Nifanyeje? Upweke unatafuna moyo wangu vibaya mno

Asikwambie mtu, upweke ni balaa.
Mtu anakunywa bia 4+ anarudi nyumbani anakunywa dawa za usingizi waapi macho hayafumbi hadi asubuhi.

Na kama si upweke kuna kitu kinaitwa anxiety, sema vinatibika mtu akiwaona wataalam wa afya.

Usingizi ni dawa.
Balaa kweli bora hata uoe kama ndoa ikikushinda itakuwa umejifunza kitu.
 
vuta pisi kali ndani gentleman,
nakuhakikishia, kwa kufanya hivyo utakua umeondokana na kumaliza kabisaa kadhia ya upweke wenye mawazo mengi, majuto na roho ya kukata tamaa, na hatimae utaopata pumzi mpya maishani na wepesi wa ajabu katika kazi na majukumu yako ya kila siku.

Mungu akubariki sana, Aimen πŸ’
 
Umejaribu kuoa ukakataliwa? Kuna single wengi tu mtaani wanatafuta was kuishi nao wewe umekwama wapi?
 
Mkuu, Chukua likizo fupi ya siku saba, safiri kokote ambako hujawahi kufika au kuishi.
Chukua chumba cha wageni kwa siku tatu, kula vizuri lala na kupumzika sana siku hizo tatu na uepuke kunywa pombe au kunywa kidogo.
Jichanganye na wenyeji, fanya udadisi wengine wanaishi vipi na ujaribu kusahau shughuli zako za kila siku .... Raha jipe mwenyewe!

Baada ya siku hizo saba rudi kazini kwako ulete mrejesho hapa.

Angalizo: Kama tatizo ni pesa, huo ushauri hapo juu hautasaidia kitu....Tafuta pesa!.
 
😭😭😭😭😭😭 Roho inataka kutoka hapa na sijui chanzo ni nn!
Tatizo lenu wanaume wagumu kulia
Ingekuwa unaweza kila siku kulia walau hata nusu saa hio hali ingekuondoka
Pole sana...
Km muuminini wa dini na unaamini Mungu basi sali tu sana. Mungu Atakupa furaha ya kudumu
 
Ndugu fanya uoe then kama itakuwa bado utabadilisha mawazo ,sisi tunaishi maisha bila ya wenza ni hatari sana hata wanyama wana wenza wao.
 
1. IPO he
2. Sina apart from sex, kula, kulala
3. Ntajaribu 😁

1. Tumia muda unaokjwa idle kupanga matumizi ya pesa zako. Ukishapanga kesho yake kaa tena panga upya matumizi mengine hedi hela uliyonayo uone haitoshi, kisha toka katafute pesa nyingine.

2. Can't say anything on sex. Go to different restaurants hadi level za mama ntilie kuka mapishi tofautitofauti, ukichoka anza kupika mapishi tofautitofauti ule ladha unayoipenda. Nunua godoro zuri lala kila unapokuwa na muda. Tafuta namna ya kulala kwa haraka.

3. All the best.
 
More money more problem.

Jaribu kufanya mazoezi ya kuituliza akili ,roho na nafsi huitwa Meditation and tyr to lower ur Expectation in ur life

At the age of 35 only you need is good health physically & mentally, so stay humble .
 
Same here πŸ˜‡πŸ˜­.bora wewe unateketea..mimi nilishateketea.no happyness at all.
***** maisha haya bwana...
Usioe mwaya unaweza juta zaidi
Jaribu therapy ya kuendesha gari just for fun kwa muda mrefu ukisikiliza bang unazopenda.hii mimi inanisaidia!
 
Hayo yanayokuumiza yanatokana na kazi yako ama vipi?
 
Uko sahihi
 

Jambo la kuhakikisha unakuwa nalo ni kuwa financial stable .

Ila Mwanamke hana uwezo wa kuondoa upweke kwakuwa upweke ni tatizo la akili.

So Endapo utatafuta MTU , tafuta MTU kwa malengo ya kuwa na familia Ila sio ili akuondolee upweke au akupe furaha kwakuwa hakuna MTU mwenye uwezo wa kufanya yote hayo then meditation ndo dawa ya uhakika Just try it you will never regret
 
Ninaelewa sana mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…