Nilibisha sasa nimeamini, FIFA wanataka Messi ashinde hili Kombe la Dunia

Nilibisha sasa nimeamini, FIFA wanataka Messi ashinde hili Kombe la Dunia

Imesemwa na wachezaji wa Ureno na wachambuzi wengi kuhusu Argentina kupendelewa, nikabisha.

Yaani hadi sasa Messi ana magoli 5, na 4 kati yake ni penalti!

Argentina wamepewa penati nyingine yenye utata tena leo, tena baada ya Croatia kunyimwa kona ya wazi.

Hii sio mara ya kwanza Agentina kupewa penalti ya utata, Vs Poland walipewa penalti nyingine tena yenye utata.
Hao Ureno wako waliosema hayo walifunga hata goli 1 likakataliwa ?
Penalty waliyopewa Ureno dhidi ya Ghana ilikuaje ?
Kubalini tu Argentina walibadirika baada ya kufungwa na Saudi Arabia
 
Miss hata tuzo zake zote 2 za Balloon D'O ni za utata.

2010 alilalamikiwa kuchukua tuzo ya aliyekuwa anastahili Iniester.

2020 pia alilalamikiwa sababu alichukua tuzo ya Lewandosky hata Messi naye alikiri hivyo [emoji23]

Miss anaandaliwa kupewa tuzo ya mchongo kwa kupewa penalty zaidi ya 5 zote, anayekataa kuwa life is not fair ajiite Taahira [emoji28]
Sasa kama kwenye timu yake ya Taifa mpiga penalty ni yeye amechaguliwa ulitaka asipige au??
 
Changamoto kubwa ya kizazi Cheni ni ufuasi. Huu ufuasi wenu upo kila mahali. Kwenye Dini, Siasa, Muziki na hata mpira. Watu wanaabudu wanadamu wenzao na huwaambii kitu kuhusu hao wawapendao.

Kimsingi kwa jicho la tatu, ilishaonekana. Ili mchezaji awe GOAT ni lazima ashinde kombe la Dunia. Kwa sasa mchezaji anayeheshimika zaidi duniani ni Pele na ndiye mchezaji mkubwa zaidi ya wachezaji wote Duniani toka kuimbwa kwa ulimwengu. Pamoja nankuwa ametokea Brazil ila ni ngozi nyeusi. Ilikuwa ni lazima kwa ngozi nyeupe kuandaa wazi wao watakaokuwa na kuimbwa kuwa ni wachezaji bora zaidi ya Pele. Sikatai Messi ni mchezaji mzuri ila ameandaliwa kwa muda mrefu aonekane kuwa ni bora zaidi ya Pele. Kuna "Bal on dor" zaidi ya mbili ambazo zililazimishwa apewe japo hakudeserve.

Hili kombe la dunia lilishaonekana muda atapewa kwani ndio kombe lake la mwisho kucheza na anaelekea kustaafu ili aonekane ni zaidi ya Pele. Sikuangalia mechi nyingi za Argentina ila ile ya jana niliangalia Kipindi cha kwanza. Haikuwa Penalti ile kwani kipa alishaucheza mpira na mchezaji wa Argentina hakuwa na uwezo wa kuucheza wala kuu kutakuukuta tena ule mpira hivyo kuwa na uhakika wa kufunga goli au kuwa hatari dhidi ya wapinzani wake hata kama aliguswa na golikipa.

Wampe tu kombe lake.
 
Kamsikilize vizuri Dr Licky kwenye review za uchambuzi wa mechi ya leo.

Pia vipi penalty ya Netherland, ilikuwa ndani ya eneo la kipa?

Vipi penalty dhidi ya Poland?

Argentina wako hapo sababu ya mbeleko tu.
Mkuu, kwann umsikilize Dr. Licky?
Mchambuzi nae ni binadamu kama wew tu na wte mnaangalia mpira.
 
Ndugu yangu Kinengunengu you have wrote nothing but conspiracy, and deep inside you nawewe pia una utimu, udini na itikadi nyingine kama ulivyowahukumia vijana kuwa wanavyo

Nini kilikusababisha uache kufuatilia WC?? Eti sababu Argentina anabebwa???mbona sababu dhaifu/ mfu kabisa???

Ngoja nikutajie team kubwa pengine bila shaka zingemfunga Argentina zilizotoka afu uniambie kuwa zilifanyiwa figisu ili Argentina asikutane nazo

Brazil: alifanyiwa figisu????
Spain: alihujumiwa???
German: alifanyiwa ukiritimba???
Belgium: alifanyiwa njama???
Portugal: alifanyiwa njama???

Hao Argentina wenyewe ni kama tu kisimati tu mungu kaamua hivyo

Alipigwa na saudia akawa anahitaji point sita kwa Mexico na Poland ili afuzu na zile kw a taarifa yako ndio zilikuwa game muhimu kwa Argentina kuliko hata hiyo ya Croatia... Je katika hizo game mbili za Mexico na Poland ambazo zote alishinda goal mbili bila kuna goal penalty (kwasababu nyie tafsir yenu penalty ni kubebwa) tulipata penalty dhidi ya Poland ila tulikosa

Mpira ni mchezo wa wazi wenye waamuz watano katika uwanja plus VAR hivi Argentina angefungwa goal tatu au mbili ya halal wangeyafuta au kuyakataa na dunia inaona???

Mbona game dhidi ya Netherlands ziliongezwa ten minutes hadi tukachomolewa goal ingekuwa yaandaliwa kuwa bingwa na alikuwa keshazidiwa zisingeongezwa hata dakika nane achilia mbali kumi

Mbona hatujaona akifungwa na goal kukataliwa???

Acheni propaganda za ajabu ambazo hazipo kwa sababu timu zenu zimetoka acheni chuki binafsi

Messi mwenyewe ana goal tatu za penalty katika mechi sita na ni za halal lakini zinavyoongelewa utafikiri magoal yote 11 ya Argentina ni penalty

Msiishi kwenye mi conspiracies eti kila kitu mnaamini kuna something behind huo pia ni ugonjwa....ni kweli Wenda watu wengi wanatamani messi ashinde WC lakini sio kuja kusema anaandaliwa, anaandaliwa vipi sasa na akifungwa na team pinzani goal zitafutwa??? Mbona alivyosawazishiwa na Netherlands goal hazikukataliwa??? Na magiant wote waliotoka ambao hawakukutana na Argentina ila walikuwa wanauwezo wa kumfunga na kumtoa pia ni planned???

Hamna hoja mna rukaruka tu

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Haikuwa penati ile, mpira ulikuwa ushaguswa na mchezaji.
Kwa sababu mpira uliguswa na mchezaji basi ndo sababu refa alitoa penalti.
Angalia goal la pili kama golie asingemgusa Alvarez basi angeukuta ule mpira na kufunga

Bingwa ni Morroco
 
Kamsikilize vizuri Dr Licky kwenye review za uchambuzi wa mechi ya leo.

Pia vipi penalty ya Netherland, ilikuwa ndani ya eneo la kipa?

Vipi penalty dhidi ya Poland?

Argentina wako hapo sababu ya mbeleko tu.
Ukweli lazima usemwe japo sio lazima ukubaliwe

Penati 4 hata mimi sikukosi aisee
 
Na huyo messi katika game sita kawa Man of the match katika match nne, na kila match ya knock out stage pia kawa man of the match...... Hiyo pia anabebwa??? Jumapili akipewa player of the tournament mtasema mchongo.....ila Tanzania bwana huwa ina wachambuzi wa mpira wapo biased sana tena when it comes pale wana mapenzi binafsi au kutokuwa na mapenzi na kitu, aya hizo MOTM pia mseme mapema ni ipi kapewa ili tuzipunguze mapema

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Nimegudua watu wengi chuki dhidi ya mess imewafanya waone wanabebwa...mechi mmeangalia kweli au mnasoma makasiriko ya wazungu
 
Fj4b19VXoAYIvfG.jpeg.jpg
 
Back
Top Bottom