Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Kuna wimbo flani wa nyoshi el sadati nisaidieni jina lake, uko hivi "niko tayari ii, niko tayari ii ii kuishi na wee. anaendelea kuimba hivi japo sina hakika "mbelamu mbelamu, mzuri sana ila siujui jina lake
 
Usjali mkuu tuko pamoja sana bro.

Thanks a lot.
Ahsante sana mkuu. Yaani daah.

Nikushukuru kwa niaba ya wenzangu ukio watag. Sharing is caring. Huo namba 4 umeimbwa na Neck Breakers. Upo hapo juu. Angalia kuanzia page ya 140

Sent from my SM-N9005 using JamiiForums mobile app
Ahsante chief.

Nimekaa hapa nikawaza mb nilizopakua, nikaona kwa kweli mmeshughulika kuzi-upload si kitoto.
***

Baada ya hayo sasa nina changamoto kuna wimbo sikumbuki jina vema, nitajieleza.
Ameimba dogo mmoja hivi kupitia Motika records, nadhani huyo dogo alikuwa wa Tanga kama sijakosea. Huenda jina la wimbo ni Orbayan/Olpaiyan kitu kama hicho. Ni hip hop,
 
Wakuu nisaidieni wimbo wa dansi nafikiri wameimba wana tamtam... Kuna mahali kuna kibwagizo kinasema..

"Nina ugeni nyumbani.. Na pesa zimekwisha kwa matumizi yangu mimi na wewe..".. Ni sauti ya mwanamke..
 
Kuna wimbo mmoja hivi wa anderground wa zamani sijui kaimba msanii gani jina limenitoka unaekezea maisha kama ya kuzaliwa mpaka unatokea duniani ulikuwa unapigwa sana radio prt kabla haujabadilishwa jina na kuitwa tbc fm na kuna mwingine jina sina uhakika na jina unahusu wanafunzi kunyanyaswa sijui unaitwa ndani ya daladala haki tunanyimwa ni rap fulani hivi
 
Nisaidieni wakuu jina la ule wimbo wa nyoshi el sadat
 
Kuna wimbo mmoja hivi wa anderground wa zamani sijui kaimba msanii gani jina limenitoka unaekezea maisha kama ya kuzaliwa mpaka unatokea duniani ulikuwa unapigwa sana radio prt kabla haujabadilishwa jina na kuitwa tbc fm ...

Kama nimekupata vema itakuwa unazungumzia Mkiwa, ameimba dogo mmoja hivi akimshirikisha Ferouz.
"Mkiwa mi najikongoja, dunia naiona chungu naona bora niwafate wazazi tuwe pamoja..." hiyo ni sehemu ya chorus yake.
 
Back
Top Bottom