Ni wakinga wachache tupo kwenye mambo ya Siasa, Siasa ni kazi ya ziada kwa wakinga

Unamfahamu Kasisi wa Paradise Hotel pale Soweto Mbeya. Mbona anaishi kwenye nyumba ya matofali haina umeme
Kwa imani hii waswahili kufanikiwa ni vigumu sana. Kasisi anaishi wapi?!!!
Nimejifunza mengi kutoka kwa Chaula (wa Apple) jirani yake na Kasisi.
Tusipo achana na 'roho ya mbu',basi,Wakinga watatuacha kilomita nyingi sana kimaendeleo
 
Bila kusahau kaacha shamba la miti kijijini lina miaka minne,siku akivuna hela yote anaimwaga dukani,yanakuwa maajabu kwa wasio mjua.
 
Acha uongo mkuu
Unajua kasisi anaishi wapi?
Labda kahamia juzi tu. Lakini mpaka 2012 alikuwa anaishi eneo lisilopangwa (unsurveyed) pale Ilemi. Nyumba ilikuwa haina umeme.

Mara nyingi akiwa Mbeya hupatikana kwenye duka lake la jumla pale Mwanjelwa Stand. Naye hushiriki kubeba mizigo ya wateja ambao wamenunua na wanapakia kwenye mabasi.

Utajiri wa mateso sana ule
 
Wengine wanakuja tayari wana mitaji yao, ile kuuza kahawa na kashata ama umachinga ni njia ya kusoma mji...

Huwezi kufungua biashara kubwa kwenye mji wowote bila kufanya uchunguzi wa kina.
Uongo Mtupu, mwenye mtaji wa kufungua Duka la jumla haweza kufanya upuambavu huo. Tafiti ya biashara ya nguo ao electronics ufanye kwa kuuza kahawa na kashata [emoji848]?

Utoke utokako una mtaji wa kufungua Duka Kariakoo uanze kuuza kahawa eti kuusoma mji?

Mnasena kuwa na mitaji wa ml.100 uishi chumba cha elfu 40 kwa mwezi, ule chakula kimepikwa tandale kimebebwa ndani ya ndoo km za kutosha, uuze kahawa na kashata eti kuuzoea mji yaani NI kuhatarisha maisha yako unaweza kufa ao hela yote kupotea kutokana na risk ulizojisogezea.

Anatakiwa akiingia mjini atakutana na ndugu zake baa/hotel atawanunulia pombe/chai na hapo atapewa connection kulingana na mtaji wake, yaani uje kuusoma mji kwa kuuza kahawa una 100 kibindoni? UCHAWI MTUPU
 
Anyways nimejifunza mengi sana kwa mleta maada. Japo wanaopinga nao wasibezwe, wapewe majibu ya uhakika ili kufuta doubts.

Nakiri wazanaki tupo nyuma sana.
 
Wewe kuwa tajiri bado sana kwa akili yako hii mgando
 
Mkuu unazungumzia mambo ya 2012 leo? Kasisi haishi ilemi

Unasemaje wakinga akifa na biashara inakufa?
Unamjua mmiliki wa naura hotel Arusha? Vipi biashara zake zinaendeleaje mpaka saiv?

Vipi kuhusu kesi za Kila sku za familia ya Mengi?

Unajua mmiliki wa wanyama hotel alikufa lini na niambie biashara yake inayosuasua hata moja
 
Naura hitel ni Mrema kafariki 2019. Yeye alikuwa na matatizo ya management kutokuwa wazi. Pili ujio wa JPM na namna God bless Lema alivyovuruga biashara ya utalii ili drop.

Wanyama Hotel ya Sinza ilipigwa mnada baada yabmwenyewe kufa. Alikuwa ni Mkinga alikiuka masharti.

IPP Group ya Rrginald Mengi iko solid chini ya wanaye hata baada ya yeye kufariki. Kuna kesi ya mirathi dhidi ya make mdogo Jack Ntuyabaliwe lakini itaendelea ku flourish.

Wakinga wana utajiri wa mikataba. Unapata pesa muda fulani halafu unakufa.

Kama mnabisha njooni mniue nipo Ubungo Kibo
 
Kutembea na bidhaa mkooni Kariakoo huku una mtaji kiasi cha 100ml eti kuusoma mchezo!!!! Icho NI kipimo cha uchawi ao ukosefu wa akili.
Uelewa wako wa mambo ni mdogo sana sana

Tafuta pesa, Una stress za maisha na msongo wa mawazo

Fanya kazi acha porojo
 
Yale maghorofa Kariakoo ni ya wakinga

Onyesha ya kwenu
 
Yale maghorofa Kariakoo ni ya wakinga

Onyesha ya kwenu
Unajua dalili moja wapo ya umasikini ni kujadli mali za watu! Wakinga kweli hela wanayo ila jamii yao bado iko nyuma kielimu sana huwezi linganisha na wachaga au wahaya! Kwa mfano kwetu sisi wasukuma jamii yetu kipindi kirefu cha nyuma hatukuwekeza sana kwenye elimu kama wenzetu kwa hilo mimi huwa sibishi japokuwa kwa sasa tunawekeza sana kwenye elimu kama wenzetu wananavofanya siku zote! Ila wakinga bado wachaga washaanza harakati mda mrefu na kwenye biashara nyie sio threat kwao hata kidogo bora hata useme msukuma anaweza kuwa threat kwa mchaga kwa baadae kutokana na mabadiliko ya wasukuma na wingi wao kwenye utafutaji ila kinga big NO,
 
wewe Mkinga kweli mbona huna habari za Wakinga. Marekani walimchukua Mkinga mmoja alikuwa ana uwezo mkubwa wa hesabu aliajiriwa moja kwa moja NASA hajawahi kurudi Bongo kwa ajili ya unyeti wa taaluma yake. Mimi nilisoma naye Rungwe Alliance pamoja na Wakinga wengine bora kabisa akina marehemu Jaji Kyando. Msigwa kastaafu kazeeka bado haruhusiwi kutoka Marekani . Naweza kukutajia Wakinga wengi kwa wastani wa usomi wako juu ya makabila mengi hapa. Pia Wakinga wametawanyika Tanzania nzima. Morogoro, Tanga pia. Zungumzia unayoyafahamu usiyoyajua acha ndugu yangu.
 
Vipi kuhusu hadithi ya kutaka unyerere?
 
Mbena na Mhehe =Mnyamwezi na Msukuma
Mkinga na Mpangwa = Mnyamwezi na Msukuma
Mangula ni Mbena.
Mbena na Mhehe ni walewale tu. Mfugale, Msigwa, Kalinga, Chumi, Kigola, Nyagava, Mligo, Kabelege, n.k Humo ndani kuna wahehe na wabena. Hawa watani zangu wahehe/wabena ni watu wema sana, ila ukiwaudhi shingo yako inakuwa mti wa kujitundikia
 
Mkuu Mimi sio mkinga Ila nnaishi nao na nafanya nao kazi mpaka leo, nawajua in and out

Kuhusu ushirikina hakuna kabila lisilo na washirikina

Wakinga wanatoboa kwa njia kusaidiana, kufanya kazi kwa bidii bila kusahau ubahili uliopitilizaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…