Nifahamishe kituo cha watoto yatima chenye uhitaji mkubwa sana

Mkuu swala la mchongo na uhitaji wa walionao watoto husika havihusiani.

Nitakuwa sawa namimi nikisema hao wazazi walitakiwa wajiandae kabla,sio kuja kukosa sabuni,Yess si ndio namna Bora ya kutafuta visababu!!!
 
Anza na ndugu zako na wanaokuzunguka wenye mahitaji.

Charity begin at home.
Hapa ndipo tunapo feligi wanadamu, ni kweli unatakiwa kuangalia kwanza watu wakaribu yako ukiona umesha malizana nao haya nenda sasa extra miles ndipo baraka zitakufuata, sio et unaenda kutoa misaada mbali huko wakati wafanya kazi wako wenyewe wana lia lia njaa kali wewe ni sawa na haujatoa msaada tu.
 
Ikiwa ni mpaka mtu ayamalize matatizo ya ya familia yake, ndugu zake, ya mtaani kwake, ndiyo atawasaidia wengine, basi ni wachache sana watakaomudu kuwasaidia wahitaji, ama wanaweza wasiwepo kabisa .

Ujue, wakati kwa wengine kula ugali dagaa kila siku kunaonekana ni umaskini, kuna wasiokuwa na uhakika wa kupata alau kikombe cha uji mkavu.

Kuwasaidia wengine si mpaka ujitosheleze kwanza wewe, ni suala la upendo.

Unaweza ukaamua kutenga asilimia kumi au tano ya kila senti uipatayo kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji.
 
Ni kweli vipo vya mchongo, lakini pia vipo vinavyotoa huduma kwa uaminifu.

Comments zingine humu zimenisikitisha sana! Nilishawahi kufanya kazi kwenye kituo cha watoto! Uzoefu nilioupata ulibadilisha kabisa mtazamo wangu.

Jambo kubwa nililojifunza ni kuwa HATA WATOTO YATIMA/WA MITAANI NAO NI WATOTO.

Wanastahili kupendwa na kujaliwa kama watoto wanaoishi na wazazi wao wanvyopendwa na kujaliwa.
 
Ukisoma comments ndio utaelewa ile takwimu ya Tanzania kua nchi ambayo wananchi wake hawana furaha... mtu akikosa furaha anakua na negativity muda wote, akili inaganda, kila kitu kwake kinakua kibaya, anakua ana roho mbaya.

Inahuzunisha
Na sababu mojawapo ya mtu kukosa furaha ni ubinafsi, unamkuta muda wote anajifikiria yeye tu.

Lakini ambaye ana tabia ya kuwatanguliza wengine, si rahisi furaha impige chenga kama inavyowachenga waliouweka mbele "umimi"
 
Vituo vyote vina uhitaji ndiyo maana vikaitwa "Vituo vya watoto yatima"
Ni kweli. Lakini katika utoaji huduma, kuna baadhi ya wahudumu wa hivyo vituo wanaoishi kujimilikisha vitu vinavyotolewa msaada kwa ajili ya watoto.

Na kuna ambavyo watumishi wake ni waaminifu kiasi kwamba hata kama ni kipande cha sabuni watahakikisha kuwa kinawafikia walengwa.
 
Huyu jamaa kuna fursa anataka kuitumia kupitia kituo hicho ,kama una uwezo wa kuwasaidia bila kuwa na manufaa yako binafsi sidhani kama unashindwa kujua pakusaidia bila kuomba huku,wewe huna tofauti na wale "tuma kwa namba hii"
 
Huyu jamaa kuna fursa anataka kuitumia kupitia kituo hicho ,kama una uwezo wa kuwasaidia bila kuwa na manufaa yako binafsi sidhani kama unashindwa kujua pakusaidia bila kuomba huku,wewe huna tofauti na wale "tuma kwa namba hii"
Unahisi anataka aombe michango ya kununulia vitu vya kuwpaelekea watoto wahitaji?

Mimi sidhani kama hiyo ndiyo nia yake. Shauku yake ni kupata mahali sahihi pa kuupeleka msaada uliopatikana. Si unajua JF ni mahali unakoweza kupata taarifa sahihi? Naamini ndicho kilichomvutia mdau kuuleta Uzi wake humu. Anajua atapata taarifa zisizoghushiwa.
 
Dream organisation ipo Arusha wana Web yao naona jamaa anasomesha watoto wenye mazingira magumu kweli maana anawatoa vijijini huko...cheki nao hao kama unataka kutoa msaada ipo Murieti...
 
Na sijasema mpaka ujitosholeze. Kwa taarifa yako kujitosheleza ni neno relative na kuna watu wanaweza wasijitosheleze kamwe. Nimesema wale ambao hawakumbuki kabisa walio karibu na kuzingatia walio mbali. Watu wa aina hii wako. Unakuta mtu wazazi wake au ndugu zake wako hohehahe lakini hana habari nao na badala yake anaonekana kwenye social media akisaidia watu wa mbali.
 
Vituo vyote vina uhitaji ndiyo maana vikaitwa "Vituo vya watoto yatima"
Uhitaji unatofautiana jamani, mjitahidi sana kufanya charities mjionee, kuna vituo mfano dogo dogo center wale wako mbali sana, ufadhili wao ni mkubwa, watoto wanaishi kishua.... kuna kituo kipo Kisarawe ukifika tu chozi litakutoka mazingira ya pale hadi watoto wanakuomba uwachukue, nawapenda walivyo na upendo na ukarimu tho [emoji847][emoji3059]..... so yupo sahihi kuulizia hivyo
 
Kuna kituo kinaitwa Watoto wetu Tanzania nimekifahamu kituo hiki tokea mwaka 2008 zamani kilikuwa kimara Suka, baada ya ile bomoa bomoa zaidi wapo Goba, kiukweli kina uhitaji mkubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…