Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Nataka ule wimbo wa redio Uhuru wa kipindi cha magazeti.."nawapa hongera waandishi wetu..wa magazeti ya Africa mashariki"
 
Kuna wimbo waliimba hadi msibani kwa Ruge. Unaimbwa "iye lelele mama, ye lele mama x2 nataka kurudi Kwetu kwa baba na mama..
Nautafuta sana huu wimbo wadau
 
Mkuu KIOO kuna ngoma ya Q Chief ft Mangwea jina nafikiri unaitwa Sorry! Na nyingine ni ya Soggy ft Dogo hamidu, Suma G, Caz t, na wengineo japo nimeushau jina!!

Barikiwa kama tunaweza kuzipata hizi!!
 
Wakuu kuna nyimbo 1 ya jamaa wa kenya anaitwa Lenny km sjakosea, chorus yake ni "sasa bebigal, sio kamdigida nataka nikutach, nimekutafuta kwa shidaa sio kamdigida nataka nikutach"

Nna miaka zaid ya 5 nausaka huu wimbo bila mafanikio

Cc KIOO
hahaha nimeukumbuka ila jina sasa duh😆😆😆 nyimbo zote kali za "Genge" ninazo ila huo ndio sina ngoja niusake.
 
Mkuu KIOO natafuta nyimbo za soul and face. Hawa ni vijana waliokuwa wakiimba R&B miaka ile ya 2000 mwanzoni. Kama hutajali naomba nyimbo zao zote ulizonazo maana hata majina sizikumbuki.
 
Mkuu KIOO naomba ngoma kama 5 za Hip Hop za mbele zilizopo kwenye playlist yako japo nipate feelings zako mkuu.

Hahahahah, tatizo feelingz zangu zipo nyingi aisee. Anyway ngoja nikupe za Daktari na Bonus 1. Feel The Vibez Bro.
 

Attachments

Cosmas Chidumule - Hosanna Original,

ukisearch google na youtube inakuja hosana amabayo si wimbo wa hosana.
 
Mkuu sijui nimekukosea nini ndughyangu yaani nyimbo zoote nilizo kuomba hujanitumia hata moja yaani,wenzangu wanakuja nyuma unawatumia kulikoni??niliomba nyimbo za sqeeza na langa naona kimya tu.
Ok ni nyimbo ya sqeeza inautwa nitoke vipi au hata nikipata nyimbo zake kama tano tu rohoyangu itasuuzika mkuu pamoja na marehem langa nikipata hata tano tu leo ntaenjoy kabisa
 
Back
Top Bottom