Mkuu haukukosea kujiita andrew tate maana umeelezea hii inshu kwa undani kabisa na uhalisia wake kama ambavyo the Top G alivyo.
Wazazi ndio watu wa kutupiwa lawama pale ambapo mtoto anakuwa ni kilaza shuleni,hakuna mwingine.
Binafsi nilipoigundua hii siri ya kwamba akili ya mtoto inakuwa kwa mujibu wa mazingora na malezi basi nikawa makini sana na kijana wangu.
Nikaanza kumshirikisha kwenye kazi ninazofanya nyumbani kama vile kung'oa majani na kuyaweka kwenye mifuko na kwenda kutupa.
Au kufua nguo naye huwa namuwekea beseni lake na nguo huku akifua na niasema kabisa "baba tufue nguo" ili misamiati hiyo iingie kichwani mwake na kutengeneza uwezo mpya katika ubongo.
Hata kama kazi inanzofanya hatofanya kama mimi ila lengo ni kumuongezea uwezo na kulanua ubongo wa mtoto ili ije kumsaidia huko mbeleni.
Watu wengi hawafahamu kwamba kila jambo analojifunza mtoto kwa kufanya ama kuongea basi jambo hilo linaenda kufungua milango fulani kwenye ubongo na hatimae sasa mlango unakuwa wazi na linapotokea jambo fulani ambolo linafanana kidogo ama sana na jambo lileee ambalo lilifungua mlango basi unakuta mtoto ni rahisi kuelewa kwa sababu mlango ulishafunguka.
Siku moj nilimkuta mwanangu amefungua bomba la maji anachezea yale maji yanayochuruzika hiku akipitisha mkono kana kwamba alitarajia yale maji yatakwamisha mkono wake kama ilivyo kamba,lakini haikuwa hivyo na aliendelea na mchezo huo,binafsi nilijua kwamba hapo kuna kitu anatafiti japokuwa mwenyewe hajui kama anatafiti na hawezi kusema kwamba baba ee hapa nafanya utafiti ila unconsciously anatafiti(curiosity)na utafiti huo unaenda kufungua milango mlango wa ufahamu katika ubongo wake.
Imagine leo mzazi anamkuta mtoto anachezea maji eti anampiga na kumkataza,ukatili ulioje huu.
Lakini pia kazi ndogondogo ambazo utamshirikisha mtoto naye azifanye alaafu akawa anazifanya hata kama sio kwa ukamilifu,hapo maana yake unamtengeneza mtoto awe na tabia ya kuelewa yaani kule kufanya kwake hizo kazi basi kazi hizo zinaenda kufungua milango ya kuwa muelewa kwenye akili yake.
Yaani maanayake ni kusema kwamba kama ameelewa task nyingi anazopewa nyumbani vipi atashindwa kuelewa task za shule ?
Hapo sasa tunamtengeneza mtoto awe na tabia ya kuelewa na mimi huu ndio msemo wangu kwa watoto kwamba KUELEWA NI TABIA,hivyo tabia hiyo inatakiwa ianzie nyumbani.
Na ili tabia hiyo ianze nyumbani basi lazima mzazi awe anamfundisha mwanawe mambo mbalimbali nyumbani na ashirikiane nae kufanya kazi za nyumbani.
Kama mama anamenya vitunguu swaumu basi mpe na mtoto naye amenye hata kama hatofanya kwa usahihi ila unamtengeneza akili iwe komavu kuhandle tasks anazopewa.
Kama inaosha vyombo mpe chombo naye ashikeshike hata kama ni vya kuvunjika mpe hata akivunja kimoja atajua kwamba kumbe vinavunjika,hiyo itakuza akili.
Haya yote yanachangia katikabkukuza uelewa wa mtoto na kumfanya awe na akili njema.
Wazazi wanaogopa kuwapa task watoto nyumbani kwa kudhani hawastahili lakini ndio wanawauwa vibaya sana na kuwafanya wawe na akili iliyojifunga ambayo haina experience na vitu vingi.
hAta kwenye kula mtoto wa miaka mi3 utakuta analishwa eti kisa yeye hawezi kula vizuri,muache ale hata akimwaga chakula chini mwache aenjoy utoto wake na muda sio mrefu ataweza kula vizuri.
Yapo mengi ya kuandika kwa kuwaelimisha wazazi,nikushukuru sana bwana
Andrew Tate ate kwa mchango wako murua ambao nilikuwa nautafuta kwenye comment karibia zote.