Ni wakinga wachache tupo kwenye mambo ya Siasa, Siasa ni kazi ya ziada kwa wakinga

Ni wakinga wachache tupo kwenye mambo ya Siasa, Siasa ni kazi ya ziada kwa wakinga

Unamfahamu Kasisi wa Paradise Hotel pale Soweto Mbeya. Mbona anaishi kwenye nyumba ya matofali haina umeme
Kwa imani hii waswahili kufanikiwa ni vigumu sana. Kasisi anaishi wapi?!!!
Nimejifunza mengi kutoka kwa Chaula (wa Apple) jirani yake na Kasisi.
Tusipo achana na 'roho ya mbu',basi,Wakinga watatuacha kilomita nyingi sana kimaendeleo
 
Sio kweli hili unalosema, ukiona mkinga kaja Dar sio kwamba kaanzia kupambania Dar utakuta kaanzia mbeya huko, au tunduma au Zambia au njombe, sasa kwenye kuusoma mchezo ndio anajitahidi kufanya kitu cha kawaida kabisa lakini anamtaji wake, au ana binamu au kaka yake ambae anamfundisha kazi hivo pamoja na mtaji wake huku akisubiri kuongezewa na kupewa njia hana budi kukaa pale kwenye duka la kaka au binamu awe kama mfanyakazi ili ajifunze kazi ikoje.
Bila kusahau kaacha shamba la miti kijijini lina miaka minne,siku akivuna hela yote anaimwaga dukani,yanakuwa maajabu kwa wasio mjua.
 
Acha uongo mkuu
Unajua kasisi anaishi wapi?
Labda kahamia juzi tu. Lakini mpaka 2012 alikuwa anaishi eneo lisilopangwa (unsurveyed) pale Ilemi. Nyumba ilikuwa haina umeme.

Mara nyingi akiwa Mbeya hupatikana kwenye duka lake la jumla pale Mwanjelwa Stand. Naye hushiriki kubeba mizigo ya wateja ambao wamenunua na wanapakia kwenye mabasi.

Utajiri wa mateso sana ule
 
Wengine wanakuja tayari wana mitaji yao, ile kuuza kahawa na kashata ama umachinga ni njia ya kusoma mji...

Huwezi kufungua biashara kubwa kwenye mji wowote bila kufanya uchunguzi wa kina.
Uongo Mtupu, mwenye mtaji wa kufungua Duka la jumla haweza kufanya upuambavu huo. Tafiti ya biashara ya nguo ao electronics ufanye kwa kuuza kahawa na kashata [emoji848]?

Utoke utokako una mtaji wa kufungua Duka Kariakoo uanze kuuza kahawa eti kuusoma mji?

Mnasena kuwa na mitaji wa ml.100 uishi chumba cha elfu 40 kwa mwezi, ule chakula kimepikwa tandale kimebebwa ndani ya ndoo km za kutosha, uuze kahawa na kashata eti kuuzoea mji yaani NI kuhatarisha maisha yako unaweza kufa ao hela yote kupotea kutokana na risk ulizojisogezea.

Anatakiwa akiingia mjini atakutana na ndugu zake baa/hotel atawanunulia pombe/chai na hapo atapewa connection kulingana na mtaji wake, yaani uje kuusoma mji kwa kuuza kahawa una 100 kibindoni? UCHAWI MTUPU
 
Anyways nimejifunza mengi sana kwa mleta maada. Japo wanaopinga nao wasibezwe, wapewe majibu ya uhakika ili kufuta doubts.

Nakiri wazanaki tupo nyuma sana.
 
Inategemea na kipato cha mtu, narudia tena NI uchawi ao ukosefu wa akili. Una asset ipo kwenye mzunguko kwa siku hukosi faida ya laki 1, alafu ushindwe kunywa BIA ya 100,000 Weekend kisa unajenga ?

Laki 1 per day- mavazi yako ni suruali 3,000 shati la 2,000 kiatu cha 6,000 kisa unajenga ? BADO NITATAKA UPIMWE AKILI.

Hela ni kipimo cha nguvu/power huwezi kuwa una hela utake kuvaa,Kula,kulala ,anasa sawa na mtu wa kipato cha chini (mfano,:mmiliki wa Duka la jumla Kariakoo anaagiza chakula anacho agiza machinga anayenunua bidhaa kwake na kuuza nje ya Duka lake) uyo ni mchawi ao akili haipo Sawa.
Wewe kuwa tajiri bado sana kwa akili yako hii mgando
 
Labda kahamia juzi tu. Lakini mpaka 2012 alikuwa anaishi eneo lisilopangwa (unsurveyed) pale Ilemi. Nyumba ilikuwa haina umeme.

Mara nyingi akiwa Mbeya hupatikana kwenye duka lake la jumla pale Mwanjelwa Stand. Naye hushiriki kubeba mizigo ya wateja ambao wamenunua na wanapakia kwenye mabasi.

Utajiri wa mateso sana ule
Mkuu unazungumzia mambo ya 2012 leo? Kasisi haishi ilemi

Unasemaje wakinga akifa na biashara inakufa?
Unamjua mmiliki wa naura hotel Arusha? Vipi biashara zake zinaendeleaje mpaka saiv?

Vipi kuhusu kesi za Kila sku za familia ya Mengi?

Unajua mmiliki wa wanyama hotel alikufa lini na niambie biashara yake inayosuasua hata moja
 
Naura hitel ni Mrema kafariki 2019. Yeye alikuwa na matatizo ya management kutokuwa wazi. Pili ujio wa JPM na namna God bless Lema alivyovuruga biashara ya utalii ili drop.

Wanyama Hotel ya Sinza ilipigwa mnada baada yabmwenyewe kufa. Alikuwa ni Mkinga alikiuka masharti.

IPP Group ya Rrginald Mengi iko solid chini ya wanaye hata baada ya yeye kufariki. Kuna kesi ya mirathi dhidi ya make mdogo Jack Ntuyabaliwe lakini itaendelea ku flourish.

Wakinga wana utajiri wa mikataba. Unapata pesa muda fulani halafu unakufa.

Kama mnabisha njooni mniue nipo Ubungo Kibo
 
Kutembea na bidhaa mkooni Kariakoo huku una mtaji kiasi cha 100ml eti kuusoma mchezo!!!! Icho NI kipimo cha uchawi ao ukosefu wa akili.
Uelewa wako wa mambo ni mdogo sana sana

Tafuta pesa, Una stress za maisha na msongo wa mawazo

Fanya kazi acha porojo
 
Uongo Mtupu, mwenye mtaji wa kufungua Duka la jumla haweza kufanya upuambavu huo. Tafiti ya biashara ya nguo ao electronics ufanye kwa kuuza kahawa na kashata [emoji848]?

Utoke utokako una mtaji wa kufungua Duka Kariakoo uanze kuuza kahawa eti kuusoma mji?

Mnasena kuwa na mitaji wa ml.100 uishi chumba cha elfu 40 kwa mwezi, ule chakula kimepikwa tandale kimebebwa ndani ya ndoo km za kutosha, uuze kahawa na kashata eti kuuzoea mji yaani NI kuhatarisha maisha yako unaweza kufa ao hela yote kupotea kutokana na risk ulizojisogezea.

Anatakiwa akiingia mjini atakutana na ndugu zake baa/hotel atawanunulia pombe/chai na hapo atapewa connection kulingana na mtaji wake, yaani uje kuusoma mji kwa kuuza kahawa una 100 kibindoni? UCHAWI MTUPU
Yale maghorofa Kariakoo ni ya wakinga

Onyesha ya kwenu
 
Yale maghorofa Kariakoo ni ya wakinga

Onyesha ya kwenu
Unajua dalili moja wapo ya umasikini ni kujadli mali za watu! Wakinga kweli hela wanayo ila jamii yao bado iko nyuma kielimu sana huwezi linganisha na wachaga au wahaya! Kwa mfano kwetu sisi wasukuma jamii yetu kipindi kirefu cha nyuma hatukuwekeza sana kwenye elimu kama wenzetu kwa hilo mimi huwa sibishi japokuwa kwa sasa tunawekeza sana kwenye elimu kama wenzetu wananavofanya siku zote! Ila wakinga bado wachaga washaanza harakati mda mrefu na kwenye biashara nyie sio threat kwao hata kidogo bora hata useme msukuma anaweza kuwa threat kwa mchaga kwa baadae kutokana na mabadiliko ya wasukuma na wingi wao kwenye utafutaji ila kinga big NO,
 
Mimi Gussie nimezaliwa kaskazini na watu wananijua ni wa huko, Mimi ni Mkinga kamili wa Ikonda. Nimekaa sana Nchini Rwanda pia

Anayesemwa sana na watu Mzee Mwakipande aliyekuwa anatoa utajiri alikuwa mjomba wangu na alikwishafariki zamani, Hivi sasa anayefanya kazi za uganga ni mtoto wa mjomba anaitwa Leonard Mwakipande ndiye alirithishwa kazi

Wanaokwenda huko si matajiri tu kama watu wanavyosimuliwa, Kuna watu wana matatizo tofauti ya magonjwa ya ushirikina

Na sio kila tajiri unayemuona akienda huko amefuata utajiri Wengine wamezaliwa huko na huko ni kwao kama mimi GUSSIE

Kama una swali lolote kuhusu huko kwa Mwakipande niulize nitakujibu kwa kadri mimi ninavyoishi na hao ndugu zangu

Mambo mengi yanayosemwa kuhusu sisi wakinga sio kweli, Na hata hizi habari za utajiri kuwa Binamu yangu Leonard Mwakipande anatoa utajiri sio kweli

Kaburi la mjomba ni kweli hakuzikwa kama kuzikwa bali amewekwa kwenye kitanda chake na amejengewa nyumba ndogo tu, Yeye haozi na aliomba asizikwe

Maisha ya huko kwetu kwa sasa yamebadilika sana, Zamani tulitembea kwa miguu toka Ikonda mpaka huko, Leo kuna pikipiki za kutosha

Kuhusu Mimi Gussie kupenda siasa na kufanya kama kitu cha ziada ilitokana na sababu zifuatazo:

Mosi, Wakati huo wazazi wangu wanafanya biashara wao hawakusoma sana na hii ni kwa wakinga wengi wenye biashara hapo kariakoo, Wazazi waliamua kukata shauri na kutupeleka shule watoto ili tujue kuwa wahasibu wao na washauri. Mawazo yao hayo sasa yamefanya wakinga wafanye biashara za kisasa kwa kuzingatia sheria za nchi na kutokulalamika

Kwa kuwa wazazi wetu wengi wa kikinga walikuwa na pesa lakini elimu ndogo kila wakati waliona mambo ya kodi na sheria zinawaonea, Lakini sasa wakinga baada ya sisi watoto kwenda shule mambo yamebadilika na tunashauri wazazi vizuri

Kupitia haya mambo ya kwenda TRA na kurudi, Kuhudhuria vikao vya biashara na wanasiasa yakanifanya na Mimi kwanini nisiingie huko ili kupenyeza agenda zetu wakinga

Pili, Niliumia kuona wakinga ambao wapo kwenye siasa na Wakututetea ni wachache sana, Hata Darasani watu kutoka ukinga tulikuwa kidogo sana, Leo hii hapo Udsm sisi wakinga tuna hata mkufunzi Mkinga haikuwa jambo rahisi

Mwisho sisi ni wamoja na wala huwezi sikia tunagombana ingawa tunagombana lakini mambo yetu tunayamaliza kindugu, Hatuna wivu wala chuki sisi na mtu

Nakaribisha maswali kuhusu wakinga, Uliza nitakujibu

Mpaka Leo Mimi nikisikia Mkinga mwezangu amenunua Gari jipya nitajitahidi ninunue kama gari lake, Wakinga tunaigana sana mambo yetu, Ukifika Njombe pale utashangaa unaweza kuta magari yote ya aina moja

Msitucheke wakinga na mambo yetu ya kuigana kwenye kununua vitu

Any Question? , I 'm here to reply about Kinga' s
wewe Mkinga kweli mbona huna habari za Wakinga. Marekani walimchukua Mkinga mmoja alikuwa ana uwezo mkubwa wa hesabu aliajiriwa moja kwa moja NASA hajawahi kurudi Bongo kwa ajili ya unyeti wa taaluma yake. Mimi nilisoma naye Rungwe Alliance pamoja na Wakinga wengine bora kabisa akina marehemu Jaji Kyando. Msigwa kastaafu kazeeka bado haruhusiwi kutoka Marekani . Naweza kukutajia Wakinga wengi kwa wastani wa usomi wako juu ya makabila mengi hapa. Pia Wakinga wametawanyika Tanzania nzima. Morogoro, Tanga pia. Zungumzia unayoyafahamu usiyoyajua acha ndugu yangu.
 
Umenichekesha sana mkuu, Hapo ndipo unapoanza kufeli sasa, Na hapo ndio tunatafutiana kati ya wakinga na wengine kwenye kuthaminisha vitu au Pesa

Usiite mikeka au nyungo ni kitu kidogo, Unakosea sana huwezi fanikiwa ukishasema ni kitu kidogo

Kwanza hakuna kitu kidogo, Wala hakuna pesa ndogo

Kwa biashara ya nyungo na mikeka, Mikeka wakati huo ilikuwa na thamani kubwa sana kwa watu wa Mbeya hasa wanyakyusa. Mnyakyusa alizikwa kaburini na mkeka wa Kamba za migomba na ilikuwa heshima kubwa sana

Wanyakyusa wa Mbeya walipamba mikeka sebuleni na waliitumia sana kwenye sherehe kuwatandikia watu

Wakinga walianza kutafuta ukiri wa kusukia mikeka wakichanganya na Rangi ili kuweza kupata soko na kuwavutia wanyakyusa wengi

Mikeka ya Rangi Rangi iliyosukwa vizuri ilisababisha baadhi ya wakinga wengi wajipatie pesa za kutosha maeneo ya Mbeya na kidogo sehemu za Songea

Kumbuka wakati huo wa mikeka ipo juu sana kwa watu wa Mbeya,

Wakinga walikuwa hawaweki pesa Bank wala hawakujua maana ya Bank, Pesa waliweka ndani na kuzichimbia chini, Ilikuwa ngumu kupata taarifa ya Mkinga Bank

Pesa ndogo unayoita ilikuwa inachimbiwa ndani ya nyumba hata kwa miaka minne, Kwa kuwa hakuna taarifa Bank hivyo ni siri

Anapohitaji kuagiza kitu Mkinga inampsa aende Bank ndio hapo maneno yanaanza na wakati huo Bank ni NBC Bank, Mkinga aliweza kwenda Bulk cash NBC na maguni matano ya pesa ili aagize gari lake nje ya nchi. Maneno yanaanza kuzagaa kuwa muuza ungo na mikeka mchawi na anavuta pesa za wenzake wakati pesa alichimbia ndani kwa miaka hiyo
Vipi kuhusu hadithi ya kutaka unyerere?
 
Mbena na Mhehe =Mnyamwezi na Msukuma
Mkinga na Mpangwa = Mnyamwezi na Msukuma
Mangula ni Mbena.
Mbena na Mhehe ni walewale tu. Mfugale, Msigwa, Kalinga, Chumi, Kigola, Nyagava, Mligo, Kabelege, n.k Humo ndani kuna wahehe na wabena. Hawa watani zangu wahehe/wabena ni watu wema sana, ila ukiwaudhi shingo yako inakuwa mti wa kujitundikia
 
Naura hitel ni Mrema kafariki 2019. Yeye alikuwa na matatizo ya management kutokuwa wazi. Pili ujio wa JPM na namna God bless Lema alivyovuruga biashara ya utalii ili drop.

Wanyama Hotel ya Sinza ilipigwa mnada baada yabmwenyewe kufa. Alikuwa ni Mkinga alikiuka masharti.

IPP Group ya Rrginald Mengi iko solid chini ya wanaye hata baada ya yeye kufariki. Kuna kesi ya mirathi dhidi ya make mdogo Jack Ntuyabaliwe lakini itaendelea ku flourish.

Wakinga wana utajiri wa mikataba. Unapata pesa muda fulani halafu unakufa.

Kama mnabisha njooni mniue nipo Ubungo Kibo
Mkuu Mimi sio mkinga Ila nnaishi nao na nafanya nao kazi mpaka leo, nawajua in and out

Kuhusu ushirikina hakuna kabila lisilo na washirikina

Wakinga wanatoboa kwa njia kusaidiana, kufanya kazi kwa bidii bila kusahau ubahili uliopitilizaaa
 
Back
Top Bottom