Nilichojifunza kuhusu wanaume
Natumaini mko poa,

Nilipoteza baba nikiwa najitambua kiasi nikabaki na mama pekee. Mama alikuwa mchakarikaji sana lakini kuna vitu vilibadilika sana mambo hayakuwa kama yalivyo awali.

Maisha yalikuwa tofuti sana na kipindi baba yangu yuko hai nikaona ni kiasi gani mzee aliteseka kuhakikisha tunaishi vizuri na tunakuwa salama sisi na mama yetu nimejisikia kuwasemea leo.

Kuna wakati wanaume wanapitia mambo mengi magumu kwaajili ya familia zao ama watu wanaowapenda hasa katika utafutaji wa riziki. Kuna walio na kazi za halali, kuna wengine wahatarisha hata maisha yao Ili kuhakikisha mambo yanakuwa sawa lakini kitu kizuri ni kwamba sio wasimualiaji wazuri wa mahangaiko na mateso yao wakati wanafanya hayo.

Kuna ambao wanatamani asubuhi isifike kwani kwao ni mateso matupu. Hadi jua linazama ni mwendo wa mahangaiko na ukute kuna wakati hawapati kabisa lakini ndo hivyo waliumbiwa mateso, ni mwendo wa kichwa kupata moto tu.

Wanawake wengi tumekuwa ni wazuri kwa upokeaji lakini ni wachache wa kushukuru. Tuwahurumie na tuwaombee japo wana mabaya yao na madhaifu yao walokuwanayo lakini watabaki kuwa ni muhimu kwa ustawi wafamilia zetu.

Kwa mliopo kwenye ndoa mjitahidi kuwatia moyo na kuwahurumia pamoja na udhaifu wa waume zenu, lakini inawezekana bila huyo mambo yasingekuwa hivyo unavyoyaona; pia mkumbuke pia hatma za watoto wenu.

Na sisi wa jumuiya😀 pia tuwaombee na tuwashukuru kwani bila wao tusingeonekana huku mtaani.

Niliowakwaza mtanisamehe, ni hayo tu.
Jamani wanawake kama hawa utaachaje kumtumia na ya kutolea sasa..🥰🤑
 
Hakika hii ni siku njema sana kuwahi kutokea ndani ya january 2023, ujumbe mzuri uliosheheni upendo ambao ni wanawake wachache hutambua na kuyaishi hayo. Kuielewa hali ya mumeo ni jambo la muhimu lakini kuishi nae kuvumilia na kumuombea kwa hali hiyo ni Upendo wa kweli. Barikiwa sana sophy27 😘, nipo natafuta location nzuri ya kujenga sanamu yako. Upewe ulinzi tafadhali
Ni kweli na laiti km wote tungeishi Kwa upendo kiasi hiko tungekuwa tunaishi maishamazuri sana
 
Mwaka jana,niliugua sana,ofisi ikanipa mapumziko ya mwezi mzima nijiuguze.Siku naaga ofisini ilikuja barua nahitajika kikazi mkoa fulani..kwa muda wa mwezi mmoja..na kuna pesa nitalipwa..nilihitajika alone.
Nilipata wakati mgumu sana kuamua,hasa nilipoifikiria family yng&afya yangu...
Mwisho niliamua niende hivyo hivyo tu,b'se of family.
It wasn't simple,Mungu alinisaidia.
Nilirudi&pesa iliyokidhi mahitaji ya family members&nyingine
tukatoa sadaka.
 
Umetisha dada japo kwenye mitandao hasa page za mahusiano wanaume ndio tuna makosa Kila siku ila ukweli wanaume hatuongeagi sana Kwa mwanaume anaejitambua anatumia nguvu kubwa Sana kuhakikisha familia yake Iko sawa.
Poleni kwakweli
Lakini tuna thamini sana uwepo wenu

Tusameheane bure pale tunapowatendea ndivo sivo
Maana sanyingine ni kama tunatupiwa jini kisirani kuwavuruga jamani [emoji134]
 
kuna mmoja jamaa ake alikuwa akimpa hela kanunue nguo uvae upendeze mke wangu, alivyovaa akapendeza akaanza kuleta dharau kwa jamaa, mwamba akaona sio shida tumwagane, bibie akaanza kudai tugawane vitu tumechuma wote jamaa kamwambia haina haja ya kugawana we unachoona unakitaka kibebe hata ukitaka chumba chote, bibie akabeba alivojisikia kubeba akasepa, haikuchukua miezi mitatu aisee alivisukuma vile vitu kimoja kimoja hatimae akarudi kwa msela kuomba msamaha, msela kamwambia tulikuwa
tumepambana chumba kimejaa kwa ujinga wako saa hz ndo kama naanza maisha alafu unarudi mikono mitupu, we nenda tu. Alirudi kwao mbeya yule dada baada ya maisha kumpiga sana kila anachoshika ni kama kinaparaganyika
Muda mwingine kiukweli tunazingua mno

Ni muda wa kubadilika na kutambua ni jinsi gani mnahitaji faraja zetu na sio kua chanzo cha kuwapa stress
 
Back
Top Bottom