Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Mwenye video ya wimbo kazi yake mola haina makosa ya madee...naomba
 
Naona kwangu hii link haifunguki mkuu. Kama kuna namna nyingine naomba nisaidie

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimejaribu kupakia audio imezingua. Ikifika asilimia 100 kwenye uploading kuna notification inakuja kama hivi.
Screenshot_20200529-140824.jpg


Sent from my Infinix NOTE 3 Pro using JamiiForums mobile app
 
jaman msaadaaa
habari wana jf.
kuna mwimbo nimeusikia sehem nautafuta laki siupati ila nakumbuka muimbaji anavo anza kuiimba ni wa kike sauti inataka kufanana na rachel wa kizunguzungu ivi. unaana za ivi "akasema kwa sauti mkewangu dekaaa dekaaa aaahhh " 😆😆 icho kipand ndo nakumbuka naomba msaada apo
 
Natafuta wimbo wa AT ft Alikiba & queen darlin .....kwanini umenipenda mimi! ni old vibe ambayo verse ya Alikiba nilikuwa naielewa mno
 
Kuna wimbo ulikuwa unapigwa kwenye kipindi Cha watoto radio one zamani kabla na baada ya kipindi kuanza. Nautafuta Sana huo wimbo, ulikuwa unaanza hivi; watotooo wasafi moyoni, Ni nyota za macho ya wazazii, sisi Ni maua, tuliyoopendwa na Mungu mwenyeziii....' please mwenyewe huo wimbo tafadhali nauomba.
 
Kuna wimbo ulikuwa unapigwa kwenye kipindi Cha watoto radio one zamani kabla na baada ya kipindi kuanza. Nautafuta Sana huo wimbo, ulikuwa unaanza hivi; watotooo wasafi moyoni, Ni nyota za macho ya wazazii, sisi Ni maua, tuliyoopendwa na Mungu mwenyeziii....' please mwenyewe huo wimbo tafadhali nauomba.
Jaribu YouTube, Varda Arts- Watoto Wasafi Moyoni...
 
Habari .
Kuna nyimbo inaimbwa
Malaika wangu nitakufa nawewe tu,
Kisura wangu we tembea na mimi tu,

Hii nyimbo ni ya bongo fleva naitafuta sana na aliyeimba ni ME .
Msaada tafadhali kwa anayejua jina la wimbo au angalau artist tu wa hii nyimbo.
KIOO
Idimi
 
Wimbo niutafutao, nashauri yake yapo kama ifuatavyo.

Ondoa mawazo yako,nimekwisha kusamehe
Sasa nakuomba Joyce usifanye tena.
Uliyoyafanya mwanzo, kweli ni mabaya.
Sasa nakukanya Joyce, usifanye tena.

sent from Samsung Galaxy A30
 
wakuu nisaidieni hiyo nyimbo kwny hiyo clip asee nyimbo tamu sana
 
Tafadhali, naomba mwenye wimbo wa Mchungaji Abiud Misholi unaitwa Namna gani aniangushie hapa. Natanguliza shukrani... Mbarikiwe.
 
Natafuta wimbo ulioimbwa na FM Academia unaitwa "JELA" ulitungwa na marehemu Ndanda Kosovo.

Wimbo huu ulitungwa baada ya wanamuziki wa bendi hiyo kuingia nchini bila vibali hivyo wakaishia kwenye mikono ya dola, baada ya kutoka kwao ndio wakatoa hit song hiyo!

Nitashukuru kama nitaupata maana nimeutafuta sana bila mafanikio! Ahsanteni
 
Kuna wimbo wa zilipendwa,.una maneno haya

✓Kitanda kipo wananilaza chini
✓chakula kipo wananipa makombo
✓wazazi fanyeni haraka mje mnichukue
 
Back
Top Bottom