Ni wazo tu: Wachaga wahamishwe maeneo ya Mlima Kilimanjaro!

Huo ujinga jaribuni kufanyia sehemu nyingine, msichezee moto
 
Na wasambaa, wasafwa, wabena, wahehe, wapogolo, wandamba, wavidunda, wazigua wahame plus wapare
 
NAUNGA MKONO HOJA WANAHARIBU MAZINGIRA, WAONDOLEWE APEWE MWEKEZAJI ATUNZE MAZINGIRA
 
Shukrani...
Na Je Ngorongoro ni National Park au Conservation area?
 
Na wasukuma wahamishwe maeneo ya lake victoria
Na watu huko zanzibar wote waondolewe kisiwa kibaki chenyewe tu watalii tu wawe wanaingia,au unasemaje

Ova
 
Naunga mkono hoja,mlima Kilimanjaro miaka ya nyuma ilikuwa unaheshimika sana.Ila kizazi cha sasa kilichonzunguka mlima huo kina hatarisha mazingira,ujenzi holela ,vyanzo vya maji ,ona hata theluji ya mlima inavyoyeyuka.Ila kibaya zaidi mlima umezingukwa na makaburi kila upande,hili kabila kila Mtu akifariki hata huko aliko alijemga lazima arudishwe Kilimanjaro kuzikwa why?wakati nchi ni kubwa,kitendo cha mlima mrefu na mahala ambapo tunategemea watalii wafurike kwa wingi basi kumejazana makaburi .Na kingine wakazi wanaonzunguka mlima huu muhimu ni walevi wa kupindukia,huku mikoa mingine tumewapa maeneo ya kutosha na kuwapa fursa za biashara ikiwepo maduka madogomadogo maarifu kwa mangi nchi nzima Bado tu wanarudi kujenga majengo ambayo hawakai na kurudi kila mwisho wa mwaka kuchafua mazingira 😂😂😂jamani me mtani wenu tu😂😂
 
Nimekuelewa!! lakini onyo ni hili! SSH ataondoka saa nusu hakuna jeshi wala TISS watakawaweza wale majamaa! Hebu ajaribu tu kufikiria halafu ijulikane tu! SIYO kuandika wala kutenda!
 
Una bahati sana ,apo mwishoni😁
 
Tena Desemba watakuwa wanaenda Msomera!
Siyo Moshi tena!
Shira haiwezi tena kulipuka...

Mawenzi haiwezi tena kulipuka...


Ila si KIBO meku ....

Utani tu..natania kaka

KIBO iko "active" sasa siku VOLKANO ikilipuka na wananchi walioko karibu wakahamishwa kwa muda mfupi ama moja kwa moja watakuwa wamehamishwa na serikali ya JMT ili watalii na wawekezaji waje ?!! [emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…