Nifanyeje? Upweke unatafuna moyo wangu vibaya mno

Nifanyeje? Upweke unatafuna moyo wangu vibaya mno

Asee utu uzima dawa 🙄

Mimi ni mwanaume mtu mzima 35+ ila niseme ukweli moyo wangu unavuja damu za kutosha kila nikiingia nyumbani baada ya mihangaiko nakuwa na void moyoni isiyopimika

Sasa hivi kuna kazi inatakiwa nifanye ila nimeshindwa kabisa kufanya asee yaani najisikia kufa kufa hapa nilipo.

Kwa nje naji present kama mtu mgumu ila ndani nateketea vibaya mnoo nasikia kama mtu anachana chana huu moyo by the way naishi mwenyewe sijui ndo sababu au ni nn? Yaani najisikia vibaya kama mgonjwa hii kazi sijui nifanyeje nimevumilia nimechoka nipeni ushauri

Nikitafuta demu itasaidia? Japo Mungu hawezi kukupa vyote hilo nimeamini asilimia 100 😑
We unajuaje kama huyo moyo wako unachanwachanwa kwa ajili ya kukosa demu mpaka uamue kumtafuta kama sehemu ya suluhisho lako????
1. Yawezekana wingi wa majukumu uliyonayo ukilinganisha na muda wa kukamilisha majukumu hayo ndio mana unapata stress.
2. Yawezekana unafanya majukumu ambayo hauna uwezo nayo kitaalamu.
3. Yawezekana kazi zako hazitimizi malengo yako.
4. Yawezekana una malengo makubwa juu ya ukifanyacho.

Lielewe tatizo lako vizuri ndio utatue, huyo unaemkimbilia ndio atakuja petrol na kiberiti atekeze kabisa hiko kinacho chanwachanwa.
Ninachokiona kwako stress xako zinatokana na matumaini unayojiwekea juu ya jambo fulani ambapo kikienda tofauti haukubaliani na matokeo yake.

Demu unayrmtafuta kama hajakidhi kuhandle Stress zako anakuwa amekuongezea tene stress.

Relax, usiibebe dunia mabegani, acha matatizo yajitatue yenyewe.
 
Niliwahi soma kitabu kimoja, kuna sehem kinasema....

"Binadamu hata awe vipi kifedha, umashuhuri, power n.k, kuna nyakati huwa ndani ya nafsi yake anahisi upweke wa hali ya juu",

Alaf mwandishi akaelezea; Upweke huo ni nafasi ya Mungu, kuwa hata iweje kutakuwa na gap flan ivi utakayoihisi kwenye nafsi yako (upweke)...na gap hiyo inapaswa kuwa filled na Mungu....

Sijui ina ukweli kiasi gani, ila kiasi flani kwangu nasadiki
Hakuna gap(nafasi) yeyote ya Mungu.

Mungu hayupo.
 
Fanya kazi mkuu,kila mtu ni mpweke.Kama mimi hapa nina upweke ila nakomaa,ndo maisha yalivyo.Bora wewe unaonekana una mihela sie wengine ndo tafrani hali ngumu. Mimi ningekuwa na hali nzuri saa hii ningewasha gari huyoooo duniani kuona mambo yanayotokea usiku na refresh narudi.
Ni therapy nzuri na inasadia sana long drive
 
We unajuaje kama huyo moyo wako unachanwachanwa kwa ajili ya kukosa demu mpaka uamue kumtafuta kama sehemu ya suluhisho lako????
1. Yawezekana wingi wa majukumu uliyonayo ukilinganisha na muda wa kukamilisha majukumu hayo ndio mana unapata stress.
2. Yawezekana unafanya majukumu ambayo hauna uwezo nayo kitaalamu.
3. Yawezekana kazi zako hazitimizi malengo yako.
4. Yawezekana una malengo makubwa juu ya ukifanyacho.

Lielewe tatizo lako vizuri ndio utatue, huyo unaemkimbilia ndio atakuja petrol na kiberiti atekeze kabisa hiko kinacho chanwachanwa.
Ninachokiona kwako stress xako zinatokana na matumaini unayojiwekea juu ya jambo fulani ambapo kikienda tofauti haukubaliani na matokeo yake.

Demu unayrmtafuta kama hajakidhi kuhandle Stress zako anakuwa amekuongezea tene stress.

Relax, usiibebe dunia mabegani, acha matatizo yajitatue yenyewe.
True 100%

Solitude versus loneliness.
 
Asikwambie mtu, upweke ni balaa.
Mtu anakunywa bia 4+ anarudi nyumbani anakunywa dawa za usingizi waapi macho hayafumbi hadi asubuhi.

Na kama si upweke kuna kitu kinaitwa anxiety, sema vinatibika mtu akiwaona wataalam wa afya.

Usingizi ni dawa.
Lakini siyo uaotokana na pombe. Hii ni balaa
 
Sina familia ila uzoefu uliopo sikuzote haijalishi wanawake ni mara ngapi wanatuumiza na kutuuzi ila wana sehemu yao katika maisha ya kila mwanaume mwenyewe akili timamu. Hilo ndo jukumu umelikimbia ndio maana
 
Back
Top Bottom