Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Kwa mwenye wimbo wa FM Academia ulioimbwa na rapa wao Mulemule FBI,wenye ghani ifuatayo:

"🎼🎶 Heri kwa wale wazazi waliondoka wakawaachia mali,

Sisi wazazi wameondoka wametuacha mikono tupu. 🎶🎼🎹"

Maudhui ya wimbo kuwapa faraja yatima wote.Wimbo huo una mahadhi ya rhumba. Aliyenao pleeaaase!
 
Natafuta nymbo ya msanii mmoja jina silijui ila kwenye nyimbo hyo chorus yake anaimba " I'm gonna miss you on Monday Tuesday miss u Wednesday
 
Mimi natafuta wimbo Ameimba Jay moe alafu kiitikio kaimba t.i.d unaitwa tingisha Kama kiberiti ,nimetafuta huu wimbo lakin wapi , unanikumbusha enzi Niko form one mwaka2005 ulipigwa siku ya kutupokea aisee lile disco siwez lisahau ,sasa huo wimbo ulipigwa Zaid ya Mara Mia
Mwamba usije kuwa class mate wangu hata mie huo wimbo ulipigwa Sana welcome form 1 mi ninao kama una watsap niomp nikutumie
 
Kuna zilipendwa moja naitafuta siijui jina ila nakumbuka tu baadhi ya maneno yalikua yakisema "ona sasa kiko wap waliokudanganya wako wap wamekuacha huna pakuanzia dunia ya sasa maua maua eenh maua. Emunue .nimekuzoea eenh!

Na kuna maneno mengine yanasema baba kavunjika mguu alipoa anakufukuza nlijua eemh!
 
jina la nyimbo silikumbuki ila ina maneno haya" NI MAKOSA NI VIBAYA MNAFANYA WAZAZI NI AIBU NI HUZUNI NI OYOYOYO" ya zamani(zilipendwa) natanguliza shukrani.
 
Habari za jpili wanakikundi naombeni wimbo wa Balaji wimbo unaitwa faraja mi naliaaaa mpaka nashindwa kuvumiliaaaa.
 
Natafuta wimbo Wa kale sana sijui unaitwaje ila una maneno kama " chawa na panya waliishi nyumba moja... Samahani sana.., samahani sanaaa..!
Hapana maneno yanasema ,Kunguni na viroboto ni marafiki zaaaaanguuuuu, Chawa na panya tuliishi nyumba moja, ila kwanini usiku mnanisumbuuua... Naaaasikitikaaaaaaaa.....halafu ndio anasema samahani saaana saaamaani saaaaana.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]




Kanyimbo hako marehemu bibi mzaa baba alikuwa anakapenda balaa.

Tunamuwekea katika redio yake ya tape , anakaa kibarazani huku anagida mbege au Ihombwa kama alivyokuwa anaiita.

Dah we jamaaaa umenikumbusha mbali sana na haka kanyimbo. Ngoja nitafute jina la msanii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wimbo nautafuta

Artist: Thug city
Song name: Preposition

Ulikuwapo YouTube miaka ya nyuma ila kuanzia 2014 nautafuta siuoni online naishia kuona lyrics ila haukuna audio wala video.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaman naomba mnisaidie jina la wasanii walio imba wimbo huu, na jina la wimbo pia ikiwezekana. Ili niweze kuutafuta.

" nikikupa kupa kuupa utalewaa aah, nanikikunyiima dhuruma ×2.
Nishachoka mie, usichokoo ×3 "
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hako kawimbo nilikuwa nakatazama ITV daaaaaah Jamaa na demu wake wanaimba kivivu ha ha ha ha ha ha ha..... Eti Hooooooi Hooooi..... [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna nyimbo za captain komba na wenzie kwenye album ya mwaka 95 kama
1.Muongo
2.Nyumba yajiran yetu inateketea moto
3.tukazane kuomba
Nanyingne kibao nmezisahau majina! Kama kunaalienazo anisaidin
 
Back
Top Bottom