Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Wakuu mwenye hizi nyimbo kwenye library yake anisaidie tafadhali:
1. Tid - Sauti ya dhahabu
2. Ney - Mitego
3. ??( nimemsahau msanii na wimbo) kiitikio kimeimbwa
"Shani wangu nakupendaaa ooh mi nakupendaaa,
Shida nilizozipata anajua ye mwenyeeeziiii..x3"


Nawasilisha
Nina huo wa Mitego.

 
Natafuta wimbo wa "Tunaelea Tunaelea tunakwenda mbinguni, jamani dunia siitaki......."

Naambiwa huo wimbo uliimbwa sana miaka ya tisini, hususani kwenye mikutano ya injili Dar, sijui ni Kinondoni revival, Kawe revival au City Christian Fellowship?

Mwenye nao atusaidie hapa, na sisi wa kizazi hichi tuburudike.
 
Msaada kwa wimbo wa Komboa Wakati kutoka AIC Arusha. Natanguliza shukrani wadau...
Screenshot_20230124-220725_Gallery.jpg
 
Ngoja niweke mashairi Kwanzaa song linaanza au linaelezea jamaa anaenda kwa mganga apate utajiri ila mganga anamwambia awaue wazazi wake jamaa linakubali baadae mambo yanamuendea kombo plus mawazo anaanza kulewa



Shairi ninalolikumbuka ilikuwa bongo flavor ya kipindi hicho

Pesa na majumba, ni vitu vya kutafuta
Usifanye wewe pupa, utakuja kuvikuta
Ona baba yako umemzka, huna huruma na mama yako mume mzma,
Sasa umebaki ohii

Lengine linasema
Mganga kamwambia, awaue wazazi wake ili apate hzo pesa zake
Akasema yeye hawezi kwani wao ndo tegemezi

Anaekumbuka tafadhali
Hii nyimbo nimeitafuta mda mrefu sana. Ilikuwa inapigwa sana chanel ten. Kama uliupata naomba unitumie. .
 
Kuna mwana hip hop mbongo anafloo kama za Rado.Ngoma ni ya kitambo sana na video yake alitolea kwenye jumba ambalo alijakamilika(Pagara).
Ndani ya wimbo kuna maneno haya"KWA NINI NISHEREHEKEE SIKU YA KUZALIWA WAKATI WALIONIZAA HAWAPO?".

Nauomba.Asante.
 
" katapila nyamaza kulia,ukilia utaliza wengi ukiwa mbaya eeee"' inaitwaje hii Ngoma?
 
Natafuta wimbo unaitwa Akoreche morechare ndani yuko young dee, mucky na nani wengine sijui.. Kipindi hiko wako chini ya maxrioba na authentic studio
 
Huo wimbo namba 3 unaitwa Shani umeimbwa na Issa E & Lil Bio ft B.o.b(bob junior wa sasa kipindi hicho alikuwa ana rap)

Sikili sikili sikilizaaa aaaa sikiliza X2
Shani nakupendaaa,shani wangu nakupedaa oooo ninakiupenda shida ninazozipata anajua ye Mwenyezi X2


Verse 1 Lil Bio
Siga zote mi nakupaaaa,na kumshukuru Mwenyezi
Kwa kunijalia kukupata wangu mpenzi.

HATA MM NIMEUTAFUTA BILA MAFANIKIO
Wakuu mwenye hizi nyimbo kwenye library yake anisaidie tafadhali:
1. Tid - Sauti ya dhahabu
2. Ney - Mitego
3. ??( nimemsahau msanii na wimbo) kiitikio kimeimbwa
"Shani wangu nakupendaaa ooh mi nakupendaaa,
Shida nilizozipata anajua ye mwenyeeeziiii..x3"


Nawasilisha
 
Mwenye nyimbo hz plz
Lg mobb-Mgambo
Kigwema-Naacha mzk
Kigwema-Bint skendo
Issa E & Lil bio-Shani
Waridi ft h baba-dear
Sir robby ft chege-Usiniache
Master Vapour-Hunifai
Zozowida-kwa mjomba kalanganzule
Mona baby ft pasha-Shoe shine
 
Nautafuta wimbo mmoja hivi uliimbwa kati ya 1999 na 2000's
Kwenye kiitikio unaimbwa " If I cant get you" sina uhakika na muimbaji kama ni Brandy, Yolanda, Monica ama nani ila ni mdada wa Kimarekani. Akiwa amemshirika kati ya Jay Z ama Rakeem[emoji120]
 
Habari wadau...
Kuna wimbo nautafuta atakayenisaida kuupata ntampa hela ya bando la wiki...
Huo wimbo nahisi Ni wagosi wa Kaya au Dani msimamo na Mr. Ebo nilikua mdogo kipindi hicho... Moja ya mistari kwenye kiitikio ilikua hivi...

Narudi nyumbani nimechoka maisha
Na huku mjini ninataabika
Narudi nifanyeje
Naomba mnipokeee ...
 
Back
Top Bottom