Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Mwenye wimbo wa Tongolanga unaitwa Sanura naomba afanye kuu-appload humu jukwaani,nimeutafuta wimbo huo kwa muda mrefu sana
Pia,kuna wimbo unaitwa my friend remix ameshirikishwa Blue Kabaisa mwenye nao naweza fanya kweli!
 
Huyu jamaani mbongo kweli mkuu?mbona jina limekaa kama la ki-Africa magharibi?

hapana mkuu, huyu ni msanii wa Mali miaka ya nyuma kidogo, nyimbo zake ni za ki - afro... kuna baadhi ya nyimbo zake nashindwa kuzipata sababu sizikumbuki jina, nakumbuka videos tu...
 
Hapana sio barua, kuna nyimbo kwenye kama anamwimbia demu huku akimbembeleza na kumpa matumaini ya kwamba ipo siku nao watakuwa na maisha mazuri
Basi ni Vumilia Ya UVC...Feruz alishirukishwa tu...

Vumilia ndo hali ya dunia..
ipo siku ndoto zetu zitatimia
 
Ndio. Nipo?
mkuu habari, nikidescribe kwa video jinsi ilivyo utaweza tambua jina la nyimbo, kwa kweli wimbo huu nimeshindwa kabisa kuupata sababu jina silijui, nilikuwa nikiuona nikiwa mdogo...
 
Mimi nautafuta wimbo fulani wa gospel uliimbwa na kwaya Fulani kitambo sana. Nmesahau jina lake na Nina la kwaya yenyewe lakini nakumbuka mistari take baadhi. Na mistari yenyewe ni ifuatayo: Nimekuleta chini nikakupa kila kitu lakini umesahau kwamba Mimi ni muumba wako. Ntashukuru Nikiupata.
Hiyo nyimbo inazungumzia kuhusu mwanadamu, anaimba mbaba flani hivi kisha kuna sauti ya wanawake inaitikia.
 
Kuna wimbo mmoja aliimba jamaa wa Uganda nafikiri miaka ya 2008, ulikuwa na maudhui nzuri sana, moja ya rhyme zake ni hizi
"Analia akitizama chini,
Na hajui atafanya Nini,
Loo lo lolooo"
Shortly unamuhusi binti ambaye alikuwa akionywa na mama ake toka akiwa mdogo asifuate ya kidunia alivofika kidato Cha tatu Basi dunia ikamhadaa akapoteza vyote mzee.
 
Wimbo wa SHARI MARTINI
unasema:

"Kuzaliwa, kwa Bwana Yesu
Ni ukombozii kwangu x2
Na kama vile ilivyotabiriwa,
Atazaliwa na Bikira Mariam,
Na kwamba wote watakao mwamini,
Waokolewe siku ya mwisho"

My Take:
Mkuu huu wimbo ninachanganya sana majina yake, kati ya
1. Kuzaliwa kwake Yesu
2. Usilie n. K
Kama waweza upata tujulishane maana Christ Mass ndo hiyo inafika.
 
Habari mkuu

Nami naomba ule wimbo wa kwaya unaosema HAKUNA MUNGU KAMA WEWE YAWEE AAAHH. AAAHH



Shukrani.
 
Back
Top Bottom