Hatujalala.

Miaka zaidi ya 60 sirikali chini ya CCCM haijawatosha kuandika KATIBA mpya.

Wasipewe muda zaidi sababu wamezeeka!!!!!
 
Hapana, sijakosea kamwe mkuu 'Bams', kuwataja CHADEMA katika zoezi hilo. Labda tu useme kwamba na wengine watakaoungana nao kulifanikisha jambo hilo.

Huwezi kuwataja wananchi kiujumla, bila wananchi hao kuwa na uongozi unaosimamia na kuratibu juhudi za wananchi hao.
CHADEMA hapa tayari wao walikwishjipambanua kuwa zoezi hilo ndilo mpango utakaotumika.

Kwa mwananchi yeyote au taasisi nyingine yeyote kuunga mkono, au kuungana na CHADEMA katika lengo hilo, haina maana ya kwamba wamekubali mambo mengine yoote ya CHADEMA kama chama cha siasa, bali wanaungana nao katika juhudi za pamoja katika lengo hili la Katiba Mpya na kuzuia uchaguzi usifanyike bila kuwepo Katiba Mpya.

Na kwa kweli siyo lazima CHADEMA wahodhi dhana hiyo ya kutoa 'ultimatum', wao kazi kubwa ni kuratibu na kuunganisha juhudi za wananchi kufikia lengo hilo.

Wananchi kwa ujumla wao hawawezi kamwe kufanya lolote bila uwepo na uongozi unaowaweka pamoja wananchi na kusimamia mipango ya wananchi hao kwenye zoezi husika.
 
Ukitaka zoezi lisifanyike at the same time uwe tayari kuruhusu wengine washiriki na wengine wasishiriki, maana yake hao watakaoshiriki watahalalisha hilo zoezi hivyo ultimatum yenu kukosa maana.

Kwangu kwa namna mleta mada alivyoleta mada yake, na makundi aliyoyahusisha, kama vyama vya wafanyakazi na wakulima, ambavyo kimsingi ni mali ya CCM na serikali yake, hili zoezi la ultimatum haliwezi kufanyika, na kama likifanyika, basi manufaa yatakuwa upande wa watawala kwa kupata uungwaji mkono mkubwa upande wao.

Hata hapo ulipowagusia Chadema kuongoza njia, napo utapoteza maana ya hili suala, kwasababu hapo tayari yale madai ya Katiba Mpya sio ya wanasiasa yatapata nguvu, na CCM pia watasema sio ya wapinzani hasa Chadema, hapa lazima pawepo na makundi mengine yatakayokuja front, na bahati mbaya, makundi hayo yako upande wa CCM mpaka sasa, kwa hofu au kupenda.
 
Nakiri, leo hii umeongeza ufahamu wangu juu ya yale niliyokuwa siyajui.
Huwa kuna baadhi ya watu ambao huwa wanatoa lawama na shutuma kuhusu Mwalimu Nyerere kumtumia Rashid Mfaume Kwawa, lakini nilikuwa sijui chanzo wala sababu hasa za hao watu kufanya hivyo. Leo umeniwezesha kuunganisha 'dots' ambazo zilikuwa haziungani. Ninatoa shukrani kwa elimu hii uliyoniongezea hapa.
Niseme pia kwamba, hali hiyo ya Mwalimu Nyerere kushawishi wajumbe ikajirudia tena kwa Mkapa; lakini ikashindikana kwa Salim Ahmed Salim..., na baadae ushawishi huo huo ndio ukaruhusu uwepo wa vyama vingi vya siasa, pamoja na kwamba wananchi hawakuafiki walipoulizwa wakati ule.

Kwa mengine yote ninakubaliana nawe, kwamba CCM ya leo ni tofauti kabisa na ile ya wakati wa Mwalimu.
 
Ukitaka zoezi lisifanyike at the same time uwe tayari kuruhusu wengine washiriki na wengine wasishiriki, maana yake hao watakaoshiriki watahalalisha hilo zoezi hivyo ultimatum yenu kukosa maana.
EeeenHeeeee!

Niongeze kwamba:

Hiyo ndiyo Demokrasia sahihi.

Mkuu 'denoo J', bila ya kutaka kuingia kwenye malumbano hapa kwenye mada hii, niseme kwamba hicho kinachopingwa, kinachofanywa na CCM siyo Demokrasia hiyo, au unaonaje?
Kukipinga kisicho halali kwa njia yoyote ile haiwezekani njia hiyo ikawa haram na hicho kinachopingwa kikawa halali.

Hili ninaliachia hapa, mkuu wangu. Silijadili tena zaidi ya hapa.
 
Samahani, ilinibidi nirudi, pamoja na ile ahadi niliyoitoa hapo juu. Nimerudi kwa sababu nilikuwa sijasoma hadi huku mwisho. wa andiko lako. ambapo nilipomaliza kulisoma nikajiuliza:
Sasa unapendekeza tufanye nini. Yaani waTanzania tufanye kitu gani zaidi ya haya yanayopendekezwa? AU tubaki tu vile vile tulivyo sasa?
 
Lazima ajifiche maana anaweza kuuwawa, hivyo ni lazima atangeneze hamasa kwanza. Kwani hao wanaofanya mabadiliko ya kimifumo yasiyotakiwa na walioko madarakani huwa wanajitokeza hadharani kuhubiri hayo?

Hii tension mnatengeneza Tu wenyewe bila maana yoyote

Nani awauwe.? Kwanini msiuliwe mnavyoongea kwenye mtandao?
 
Hii tension mnatengeneza Tu wenyewe bila maana yoyote

Nani awauwe.? Kwanini msiuliwe mnavyoongea kwenye mtandao?
Utauliwa kwenye mitandao kwa hizi fake I'd. Ingekuwa ni verified user hapo sawa. Kwa hizi fake I'd unajua ni nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…