Niliamua kumuacha huyu 'wife material' sababu ya umasikini wa kwao

"Nimekuja kujifunza na kugundua kuwa familia maskini na duni huendelea kuwa hivyo sababu ya uchawi na ushirikina."

[emoji115][emoji115]

Mimi pia nimeng'amua hili hivi karibuni. Na hawapo tayari kuuachilia. Ni jambo la kumshukuru Mungu sana kama hutokei ukoo wa kichawi/kishirikina.

Kifupi tu ni kuwa masikini wengi wameridhika na hali zao hata hawawazi, ila tu hawaridhiki na kupiga hatua chanya kwa familia zingine. Hapo ndipo penye tatizo.
 
Chief upo sahihi kabisa kwa dini yet ya kiislam ishaeleza tuoe familia yenye dini au yenye uwezo yan pesa hata mtume wetu Muhammad kipenzi alimuoa bi aisha alikuwa tajiri sana siyo maskini kwaiyo upo sahihi sana tuoe familia zenye uwezo wa pesa
 
Washamba ndio wanahisi mapenzi ni kuwa na pesa. Wanaishia kuumia vibaya sababu wanakosa real ass partners.
 
We mwenyewe sikujui ila nina uhakika kuna wanawake uliwatamani ukawakisa sababu walikuona hauna uwezo,sijui lakini nahisi tu
That was the problem, mwanamke asipokukubali jinsi ulivyo wewe ndio una faida zaidi kwa sababu yeye ameamua kuchagua fake path.Atapata ambaye ana hela ila hampendi anamuigizia.
 
Mungu hampangii mtu kuwa tajiri au masikini
 
Hiyo Ni tabia tu ya kupenda kitonga na uoga wa majukumu ambao Ni janga la hiki kizazi.....yaani mwanaume kabisa unajinadi lazima nioe mtoto wa kishua ili iweje wajomba wakuendeshee familia kwa Mali za baba mkwe??Kitawakuta kitu Shauri zenu
Kwamba kuoa ni lazima uoe familia nzima?
 
Nyie wenyewe hamuwezi kuolewa na mwanaume mwenye background ya umaskini kwao

Mnatumia neno "Kitonga " kama defence mechanism kwenu

Ku oa mwanamke mwenye background nzuri haimaanishi usaidiwe majukumu
Shida ya wanawake wa hivyo ukimleta mjini akapata exposure anakuona wewe kidampa. Wanakuwaga na ulimbukeni wa kishamba sana na kama ni pisi basi lazma vijana wa mjini watapiga tu.
 

Una uhakika ni mtu anayeamini uwepo mungu huyu?
Maana sidhani kama angefanya au kuandika hayo aliyoyafanya
 
Shida ya wanawake wa hivyo ukimleta mjini akapata exposure anakuona wewe kidampa. Wanakuwaga na ulimbukeni wa kishamba sana na kama ni pisi basi lazma vijana wa mjini watapiga tu.
Akishakua hivyo unapiga chini una download mwingine..kuishi kwa hofu ya kuwaza mabaya nao ni umaskini wa akili.

Mimi familia pekee ambayo siwezi kuoa bwana ni yenye mambo ya kichawi. Mamaye hizo naogopa kama moto wa jehanamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…