Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Wadau natafuta wimbo mmoja hivi ni kama rumba umeimbwa kiswahili nahisi na lingala, tbc1 walikua wanauonyesha sana miaka ya nyuma.
Unaimbwa "ya rabanna sikuiba, ya rabanaa sikuua........."
 
Wakuu nifanyieni msaada wa nyimbo hizi:
1. Mpende akupendae -Tot akiwemo marehemu banza stone na waziri sonyo

2. Eda - hii ni taarab uliimbwa na kundi la Babloom kina Seif Kisauji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Kuna nyimbo na Mimi nazitafuta
1 - Ya TOT PLUS Wanaimba “Ooh ooh dada eee, Usilie na Mimi dada, mpenzi wako Mimi sija mwita eee, kaona mambo wewe huyawezi, ndipo kaja kwangu” Abdul Misambano yupo humo ndani
 
Deo mwanambilimbi feat banana zoro "siwezisema kwanini nliachana na yeye, mapenz yangu nae yalikua ya hadithi"
Kama hiyo
Abdul misambano na TOT band..." oooh kakaee usilie na mimi babaaa , mpenzi wako mimi sijamwita eeeh...kaona mambo wew huyawezi ndio kaja kwanguuu"
Kaka hiyo Ngoma kama unayo naomba nitumie ama kama una link ya hiyo nyimbo pia tafadhali naomba
 
Nautafuta wimbo unaitwa KITAMBO KIDOGO wa BDP KAMILI.

Aisee mwenye nao
 
Ninatafuta wimbo wa YAKI, ni mshaji wa Iringa. Wimbo unaitwa Mshkaji Wangu.
Chorus yake inaimbwa
"Yes,, ungenikubalia yote yasingetokea,
Yes, bora ningekaa kimya kilichokuja tokea"

Kuna verse anachana,

"Unakumbuka shule, ulianza kama masihara,
Day moja nilikuotea class na pack ya sigara,
Ukajitete kwamba unafanya biashara,
Leo umelose brain kila kitu kwako hasara,
Mathe sio sana ila geo ulikua kichwa,
Na uliapa iko siku siku ndege utakuja kuirusha,
Ila leo hata baskel tu unaangusha,"
 
Kuna wimbo kiitikio wanaimba "Acha waseme ninachokupa hawajui kwa maneno yao kwetu taf kasirika honey nadhani humo wameshirikishwa kina mandojo mwenye kujua jina la wimbo msaada please
 
Kama kuna mdau ana nyimbo za Hongera wa michano mfano round ya pili,mashabiki na baadae apandishe hapa tafadhali..
 
Kuna wimbo unaimbwa;

Ooh nikuite jina gani mpenziii,
Ujuwe nakupendaa.

Sauti ya mdada jamani km Kuna mtu anajua jina la muimbaji,au jina la wimbo anisaidie kunikumbusha,au mwenye nao akiniwekea itakua poa sana.

Na Kuna wimbo unaitwa;
miss bongo wa jaji hakim,
Msaada wakuu nimeutafuta sana bila mafanikio.
 
Msaada jamani naomba nyimbo mbili ila majina ya nyimbo Sina uhakika;
1; Bui Bui - Nenda
2; Fred - Nalizwa
Nawasilisha ombi kwenu Wakulu.
 
Natafuta ile tune inayopigwa na brass band pindi Rais akiapisha mawaziri, mabalozi au viongozi wowote.

pia hupigwa sana kwenye sherehe na dhifa za kitaifa.
pwi...pwi..... pwipwipwi......pwi....pwiriiiiiiii X2

pwiiiiii...... pwipwipwipiriiiii.....pwipwipwipiriiiii.

pi...pi...pi...pi...piiiiiiiiiii.
 
Kama kuna mdau ana nyimbo za Hongera wa michano mfano round ya pili,mashabiki na baadae apandishe hapa tafadhali..


 
Back
Top Bottom