Nifanyeje wanangu wawe na akili nyingi darasani

Nifanyeje wanangu wawe na akili nyingi darasani

Akili ya darsani inategemea mazingira ya nje zaidi na sio inborn.
Hapana, In born nature inaifluhence sana akili ya mtoto.
Binafsi nimezaliwa na wazazi wenye akili sana, Na watoto wote katika familia ni wenye akili, za darasani na hata za utatuzi wa mambo mbalimbali.
Tatizo nililojifunza ni kwamba kuna tofauti ndogo sana kati ya akili nyingi na ukichaa.
 
Albert Einstein alipokuwa mvulana mdogo akiwa shuleni, uwezo wake ulikuwa mbovu kiasi kwamba mwalimu alifikia hatua ya kumuambia aache shule kwani hawezi kuja kufanikisha chochote. Lakini ndiye alikuja kuwa winner wa nobel prize 1921, tuzo za heshima kubwa sana duniani.

Thomas Edison mwanasayansi aliyegundua bulb, kipindi ni mvulana mdogo akiwa shuleni uwezo wake darasani ulikuwa mbovu kiasi kwamba mwalimu wake akamuambia ''wewe ni mjinga sana na huwezi ukaelewa chochote'', Siku moja dogo kipindi anatoka shuleni, akamuambia mama yake "mama mwalimu kanipatia karatasi hii, lakini kaniambia usome ni wewe pekee unapaswa kusoma, kwani barua hio inasemaje mama?"
Mama alibubujikwa na machozi na akasoma ile karatasi kwa sauti "mtoto wako ni genius sana, hii shule ni ndogo sana kwake na hakuna walimu wanaoweza kumfundisha, tafadhali mfundishe mwanao mwenyewe."

Miaka mingi baadae baada ya mama yake na Thomas Edison kufariki na Edison amekwisha kuwa mwanasayansi mkubwa wa karne aliweza kukuta ile barua kwenye kabati la nguo la mama yake, kumbe kile kikaratasi kiliandikwa "mtoto wako ana upungufu wa akili, hatuwezi kumuacha aendelee na shule yetu, tumemuachisha shule", kwa lugha ya kiingereza mentally deficiency tukitafsiri ni mtu mwenye upungufu wa akili, wengine huku wanasema dishi limecheza, sasa you can imagine Edison uwezo wake ulivyokuwa mdogo darasani.

Baadae Edison aliandika kwenye diary yake “Thomas A. Edison was a mentally deficient child whose mother turned him into the genius of the century.” --
Akiwa na maana kwamba "Thomas A. Edison alikuwa mtoto mwenye upungufu wa kiakili ambaye mama yake alimgeuza kuwa genius wa karne hii."

Hio tunaita ni nguvu ya maneno, maneno ya mama yalimfanya mtoto awe mgunduzi wa bulb ambayo tunaitumia leo, mkuu jaribu kukaa karibu na watoto wako, wapende, wajali, wape moyo, usiwachape hovyo na kuwaita wajinga ukifikiri unawajenga wakati unawaua ndani kwa ndani, ndio watoto wako Mungu kakupa hakuna wengine, mbeleni wanaweza kuja kufanya maajabu kama Edison 🙂
Una akili kubwa☺️
 
Mkuu haukukosea kujiita andrew tate maana umeelezea hii inshu kwa undani kabisa na uhalisia wake kama ambavyo the Top G alivyo.

Wazazi ndio watu wa kutupiwa lawama pale ambapo mtoto anakuwa ni kilaza shuleni,hakuna mwingine.

Binafsi nilipoigundua hii siri ya kwamba akili ya mtoto inakuwa kwa mujibu wa mazingora na malezi basi nikawa makini sana na kijana wangu.

Nikaanza kumshirikisha kwenye kazi ninazofanya nyumbani kama vile kung'oa majani na kuyaweka kwenye mifuko na kwenda kutupa.

Au kufua nguo naye huwa namuwekea beseni lake na nguo huku akifua na niasema kabisa "baba tufue nguo" ili misamiati hiyo iingie kichwani mwake na kutengeneza uwezo mpya katika ubongo.

Hata kama kazi inanzofanya hatofanya kama mimi ila lengo ni kumuongezea uwezo na kulanua ubongo wa mtoto ili ije kumsaidia huko mbeleni.

Watu wengi hawafahamu kwamba kila jambo analojifunza mtoto kwa kufanya ama kuongea basi jambo hilo linaenda kufungua milango fulani kwenye ubongo na hatimae sasa mlango unakuwa wazi na linapotokea jambo fulani ambolo linafanana kidogo ama sana na jambo lileee ambalo lilifungua mlango basi unakuta mtoto ni rahisi kuelewa kwa sababu mlango ulishafunguka.

Siku moj nilimkuta mwanangu amefungua bomba la maji anachezea yale maji yanayochuruzika hiku akipitisha mkono kana kwamba alitarajia yale maji yatakwamisha mkono wake kama ilivyo kamba,lakini haikuwa hivyo na aliendelea na mchezo huo,binafsi nilijua kwamba hapo kuna kitu anatafiti japokuwa mwenyewe hajui kama anatafiti na hawezi kusema kwamba baba ee hapa nafanya utafiti ila unconsciously anatafiti(curiosity)na utafiti huo unaenda kufungua milango mlango wa ufahamu katika ubongo wake.

Imagine leo mzazi anamkuta mtoto anachezea maji eti anampiga na kumkataza,ukatili ulioje huu.

Lakini pia kazi ndogondogo ambazo utamshirikisha mtoto naye azifanye alaafu akawa anazifanya hata kama sio kwa ukamilifu,hapo maana yake unamtengeneza mtoto awe na tabia ya kuelewa yaani kule kufanya kwake hizo kazi basi kazi hizo zinaenda kufungua milango ya kuwa muelewa kwenye akili yake.

Yaani maanayake ni kusema kwamba kama ameelewa task nyingi anazopewa nyumbani vipi atashindwa kuelewa task za shule ?

Hapo sasa tunamtengeneza mtoto awe na tabia ya kuelewa na mimi huu ndio msemo wangu kwa watoto kwamba KUELEWA NI TABIA,hivyo tabia hiyo inatakiwa ianzie nyumbani.

Na ili tabia hiyo ianze nyumbani basi lazima mzazi awe anamfundisha mwanawe mambo mbalimbali nyumbani na ashirikiane nae kufanya kazi za nyumbani.

Kama mama anamenya vitunguu swaumu basi mpe na mtoto naye amenye hata kama hatofanya kwa usahihi ila unamtengeneza akili iwe komavu kuhandle tasks anazopewa.

Kama inaosha vyombo mpe chombo naye ashikeshike hata kama ni vya kuvunjika mpe hata akivunja kimoja atajua kwamba kumbe vinavunjika,hiyo itakuza akili.

Haya yote yanachangia katikabkukuza uelewa wa mtoto na kumfanya awe na akili njema.

Wazazi wanaogopa kuwapa task watoto nyumbani kwa kudhani hawastahili lakini ndio wanawauwa vibaya sana na kuwafanya wawe na akili iliyojifunga ambayo haina experience na vitu vingi.

hAta kwenye kula mtoto wa miaka mi3 utakuta analishwa eti kisa yeye hawezi kula vizuri,muache ale hata akimwaga chakula chini mwache aenjoy utoto wake na muda sio mrefu ataweza kula vizuri.

Yapo mengi ya kuandika kwa kuwaelimisha wazazi,nikushukuru sana bwana Andrew Tate ate kwa mchango wako murua ambao nilikuwa nautafuta kwenye comment karibia zote.
Mkuu umeeleza vema ila kazi za nyumbani hazina msaada wa kutosha kumsaidia mtoto kufanya vizuri darasani. Genetics inahusika kwa 100%. Uwezekano wa vilaza kuzaa mtoto kipanga ni mdogo. Utakuta familia ya watoto 6 ni mmoja tu kipanga.
 
Kinachofanya mtoto awe na uwezo mzuri darasani ni two factors:
1. Hereditary factor - biological factor
Kwenye hiyo factor baba ukiwa na elimu ya kuunga unga na mam elimu ya kuokoteza okoteza basi hata ikitokea baba ukabahatisha kupata fedha za kutosha na uwezo mkubwa wa kiuchumi usije tegemea mtoto wako atakuwa na akili darasani.

Na ndio maana mnapotaka kuoa mnashauriwa usichague mwanamke kwa kuangalia shepu lake mkadhani mwanamke akiwa na mshepu ndio akili, matako makubwa sio indicator ya kusema huyu mwanamke atanizalia watoto ambao watakuwa bright, au mwanamke mweupe ukadhani uzuri - weupe wake mwanamke ndio utafanya watoto wawe na akili. HILO SAHAU KABISA.
Wanaume wengi walio oa wanafeli kwenye hili.

2. Factor ya pili ni environment unayowalelea watoto wako. Ukiwalea watoto kwenye mazingira duni don't expect kuwa watakuwa na akili darasani. Lakini hii factor ni supplement tu kwenye factor namba moja hapo.

Kwa maana nyingine hata uishi masaki, osysterbay, mikocheni etc with very good life lakini una mwanamke akili kisoda au wewe mwenyewe akili yako ya kitapeli tapeli tu halafu ndio ukaangukiwa na bahati ya mtende kuwa na FEDHA, ndugu yangu hata ufanye vipi toto lako litaendelea kuwa la hovyo hivyo hivyo.

Imagine mke darasa la saba, baba diploma au degree ya kuunga unga halafu mtoto awe na akili darasani kweli kwa ku-compete na watoto wenye mama zao ambao ni Bachelor degree holders? Hiyo sahau mkuu, kwa maana ya never ever!

Ulishapotea kwenye kufanya choice ya mke wa kuoa.

NB: MIMI NDIO MAANA KWENYE TANGAZO LANGU LA KUTAFUTA MKE NIMEKUWA VERY CLEAR - mwanamke awe Bachelor degree holder or above it na wala sitaki mwanamke mwenye elimu ya kuunga unga eti mara nilisoma certificate mara diploma, no please 🥺

Kaka ulishayakanyaga, endelea kukomaaa tu na hali yako
Mtu asiye na akili anatakiwa ashauriwe na mtu mwenye akili, By the way degree sio akili.
Degree ya kuungaunga inategemeana mtu amepita katika changamoto zipi za kielimu na kimaisha.
 
Hapana, In born nature inaifluhence sana akili ya mtoto.
Binafsi nimezaliwa na wazazi wenye akili sana, Na watoto wote katika familia ni wenye akili, za darasani na hata za utatuzi wa mambo mbalimbali.
Tatizo nililojifunza ni kwamba kuna tofauti ndogo sana kati ya akili nyingi na ukichaa.

Tatizo watu mnaubishi Sana.
 
Miongoni mwa mambo ya maana katika hii dunia mbaya ya siku za mwisho ni Elimu. Kila mzazi anatamani kama mimi ninavyotamani wanangu wawe vichwa darasani katika masomo yao, lakini wengi, kama mimi pia tunaishia kutamani tu hasa tunapoona watoto wa wengine wakifanya maajabu katika masomo yao.

Kwangu mimi wanangu hawaendi nitakavyo, mimi pamoja na wanangu kusoma shule za binafsi, English mid. Anayejua siri ya watoto kufanya vizuri anipe wandugu.

Nimejitahodi kuwakazania kusoma na kuwasaidia mimi mwenyewe. Tuition za kufa mtu, vitabu nanunua. Wakifeli na fimbo wanapata, wakifaulu zawadi wanapata. Lakini sioni kufanya vizuri kule mimi ninakotaka, inaniuma sana.

NIFANYEJE
wako english medium scholl?
 
Mama ni wa la saba tu, baba ana diploma ya IT, na anadigrii ya uongozi na maendeleo ya jamii, pia anacheti ya veta ya udereva. Huyo bado sio, hata kwao baba ndugu zake ni wasomi waziristan tu hata mzazi wa baba naye msomi mzuri tu.
Mkuu wala usifikirie vibaya watoto ni umri tu watakaa sawa mama yao kuishia la 7 haina maana hana akili bali ni kwamba hakupata nafasi ya kusoma tu yawezekana akawa na akili kuzidi ata ww sema kwa kuwa hakupata hiyo nafasi tena usije ukaanza kumtamkia maneno machafu kwa kuchukua maneno ya wadau humu ukiamini labda wameiga kwake hicho kitu hakipo mkuu,watoto wanachukua kote kwa baba na mama pia wengine wanakuwa na akili za peke yao
Hivyo tuliza akili wakijitambua wata ku surprise amini hilo mkuu
Wapo watoto ambao wazao wao ni vilaza tena wale mburura lakini wamekuwa best students katika mitihani yao na kufsnikiwa kusoma special schools tunazozifahamu kama mzumbe,ilboru n.k
Muombe Mungu abariki kizazi chako usiwe na imani potofu ukaanza kumsingizia mama yao
 
Akili huanzia kutoka kwa wazazi, inavyosemekana...

Cc: Mahondaw
 
Albert Einstein alipokuwa mvulana mdogo akiwa shuleni, uwezo wake ulikuwa mbovu kiasi kwamba mwalimu alifikia hatua ya kumuambia aache shule kwani hawezi kuja kufanikisha chochote. Lakini ndiye alikuja kuwa winner wa nobel prize 1921, tuzo za heshima kubwa sana duniani.

Thomas Edison mwanasayansi aliyegundua bulb, kipindi ni mvulana mdogo akiwa shuleni uwezo wake darasani ulikuwa mbovu kiasi kwamba mwalimu wake akamuambia ''wewe ni mjinga sana na huwezi ukaelewa chochote'', Siku moja dogo kipindi anatoka shuleni, akamuambia mama yake "mama mwalimu kanipatia karatasi hii, lakini kaniambia usome ni wewe pekee unapaswa kusoma, kwani barua hio inasemaje mama?"
Mama alibubujikwa na machozi na akasoma ile karatasi kwa sauti "mtoto wako ni genius sana, hii shule ni ndogo sana kwake na hakuna walimu wanaoweza kumfundisha, tafadhali mfundishe mwanao mwenyewe."

Miaka mingi baadae baada ya mama yake na Thomas Edison kufariki na Edison amekwisha kuwa mwanasayansi mkubwa wa karne aliweza kukuta ile barua kwenye kabati la nguo la mama yake, kumbe kile kikaratasi kiliandikwa "mtoto wako ana upungufu wa akili, hatuwezi kumuacha aendelee na shule yetu, tumemuachisha shule", kwa lugha ya kiingereza mentally deficiency tukitafsiri ni mtu mwenye upungufu wa akili, wengine huku wanasema dishi limecheza, sasa you can imagine Edison uwezo wake ulivyokuwa mdogo darasani.

Baadae Edison aliandika kwenye diary yake “Thomas A. Edison was a mentally deficient child whose mother turned him into the genius of the century.” --
Akiwa na maana kwamba "Thomas A. Edison alikuwa mtoto mwenye upungufu wa kiakili ambaye mama yake alimgeuza kuwa genius wa karne hii."

Hio tunaita ni nguvu ya maneno, maneno ya mama yalimfanya mtoto awe mgunduzi wa bulb ambayo tunaitumia leo, mkuu jaribu kukaa karibu na watoto wako, wapende, wajali, wape moyo, usiwachape hovyo na kuwaita wajinga ukifikiri unawajenga wakati unawaua ndani kwa ndani, ndio watoto wako Mungu kakupa hakuna wengine, mbeleni wanaweza kuja kufanya maajabu kama Edison 🙂
Thread imefungwa mkuu ahsante kwa ushauri huu

Mtoa mada zingatia hapa
 
Sasa kama mtoto mdogo anaukariri mwimbo wote wa dula makabila au zuchu tena anauimba bila kukosea,si Ana akili huyo 😄

Ova
 
Watoto wadogo Huwa wana kawaida ya ku-adapt mazingira yaliyowazunguka endapo familia ukiwa na ya wasomi au la.

Hivyo tabia ya kusoma kwa mtoto Huwa inajengwa nyumbani na inasimamiwa na watu wa nyumbani hasa wazazi.

Hili ni jambo muhimu Sana wadau tujue kama watoto wetu hatuwasimamii sisi wazazi na kuhakikisha tunakaa nao pamoja karibu wanaposoma, basi sio ajabu kuona mtoto anakosa muendelezo mzuri darasani.

Suala la kusoma tuisheni ni swala linalomhusu mwanafunzi binafsi na kama mtoto mwenyewe hapendi elimu mpaka asukumwe basi tutambue elimu yake utakua kwa AJILI ya wazazi wake na sio asome aelewe binafsi.

Nidhamu ya woga itamuungoza na hataweza kupata kitu darasani awapo mwenyewe ila atasoma kwa sababu mzazi anamlazimisha asome.
 
Miongoni mwa mambo ya maana katika hii dunia mbaya ya siku za mwisho ni Elimu. Kila mzazi anatamani kama mimi ninavyotamani wanangu wawe vichwa darasani katika masomo yao, lakini wengi, kama mimi pia tunaishia kutamani tu hasa tunapoona watoto wa wengine wakifanya maajabu katika masomo yao.

Kwangu mimi wanangu hawaendi nitakavyo, mimi pamoja na wanangu kusoma shule za binafsi, English mid. Anayejua siri ya watoto kufanya vizuri anipe wandugu.

Nimejitahodi kuwakazania kusoma na kuwasaidia mimi mwenyewe. Tuition za kufa mtu, vitabu nanunua. Wakifeli na fimbo wanapata, wakifaulu zawadi wanapata. Lakini sioni kufanya vizuri kule mimi ninakotaka, inaniuma sana.

NIFANYEJE
Maombi kwa Mungu kwa kuomba rehema kwa kuwa ni jambo la kimungu na sio la kimwili zaidi ni kiroho Mithali 3:5-6 Mtumaini Mungu wako. Wapeleke kwa wachungaji waombee ukishindwa na mkono wa Mungu utawafungua.
 
Miongoni mwa mambo ya maana katika hii dunia mbaya ya siku za mwisho ni Elimu. Kila mzazi anatamani kama mimi ninavyotamani wanangu wawe vichwa darasani katika masomo yao, lakini wengi, kama mimi pia tunaishia kutamani tu hasa tunapoona watoto wa wengine wakifanya maajabu katika masomo yao.

Kwangu mimi wanangu hawaendi nitakavyo, mimi pamoja na wanangu kusoma shule za binafsi, English mid. Anayejua siri ya watoto kufanya vizuri anipe wandugu.

Nimejitahodi kuwakazania kusoma na kuwasaidia mimi mwenyewe. Tuition za kufa mtu, vitabu nanunua. Wakifeli na fimbo wanapata, wakifaulu zawadi wanapata. Lakini sioni kufanya vizuri kule mimi ninakotaka, inaniuma sana.

NIFANYEJE
Cha kukushauri hapo Ni kujaribu kuchunguza vipaji vya watoto wako,Kuna wengine Mungu amewapa vipawa vya maisha nje ya darasa ,huenda watoto wako hawana vipaji vya darasani Ila jaribu kuboresha vipaji vyao.Kuna mafanikio makubwa kwa watoto nje ya elimu ya darasani, wakati mwingine Ni bora tuwasikilize watoto kuliko kulazimisha.
 
Mkuu umeeleza vema ila kazi za nyumbani hazina msaada wa kutosha kumsaidia mtoto kufanya vizuri darasani. Genetics inahusika kwa 100%. Uwezekano wa vilaza kuzaa mtoto kipanga ni mdogo. Utakuta familia ya watoto 6 ni mmoja tu kipanga.
Mkuu nazungumza kitu ninachofahamu na nina ushahidi nacho.

Suala la genetics halina uhalisia wowote.

hata mimi binafsi nimeshapractice hivyo vitu.

Kuna mdogo wagu yeye alikuwa ni kipanga sana class ila wazazi wetu wameishia darasa la saba,ila kwa namna ambavyo niliweza kushift mind yake mpaka akafikia kupata division 1 shule ya kata huko vijijini kwetu it's amazing.

So mkuu kama unaamini kwenye genetics achana na hizo myth ambazo hazina mshiko hata kidogo.

Ishu nyingine nakupa.

Kuna jamaa tumsoma nae yeye alikuwa ni kipanga darasani il wazee wake wote waliishia darasa la saba na wazee hao hawaa histori yoyote ya kufanya vizuri.

Ingelikuwa kufaulu ni genetics kutoka kwa wazazi basi leo tusingeona watoto wa wazee wasiosoma wakifanya vizuri.

Hiyo inaonesha namna ambavyo kufaulu ama kuwa na akili kwa mtoto sio ishu ya genetics.

Ila hii siri watu wengi hawaijui hivyo ni vigumu kukubali kwamba ufaulu wa mtoto darasani na uelewa wake unatokana na malezi na wau waaomzunguka kwa99%.

Msome na jamaa hapo juu Andrew Tate kaelezea vizuri sana kuhusu haya mambo.
 
Kwahiyo hiyo mifano yako miwili ndo imekupa majibu ya utafiti wako? Genetics sio myth. Ni kitu halisi ambacho kipo. Mtoto wa mwanariadha kuzaa mtoto mwenye kipaji cha riadha sio ajabu. Ingekuwa genetics haina nchi nyingi ikiwemo Marekani zingetengeneza vipaji vingi vya mpira kwa kusaidiea na mazingira tu kama unavyosema wewe.
 
wahiyo hiyo mifano yako miwili ndo imekupa majibu ya utafiti wako?
KUmbe ulitaka nikupe mifano milioni moja ili nijaze likitabu alafu usisome mkuu ? 😀.

Nimekupa sample ya utafiti tu huku nikiwa na mifano mingi kando inayoendana na sample hiyo.
Genetics sio myth.
Sijasema genetics ni myth bali myth ni kusema kwamba ufaulu wa mtoto darasani eti ni genetics 100%,hizo ni ishu sizo kabisa hazina ukweli wowote.

Wale wa kwaza kuanza shule wakafaulu unadhani waitegemea genetics za wazazi ambao hawakusoma ama ? Jiulize maswali kama hayo.
Mtoto wa mwanariadha kuzaa mtoto mwenye kipaji cha riadha sio ajabu
Riadha so kipaji bali ni mazoezi,ndio maana leo hussein bolt tizi analokula sio la mchezo,it's all about practice and not talent.

Ndio maana hakuna mwanariadha mwenye kipaji cha riadha alafu akawa hafanyi mazoezi ya kukimbia,
Ingekuwa genetics haina nchi nyingi ikiwemo Marekani zingetengeneza vipaji vingi vya mpira
kuna wachezaji wengi ambao wazee wao hawana historia ya kuwa wachezaji,lakini kupitia mazngira na makuzi wanajikuta wakiwa wachezaji wazuri wanaotajwa kwa vipaji.

Hiyo ni dhahiri kwamba ishu nzima ins rely kwenye makuzi na mzingira yanayomzunguka na sio genetics.

Alafu MAREKANI sio kipimo cha uhalisia wa mambo mzee,kwani hao jamaa si ndio katika wale wanaoweza kufanya surgery na kujibadilisha maumbile.

So marekani hautakiwi kuiweka kama reference kwa sababu nao wana mambo yao ya kipuuzi kibao tu.

So huwenda ukaifanya marekani kuwa reference kweye jambo lako alafu kumbe hilo jambo ni katika yaleee mambo yao ya kipuuzi
 
KUmbe ulitaka nikupe mifano milioni moja ili nijaze likitabu alafu usisome mkuu ? 😀.

Nimekupa sample ya utafiti tu huku nikiwa na mifano mingi kando inayoendana na sample hiyo.

Sijasema genetics ni myth bali myth ni kusema kwamba ufaulu wa mtoto darasani eti ni genetics 100%,hizo ni ishu sizo kabisa hazina ukweli wowote.

Wale wa kwaza kuanza shule wakafaulu unadhani waitegemea genetics za wazazi ambao hawakusoma ama ? Jiulize maswali kama hayo.

Riadha so kipaji bali ni mazoezi,ndio maana leo hussein bolt tizi analokula sio la mchezo,it's all about practice and not talent.

Ndio maana hakuna mwanariadha mwenye kipaji cha riadha alafu akawa hafanyi mazoezi ya kukimbia,

kuna wachezaji wengi ambao wazee wao hawana historia ya kuwa wachezaji,lakini kupitia mazngira na makuzi wanajikuta wakiwa wachezaji wazuri wanaotajwa kwa vipaji.

Hiyo ni dhahiri kwamba ishu nzima ins rely kwenye makuzi na mzingira yanayomzunguka na sio genetics.

Alafu MAREKANI sio kipimo cha uhalisia wa mambo mzee,kwani hao jamaa si ndio katika wale wanaoweza kufanya surgery na kujibadilisha maumbile.

So marekani hautakiwi kuiweka kama reference kwa sababu nao wana mambo yao ya kipuuzi kibao tu.

So huwenda ukaifanya marekani kuwa reference kweye jambo lako alafu kumbe hilo jambo ni katika yaleee mambo yao ya kipuuzi
Hussein Bolt ❌ Usain Bolt ✅
Kumbe nabishana na mtu mpumbavu. Kama riadha sio kipaji ni nini? Wewe bora ungekaa tu kimya. Ukizidi kuandika utazidi kujivua nguo.
 
Back
Top Bottom