Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Aisee natafuta ngoma moja ya Snare yule alikuwaga kwenye kundi la East coast team... unaimbwa "Kwenye game jinsi inavyokuwa... kuwa na umakini mambo mengi yanatokea! Niite Snaareee mashit! Yanaendelea... haina noma kwenye game mi nasogea!..." tafadhali anaejua nitaipata vipi anisaidie tafadhali inanikumbushaga mbali sana. Zamani ndo kulikuwa na nyimbo, yaani Ukisikiliza ujumbe, mpangilio, mashairi na hata watu walivyovaa unaburudika! Ingawa tulikuwa bado sana kwenye videos. Those days was good!
Da umenikumbusha mbali Sana huu wimbo nilikuaga naupenda kinyima aisee ukiupata nipe pia
 
kuna ngoma moja ya msondo ngoma naitafuta sanaa.. ipo hivi " Mapenzi yamegawanyika katika sehemu kuu mbili ninavojua mimiii.. sehemu ya kwanza ni faraja vicheko pamoja na... utadhani duniahii ndugu yote ni yako" Walamsishangaeee..... " Jama Jamaa Nauombeni sana aisee..
 
nautafuta wimbo(instrument) ile zamani ilikuwa inapigwa Radio One saa 4 usiku kionjo cha kipindi cha chombeza time, mwenye jina la wimbo huo au msanii aliyepiga wimbo huo tafadhali tutajie
 
Kuna ngoma nimeiskia juzi kwenye kibanda cha kuchoma CD naitafuta na sijui ntaipataje,,, anyways naeza saidiwa tafadhali,,,, ni amapiano moja tam sana ni ya kibongo na inahusu mapenzi,, jamaa anasauti kama ya belle nine,,, inahusu jamaa aliziezidiwa na mapenzi,, mwishoni kabisa lyrics za mwisho anaimba taratibu na neno lenyewe anaimba "nyang'anyang'a"
 
Wa judy burchure

This is love my dear wellcome to my world and let shere the good time together naipenda sana
 
Kuna ngoma flani naitafuta bila mafanikio
*ngoma imeimbwa na masister flani nadhani ni wa west africa

*ngoma ni ya vibe na inapigwa sana club
*video yake wale madem wanacheza san style kmma ya gwala gwala

kionjo chake kabla ya beat lao kali linasikika ""alee alee eeeh ale ale aaah" alaf beat [emoji119]
 
Kuna nyimbo naitafuta ni mtindo wa chakacha nadhani msanii ni wa kutoka kenya. Niliusikia miaka ya 90s mwishoni. Muimbaji ni mdada. Maneno ninayo yakumbuka kwenye wimbo huo ni "Chakacha ndio kipaji changu"
 
Wimbo unaitwa Veronica, uliimbwa na msanii G short ft. Nurueli

Mwenye nao jamani
 
kuna ngoma moja ya msondo ngoma naitafuta sanaa.. ipo hivi " Mapenzi yamegawanyika katika sehemu kuu mbili ninavojua mimiii.. sehemu ya kwanza ni faraja vicheko pamoja na... utadhani duniahii ndugu yote ni yako" Walamsishangaeee..... " Jama Jamaa Nauombeni sana aisee..
Unaitwa penzi kizungumkuti
Unamkuta Othmani Momba humo ndani ngoja nikutafutie kwenye library yangu
 
kuna ngoma moja ya msondo ngoma naitafuta sanaa.. ipo hivi " Mapenzi yamegawanyika katika sehemu kuu mbili ninavojua mimiii.. sehemu ya kwanza ni faraja vicheko pamoja na... utadhani duniahii ndugu yote ni yako" Walamsishangaeee..... " Jama Jamaa Nauombeni sana aisee..

Mkuu app ya jf inazingua kuweka attachment nimejaribu bila mafanikio
 
Kuna ngoma flani naitafuta bila mafanikio
*ngoma imeimbwa na masister flani nadhani ni wa west africa

*ngoma ni ya vibe na inapigwa sana club
*video yake wale madem wanacheza san style kmma ya gwala gwala

kionjo chake kabla ya beat lao kali linasikika ""alee alee eeeh ale ale aaah" alaf beat [emoji119]
Nahisi unawasemea obession hawa ni wa Uganda huo wimbo unaitwa Jangu… check YouTube
 
Back
Top Bottom