Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Natafuta wimbo wa kitambo hivi wa Bongo flavour kaimba mdada mistari yake ni hii

" sheila sheila uwe na huruma kwani moyo unaniuma penzi langu ni la dhati kwani nimempata wa bahati sheila uhuuuu sheila ahhhhh" "
Esther Wassira nakumbuka ndio ana huo wimbo.
 
Naomba wenye wimbo unaoimbwa "Bure bado wasumbuka kubeba bila kushika Kama huna asili navyo mwiba unachoma kote si rahisi kukwepa Kama huna asili navyosijui umeimbwa na NI I Kama unao nitumie
 
Wakuu samahani kuna wimbo Jose Mara unaitwa imebaki story, ndivyo nilivyousikia Lakota akiutaja jina kweny weekend bonanza.. Nimeutafuta you tube, google lakini sijaupata msaada tafadhali kwa mwenye nao.

Pia kuna wimbo mmoja wa Msondo ngoma kuna sehemu wanaimba hivi 'Wanasema atapa shida atapata taabu yeye mtoa ridhiki" kama sijakosea ni hivo, nao naomba msaada kwa mwenye nao
Mkuu huo wimbo wa msondo ngoma ushaupata???? Nautafuta sana bila mafanikio Kuna sehemu ya huu wimbo wanaimba hivi " mikononi naweka roho yangu nikomboe kwenye dhiki na faraja tuwe pamoja,naamini busara yangu nayako vitatumika mbele ya wale wasiopendaa, laazizi wewe ndiye mpenzi wangu utanichunga jangwanii....."
 
Kuna wimbo una maneno " bolingo sekotuo...bolingo sekotuo..". Midundo yake inaendana na upigaji wa Empire Bakuba bendi ya hayati Pepe Kalle.
 
Natafuta sana nyimbo hizi bila mafanikio.Mpangilio wake kwenye albam ulikuwa hivi
Sauti ikatoka
Adamu na Eva walikula tunda
Mateso yake bwana yesu
Nimekuweka chini
Bwana ndiye mchungaji wangu
Mimi mzabibu
Bwana Mungu asema leteni dhaka
Bwana niangaze n.k

Nimetafuta kila mahali mitandaoni sipati.Hakika zilikuwa zinanibaliki sana mwenye nayo albam hii anisaidie

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
HIZI NYIMBO ZIPO YOU TUBE ILA SIO KWA MOJA MOJA, YANI ZIPO ALBUM NZIMA NA TATIZO HAZINA QUALITY NZURI.
 
Wimbo wa THT Milele na milele kuna bui bui mle ndani...
 
Kuna ngoma moja hivi ya kimexico au kivenezuela ilikuwa inachezwa kwenye tamthilia fulani hivi inaitwa la revanja cjui. Kwa wale waliokuwa wanafatlilia tamthilia za zaman watakuwa wanaifaham.

Ni tamthilia ambayo ilikuwa inasisimua sana. Anayeifaham ile nyimbo anitajie ili niweze ipakua.
 
Kuna wimbo hivi wa romani Katoliki. Mashairi yake ni haya

'' nasi tumeumbika tulivyo kwa ajili ya mapenzi yake mungu ili utukufu wake mungu Mwenyezi ujulikane kwa wote ''
Msaada jamani
 
Back
Top Bottom