NIDA yangu imefutika kabisa, personal details zote hazionekani kimebaki ki card blank tu. Je Kuna uwezekano wa kupata on same day?

Mnashangaa NIDA? Ukitaka ku renew passport unaanza upya utafikiri data zako huwa wanazi delete kwenye system. Miaka na miaka tunauliza kwanini unaanza kujaza form upya unajaza vitu vile vile ambavyo vipo kwenye database ya uhamiaji na NIDA?
Kwa kifupi ukitaka kufanya application ya chochote huku bongo wana act kama hawakutambui!
 
Nadhani ni swala la kiongozi wa nchi kuamua kuwawajibisha hao wanaosimamia hizo sekta. JPM was on the right path. Hiyo kitu inawezekana sema serikali yetu Ina deal na mambo mengi madogomadogo ambayo hayaishi na kukosa muda wa kufix issue muhimu kama hizi. Tutafika lakini japokuwa itachukuwa muda
 
Itakuwa aliwapa maelekezo Wachina wampe mashina za kuchekecha materials
😀😀😀. Huo ndo ukweli, wanajari big margin bila kuzingatia namna itakavyosumbua jamii.
Ila nahisi walikuwa na plan ya kutucharge fee ya kutengeza kingine ukipoteza au kikifutika. Wew haujiulizi haka ka card ka cost 20,000 mpaka 30,000 wakati material yake yote ya kukatengeneza hayazidi hata 2000?
 
Kweli? Hii mpya..
Siyo jambo jipya hilo.

Wakiingiza # ya NIDA kwenye mfumo namba na jina vinaonekana kisha wanaprint, lakini inakuwa siyo card original na kinafanya kazi kama kawaida.

Mi mwenyewe natembea na photo copy kuepuka adha ka'izi.
 
Siyo jambo jipya hilo.

Wakiingiza # ya NIDA kwenye mfumo namba na jina vinaonekana kisha wanaprint, lakini inakuwa siyo card original na kinafanya kazi kama kawaida.

Mi mwenyewe natembea na photo copy kuepuka adha ka'izi.
Hiyo huduma inapatikana wapi mkuu?
 
Pale nyuma ya id wameweka katazo la kufanya reprinting ile id. Any guy who reprints commits an offence.
Kabisa, sema wabongo tunachukulia mambo kidogo. Na nadhani wameamua kutofuatilia makusudi because wanatambua na wao ni sehemu ya tatizo hili.
 
Kabisa, sema wabongo tunachukulia mambo kidogo. Na nadhani wameamua kutofuatilia makusudi because wanatambua na wao ni sehemu ya tatizo hili.
Mimi natumia copy baada ya jamaa kunizungusha almost mwaka sasa.
Nilifanya maombi ya id mpya mwaka jana, hadi leo hii sijapata ila nilichoona wamefanyia kazi mabadiliko niliyoyafanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…