Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usitishe watu. Tutayasema haya usiku na mchana, kwenye vyombo vya habari na hata sehemu za wazi kama barabarani au majukwaani.
Kama umezoea kutisha watu, umepitwa na wakati. Ulimwengu wa leo siyo wa kumtisha yeyote.
Bams upo sahihi ✔️ Je uvccm watakuelewa?Ifike wakati Watanzania tutoe amri kwa watawala kwamba kama hakuna katiba mpya, hakuna uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024, wala uchaguzi mkuu mwaka 2025.
Nchi hii ni ya Watanzania. Watanzania ndio wanaotakiwa kuwa na maamuzi ya namna gani wanataka nchi yao ifanye kila kitu.
Katiba hii ambayo Baba wa Taifa alisema inamfanya Rais kuwa dikteta sasa ifike mwisho. Rais anatakiwa kupewa mwongozo tuliokubaliana namna anavyotakiwa kutuongoza, na siyo yeye kutupangia namna anavyotaka kututawala kama ilivyo sasa.
Leo hii kila kitu ni Rais, kama vile nchi ni ya Rais. Kodi ni ya mwananchi, lakini Rais ndiye anakuletea mkurugenzi kuja kusimamia matumizi ya pesa yako. Hata ukiona huyo mkurugenzi anaiba, wewe unayetoa pesa huna uamuzi, mpaka aliyemteua apende, asipopenda, mteule wake anaendelea kutafuta pesa ya wananchi na hamna uwezo wa kumfanya chochote.
Fikiria, mpaka pesa ya wananchi, siku hizi inatajwa kuwa ni pesa ya Rais, eti Rais emetoa bilioni kadhaa kwaajiki ya ujenzi wa kisima, zahanati, shule, n.k.
Hata huko kwenye mataifa yenye katiba nzuri, sheria nzuri na mifumo mizuri ya utawala, siyo kwamba watawala walikuwa malaika, bali pressure ya wananchi iliwalazimisha watawala kukubali matakwa ya wananchi.
Kwa kuwa Serikali inalegalega, na kupiga danadana nyingi kuhusiana na suala la katiba nzuri mpya, katiba ya wananchi, lazima nguvu ya wananchi ishike hatamu, na Serikali ilazimishwe kufuata matakwa ya wananchi.
Na kwenye hili wananchi tushikamane, tuache mambo ya uCHADEMA, uCCM, uCUF, uACT, au tofauti zile nyingine za kijinga eti huyu ni sukuma gang, yule ni msoga gang, nasema huo ni upuuzi, sote tuunganishwe na utaifa wetu.
Leo mmesikia kuwa TANESCO, inayoendeshwa kwa ruzuku ya Serikali ya bara (nishati siyo suala la muungano) imesamehe deni la zaidi ya shilingi bilioni 60 iliyokuwa ikiidai Zanzibar. Hizi ni pesa za wananchi walipa kodi. Msamaha huo umetolewa kwa namna gani? Ni utaratibu upi uliofuatwa? Ni nani aliyetoa uamuzi wa kusamehe hilo deni? Ana mamlaka hayo?
Mambo haya inawezekana yanafanywa ama kwa shinikizo ama kwa kujipendekeza kwa Rais kwa sababu ni mzanzibari. Hatupingi kusamehe deni, tena kwa sehemu mojawapo ya muungano au kutoa msaada inapolazimu, lakini ni utaratibu upi umefuatwa kwa shirika linaloendesha kwa pesa za walipa kodi kuweza kufuta deni? Mbona hatujawahi kusikia kuwa TANESCO imewafutia deni wadaiwa sugu wa huku bara?
Katiba mpya itayaweka haya mambo yote wazi, na kuweka taratibu zilizokubalika na ambazo kila mmoja, na hasa viongozi, watatakiwa kufuata.
Hii ya kila kitu Rais, haikubaliki kabisa kwa namna yoyote ile. Kwenye teuzi, Rais aishie kuwateua mawaziri tu ambao wataidhinishwa na wabunge. Wengine wote waajiriwe au wachaguliwe. Wakivurunda, mamlaka za uajiri ziwafukuze kiurahisi.
Katiba siyo ya akina Lisu na Mbowe, siyo ya Rais wala Mutungi, siyo ya Chongolo, bali ni ya Watanzania wote. Yeyote anayetaka kujimilikisha uandaaji wa katiba ni adui yetu sote. Yeyote anayetaka kutushirikisha sote kwenye kupata katiba tunayoitaka, ni mzalendo wa Taifa letu, ni mtu mwenye upendo kwa Watanzania wa leo na vizazi vijavyo, na huyo ndiye tuandamane naye.
Hatutaki katiba maslahi ya watawala au wanasiasa tu, bali katiba itakayompa mamlaka makubwa mwananchi.
Kama tunakubaliana kila baya na jema lina watu wake, basi hapo moja kwa moja tumeshakubaliana pia kwamba, hata wale wananchi ambao watakuwa wagumu kuiunga mkono hiyo ultimatum nao watakuwa na haki, bila kujali kama kwa mtazamo wa wengine wako sawa, au hapana, ndivyo haki ya kuchagua ilivyo.Hakuna kibaya kisicho na wa kukiunga mkono.
Leo hii hata tukitaka kuweka utaratibu utakaowafanya viongozi wasitumie vibaya oesa ya Serikali, wapo ambao watataka hilo lisitokee, kwa sababu wao ni wanufaika ni mianya hiyo ya sheria.
Hata hii katiba yetu mbaya tuliyo nayo sasa, wapo wanufaika wengi wa moja kwa moja na wengine indirectly. Hao hawawezi kuwa nasi katika kuweka utaratibu ambao wao watakuwa hawana uhakika kama wataendelea kunufaika kama ilivyo sasa.
Wapi pa kuanzia kutoa ultimatum, nionavyo ni kwa kupitia taasisi mbalimbali mbalimbali, vyama vya siasa, vyama vya kitaluma, vyama vya wafanyakazi, vyama vya wakulima, majukwaa mbalimbali, n.k. Hawa wakishatoa matamko ya kitaka Serikali kuliweka suala la katiba mpya kwenye top priority, inakuwa tayari ni hatua.
Hakuna mapambano yasiyo na kiongozi. Na kwenye hili tayari CHADEMA wameonesha kuchukua nafasi ya uongozi. Kuwa kiongozi kuna gharama kubwa, na siyo kila mtu anaweza kuwa kiongozi, hasa kwenye mapambano. Kwa hiyo ni vema kuwaunga mkono CHADEMA kwenye hoja hii ya katiba maana wanalo jukwaa tayari, tena jukwaa kubwa.
Hapakwetu ni mwendo wa kutii maagizo tuKasoro Marekani (USA); lakini hata wao, kuna mambo mengi sana waliyolazimishwa na matakwa ya wananchi, na serkali ikatii. Hapa kwetu ni serikali( hapana Rais) ndiyo inayotuamrisha tufanye nini!
Mkuu 'Sandinista', safari hii tumefika kwenye 'tipping point'; mabadiliko haywezekani kuzuiwa tena kwa njia yoyote.SSH aliposhika madaraka ya uongozi wa nchi yetu wengine tuliamini alikuwa na maono ingawa hatukuwa na uhakika aliona mbali kiasi gani na alijiamini kiasi gani katika maono yake hayo. Hata hivyo taratibu alianza kubadilisha mwelekeo kiasi cha kupelekea vurugu nyingi ya kuvunja vikao vya ndani vya vyama shindani. Bila shaka hili lilitokana na ushauri wa kiusalama uliotolewa wenye lengo la kudhibiti vuguvugu la mabadiliko. Hitimisho la ushauri huo wa kusambaratisha vuguvgu la mabadiliko ni ile kesi ya ugaidi.
Tunaweza kusema kuwa mfumo ulifanikiwa kumbadilisha maono ya SSH na pengine hata kumkaripia kuwa maono yake yangepelekea kukabidhi nchi kwa "mabeberu"! Kwa sasa tunaweza kusema kimwelekeo tumepiga "U" turn. Wakati huo tumeaminishwa kuwa yapo mazungumzo ya maridhiano yanaendelea ingawa yanahusisha vyama viwili vikibwa tu. Tulitegemea msingi wa maridhiano endelevu ni katiba mpya. Wengine tumekuwa tukidhani agenda mojawapo ya hayo mazungumzo ya maridhiano ni kutafuta makubaliano kuhusu mchakato adilifu na wa wazi wa kufuata ili kupata katiba mpya bora. Kinyume chake tumetangaziwa kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa itaratibu hiyo kazi. Wakati huo huo mmoja wa wale tulioambiwa wanaridhiana akatangazi kutokuwa na imani na mpango huo!
Ndiyo kusema yale mazungumzo ya maridhiano yamesambaratika! Tunarudi kwenye zama za giza! Kwa mwendo huu hakika 2024 na 2025 tutashuhudia uchafuzi mbaya zaidi kuliko hata ule wa 2019 na 2020. Uchafuzi ujao utakuwa mbaya zaidi kwa sababu moja kubwa. Tofauti na kipindi cha nyuma ambapo kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa akitoa amri, safari hii amri zitakuwa zinatolewa na watu wengi kama ambavyo tumekuwa tukiona: wapambe, machawa na wale wote waliopewa au kujipa kazi ya kuuhami na kuupigania utawala uliopo madarakani ikiwa ni pamoja na kuuwezesha kupata kipindi kingine. Kufikia hapo tumuombe sana Mungu atuwezeshe kupata busara na kufanya tafakuri ya kina kuhusu mustakabali wa nchi yetu. Tuwaombee viongozi wetu wa kiroho wapate hekima na ujasiri wa kututangulia katika hili. Mwaka 2014 kuna umoja wa madhehemu ya dini ulijitokeza hadharani kutoa kauli kuwa wasingeunga mkono Katiba Pendekezwa na kwamba muda wa kura ya maoni utakapofika wao wangeendesha kampeni ya kupinga hiyo Katiba Pendekezwa. Baadhi yetu tunaamini msimamo ule uliponya taifa. Mtazamo huo unahitajika zaidi sasa wakati ambapo tofauti na huko nyuma mgawanyiko wa kitaifa unaongozeka.
😆😆😆 Kuongea hayo mambo ukiwa umejificha Kwenye keyboard ni very easy
Toka nje, simama pale kariakoo then sema hayo uliyoandika, hapo ndio tutajua kweli Una maanisha
Samahani kama naingilia hoja zenu, mkuu 'denoo J', lakini ningependa kujua maoni yako kuhusu nini kifanyike badala ya hayo anayopendekeza Bams.Sasa kwa hii ultimatum uliyotuletea na unayopendekeza hapa, na kwa kuzingatia ugumu wa mazingira kama nilivyokuonesha hapo juu, niambie utayaunganisha vipi hayo makundi ili yasiogope vitisho vya CCM na athari zake kwao? kwasababu nionavyo kiuhalisia na mazingira hapa tulipo, hii ultimatum yako haitekelezeki..
EEEeeeHEEEE!Najiuliza tu, hivi kila Mtanzania akianza kupiga mawe mbunge wake na mawaziri wezi huku mitaani CCM hawatakubali kweli kutuletea katiba Mpya? Naona tuanzie hapa.
LOoooh!MNYIKA amekuwa akiirudia sana kauli hiyo.
Bila KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi hautafanyika uchaguzi wowote.
Sanduku la kura limeporwa na halijulikani lilipo,
Wananchi tunasubiri Kwa hamu kupiga KURA YA WAZI viwanjani na mabarabarani.
Tusubiri.
Hatujalala.LOoooh!
Unayo aina yako maalum ya kuwasilisha ujumbe.
Hapa umetoa 'HINT, sijui kama wengi wataelewa ulichokusudia kukifikisha.'
Hoja yako ni nini hapa? Helkopta inazuia katiba kupatikana?Kama wananchi wanataka katiba mpya mnazunguka na helikopta kutafuta nini?
Hapana, sijakosea kamwe mkuu 'Bams', kuwataja CHADEMA katika zoezi hilo. Labda tu useme kwamba na wengine watakaoungana nao kulifanikisha jambo hilo.Umenena vema ila hapo mwishoni, kusema CHADEMA wajipange siyo sahihi. Bali tuseme kuwa wananchi wote tunatakiwa tujipange. Kama katiba tunayoitaka ni kwaajili ya wananchi, na tunaoitaka ni sisi wananchi, kwa nini tuseme CHADEMA pekee ndiyo wajipange? Tunaishukuru CHADEMA kwa kusimama mbele na kuwa kinara katika hili, lakini nguvu na msukumo wa wananchi wote wazalendo, ni muhimu zaidi.
Ukitaka zoezi lisifanyike at the same time uwe tayari kuruhusu wengine washiriki na wengine wasishiriki, maana yake hao watakaoshiriki watahalalisha hilo zoezi hivyo ultimatum yenu kukosa maana.Samahani kama naingilia hoja zenu, mkuu 'denoo J', lakini ningependa kujua maoni yako kuhusu nini kifanyike badala ya hayo anayopendekeza Bams.
Kwa maoni yangu, kazi ya kuzuia uchaguzi usifanyike hauhitaji watu wote washiriki katika kuzuia zoezi hilo. Vile vile, kama sote tunavyojua, kuzuia uchaguzi usifanyike kunaweza kuwa kwa njia mbalimbali.
Nadhani jambo ambalo mkuu 'Bams' hakuligusia katika mada yake ya "wananchi kutoa 'ultimatum...' ni swala la nani hasa atakuwa anaongoza juhudi hizo na kuwaunganisha wananchi watimize lengo hilo la kuzuia uchaguzi. Ni dhahiri bila ya uwepo uongozi wa wananchi hao, kamwe haiwezekani wafikie lengo hilo, kwanza halitakuwa lengo, kwa sababu hapatakuwepo na walioliasisi lengo lenyewe.
Ndiyo maana, baada ya kusoma kichwa cha mada aliyotumia kabla sijasoma aliyokuwa amewasilisha ndani ya mada yenyewe, nikadhani kachukua yale yale waliyokwishayaamua CHADEMA, kama chama kuhusu hiyo Katiba Mpya; na mchango wangu wa kwanza kwenye mada hii utaona iliegemea huko, kuwa wananchi hawa watakuwa wanatimiza adhma ile ile waliyokwisha idhamiria CHADEMA kuitimiza.
Kwa hiyo, kwa maana hiyo, nikachukulia kwamba itakuwa ni kazi ya chama hicho, na wengine wote watakaopenda kuungana kulisimamia jambo hilo na kulifikisha kwa wananchi na kuwaongoza, na kuwaunganisha pamoja wakisimamia zoezi hilo lifanyike kwa ufanisi.
Nina hakika CHADEMA na wengieo wakipenda kuifanya kazi hiyo vizuri na kuifikisha kwa wananchi, safari hii inawezekana kabisa kuzima hizi njama za kila mara zinazofanywa na CCM
Kuzuia uchaguzi usifanyike ni zoezi linalohitaji kufanyiwa kazi tu kwa mipango inayoeleweka. Hapahitajiwi zaidi ya watu milioni moja kutimiza zoezi hilo kwa ufanisi mkubwa, kama wananchi walisha elimishwa vya kutosha wasishiriki kwenye uchaguzi batili.
Kubaki tu nyumbani bila kwenda kwenye kituo cha kupigia kura, hiyo ni sehemu moja tu ya kuzuia uchaguzi usifanyike. Watu wanaoelewa maana ya kufanya hivyo ni nini, hawataweza kusita kuunga mkono hatua hiyo ndogo wanayotakiwa kushiriki ili kuleta mabadiliko ndani ya nchi yao.
Nakiri, leo hii umeongeza ufahamu wangu juu ya yale niliyokuwa siyajui.Ndugu yangu Kalamu, tukitaka kuwa wakweli wa nafsi zetu, na hasa sisi wa umri wa Pascal Mayala na zaidi, ni dhahiri wakati wa mfumo wa chama kimoja, kulikuwa na demokrasia ya kuwango fulani (ukiacha demomrasia ya vyama vingi) kuliko ilivyo sasa.
Hata kwenye uchaguzi (ukiacha zile kura za Rais za ndiyo au hapana), kwenye ubunge na udiwani, kulikuwa na uchaguzi halisia. Wagombea walitakiwa kusafiri kwenye gari moja, kulala chumba kimoja, kula pamoja; yote ilikuwa kuhakikisha hakuna rushwa ya aina yoyote au mbinu chafu. Aliyetangazwa kuwa mbunge, ni kweli alikuwa amechaguliwa na wananchi.
Vikao ndani ya chama, vilikuwa vya uhuru mkubwa sana. Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa machozi alipopendekeza jina la Kawawa kuwa Katibu mkuu, wajumbe kabla hata ya kupiga kura, wakaanza kutikisa vichwa kumgomea. Mwalimu Nyerere aliinama kwa muda, wajumbe hawakujua ni kwa nini, baadaye alitoa leso mfukoni, akapangusa machozi yake. Ndipo wajumbe walipogundua kuwa Mwalimu alikuwa analia kutokana na wajumbe kuonekana kutomkubali Kawawa kuwa katibu mkuu wa chama.
Mwalimu kwa taabu akasema, "nimfananishe na nani Rashid katika nchi hii? Wakati wote tulipokuwa na jambo ambalo hatuna uhakika kama litafanikiwa au kama wananchi watalikubali au kulikataa, tulimpa Rashid akatangaze. Hata lilipoonekana jambo hilo kukataliwa na wananchi, Kawawa alisemwa vibaya na kulaumiwa, sisi sote tulikaa kimya, Kawawa hakujitetea, aliibeba aibu ya sisi sote". Baada ya maneno hayo ukumbi mzima ulilipuka na kuimba, Kawawa, Kawawa, Kawawa. Lakini CCM hii ya leo, kweli kuna mwanaCCM tena mjumbe wa Halmashauri Kuu wa kumfanya Mwenyekiti atoe machozi kuomba kuungwa mkono kwenye maamuzi?
Wakati ule wa G55, wabunge wa Bunge la chama kimoja, akina Kasaka, waliitikisa hasa Serikali, lakini hakuna aliyefanyiwa fitina. Kama ingekuwa ni hii CCM ya leo, hilo lingewezekana?
Ukweli ni kwamba, tunafikiria tunaenda mbele lakini kwenye mambo mengi tunarudi nyuma.
EeeenHeeeee!Ukitaka zoezi lisifanyike at the same time uwe tayari kuruhusu wengine washiriki na wengine wasishiriki, maana yake hao watakaoshiriki watahalalisha hilo zoezi hivyo ultimatum yenu kukosa maana.
Samahani, ilinibidi nirudi, pamoja na ile ahadi niliyoitoa hapo juu. Nimerudi kwa sababu nilikuwa sijasoma hadi huku mwisho. wa andiko lako. ambapo nilipomaliza kulisoma nikajiuliza:Hata hapo ulipowagusia Chadema kuongoza njia, napo utapoteza maana ya hili suala, kwasababu hapo tayari yale madai ya Katiba Mpya sio ya wanasiasa yatapata nguvu, na CCM pia watasema sio ya wapinzani hasa Chadema, hapa lazima pawepo na makundi mengine yatakayokuja front, na bahati mbaya, makundi hayo yako upande wa CCM mpaka sasa, kwa hofu au kupenda.
Lazima ajifiche maana anaweza kuuwawa, hivyo ni lazima atangeneze hamasa kwanza. Kwani hao wanaofanya mabadiliko ya kimifumo yasiyotakiwa na walioko madarakani huwa wanajitokeza hadharani kuhubiri hayo?
Utauliwa kwenye mitandao kwa hizi fake I'd. Ingekuwa ni verified user hapo sawa. Kwa hizi fake I'd unajua ni nani?Hii tension mnatengeneza Tu wenyewe bila maana yoyote
Nani awauwe.? Kwanini msiuliwe mnavyoongea kwenye mtandao?