Nifanyeje wanangu wawe na akili nyingi darasani

Nifanyeje wanangu wawe na akili nyingi darasani

Akili ya mwanadamu (IQ) huwa ni Genetic...ni vinasaba vya baba na mama ambavyo nao walilithi kutoka kwa mababu zao.

Mazingira + shule nzuri husaidi ku boost IQ aliyonayo mtoto, ambapo huchangia 20 to 30%.
 
Mimi binti yangu ananiona toka akiwa kadogo kabisa nikijisomea vitabu ,kakua kwenye hiyo hali yakuiga na yeye kupenda kujisomea ,kwa sasa nipo nae mbali ila hata tukiongea kwa simu tu anaomba nimletee vitabu vizuri vya stories mbalimabali .

Hii ilimjengea uwezo wa kupenda kusoma na kudadisi mambo mbalimabali, wewe kama mzazi matendo yako yanamchango mkubwa sana kumjengea mwanao mazoea mazuri au mbaya ambayo yatamjenga au kumbomoa kwenye makuzi yake na hata maisha yake ya baadae .

Wadada wengi wenye watoto na wazazi wengi wanapenda kushinda wanachati mda wote huku wakitaka mtoto wao apende kujisomea !! Apo Lazima wafeli tu.
Sasa sisi wazazi ambao tukitoka job tunapitia kupoza koo na kurudi home madogo wakiwa wameshalala unatuambiaje sasa.
 
Ukitaka kuwa na watoto vipanga darasani hakikisha unaoa mke kipanga haswa.Yaani mkeo awe mwerevu Kweli Kweli.

Then hakikisha watoto wako hawali ugali kbsa coz Ni chakula kinachodumaza akili.
Hiko kiparagrafu cha mwanzo……. Wasipokuelewa basi achana nao. 😅

Tutalaumu watoto bure tu.

Kuna utani nilisoma mahali, mwanaume anasema nimeshaoa mke kwaajili ya watoto wangu, sasa nikatafute mwanamke mwingine kwaajili yangu, if you know you know! 🤣
 
Akili hufuata mkondo,kama wazazi bichwa maji,likewise kwa watoto,hakuna dawa hapo ulikosea kuchagua mke kilaza kwa kuangalia shape badala ya kichwa
🤣🤣 kaka ndo useme bichwa maji si useme tu kuwa hawana akili! bichwa maji imekaa kikatili sana!
 
Miongoni mwa mambo ya maana katika hii dunia mbaya ya siku za mwisho ni Elimu. Kila mzazi anatamani kama mimi ninavyotamani wanangu wawe vichwa darasani katika masomo yao, lakini wengi, kama mimi pia tunaishia kutamani tu hasa tunapoona watoto wa wengine wakifanya maajabu katika masomo yao.

Kwangu mimi wanangu hawaendi nitakavyo, mimi pamoja na wanangu kusoma shule za binafsi, English mid. Anayejua siri ya watoto kufanya vizuri anipe wandugu.

Nimejitahodi kuwakazania kusoma na kuwasaidia mimi mwenyewe. Tuition za kufa mtu, vitabu nanunua. Wakifeli na fimbo wanapata, wakifaulu zawadi wanapata. Lakini sioni kufanya vizuri kule mimi ninakotaka, inaniuma sana.

NIFANYEJE
Labda ufanye vitu kwa kiasi. Pengine hizo tuitions za kufa mtu ndio unazidi kuchosha akili zao. Jaribu kuwa unawasliana kwa karibu na walimu wao wa darasa kujua zaidi changamoto zao. Wazazi wa siku hizi busy sana kutafta hela muda wa kuwa na watoto unakuwa mdogo. Fatilia vizuri na ratiba zao za nyumbani zilivyo wakitoka shule. Jitahidi vyakula kama parachichi, almonds zinasaidia mambo ya kumbukumbu.
 
usiangaike na elimu saizi angalia wanavipaji gani alafu wapesapoti yakutosha maisha yamebadilika saizi kylan mbape mtoto mdogo tu anakunja bilioni kadhaa kwa mwezi.
 
Uko sahihi 100%. Mimi baba yangu hakuwahi kunichapa hata ningekuwa karibu wa mwisho. Wala hajawahi kunigombeza kisa sijafanya vizuri darasani. Sema baadae nilikuja kumshtukia huwa anamalizia hasira zake kwenye makosa mengine yasiyohusiana na darasani. Yaani kipigo chake anaunganisha mambo yote.
Hahaaaa
 
Miongoni mwa mambo ya maana katika hii dunia mbaya ya siku za mwisho ni Elimu. Kila mzazi anatamani kama mimi ninavyotamani wanangu wawe vichwa darasani katika masomo yao, lakini wengi, kama mimi pia tunaishia kutamani tu hasa tunapoona watoto wa wengine wakifanya maajabu katika masomo yao.

Kwangu mimi wanangu hawaendi nitakavyo, mimi pamoja na wanangu kusoma shule za binafsi, English mid. Anayejua siri ya watoto kufanya vizuri anipe wandugu.

Nimejitahodi kuwakazania kusoma na kuwasaidia mimi mwenyewe. Tuition za kufa mtu, vitabu nanunua. Wakifeli na fimbo wanapata, wakifaulu zawadi wanapata. Lakini sioni kufanya vizuri kule mimi ninakotaka, inaniuma sana.

NIFANYEJE
Wenda wapo na talent kubwa hujagundua
 
Back
Top Bottom