Nilichojifunza kuhusu wanaume
Natumaini mko poa,

Nilipoteza baba nikiwa najitambua kiasi nikabaki na mama pekee. Mama alikuwa mchakarikaji sana lakini kuna vitu vilibadilika sana mambo hayakuwa kama yalivyo awali.

Maisha yalikuwa tofuti sana na kipindi baba yangu yuko hai nikaona ni kiasi gani mzee aliteseka kuhakikisha tunaishi vizuri na tunakuwa salama sisi na mama yetu nimejisikia kuwasemea leo.

Kuna wakati wanaume wanapitia mambo mengi magumu kwaajili ya familia zao ama watu wanaowapenda hasa katika utafutaji wa riziki. Kuna walio na kazi za halali, kuna wengine wahatarisha hata maisha yao Ili kuhakikisha mambo yanakuwa sawa lakini kitu kizuri ni kwamba sio wasimualiaji wazuri wa mahangaiko na mateso yao wakati wanafanya hayo.

Kuna ambao wanatamani asubuhi isifike kwani kwao ni mateso matupu. Hadi jua linazama ni mwendo wa mahangaiko na ukute kuna wakati hawapati kabisa lakini ndo hivyo waliumbiwa mateso, ni mwendo wa kichwa kupata moto tu.

Wanawake wengi tumekuwa ni wazuri kwa upokeaji lakini ni wachache wa kushukuru. Tuwahurumie na tuwaombee japo wana mabaya yao na madhaifu yao walokuwanayo lakini watabaki kuwa ni muhimu kwa ustawi wafamilia zetu.

Kwa mliopo kwenye ndoa mjitahidi kuwatia moyo na kuwahurumia pamoja na udhaifu wa waume zenu, lakini inawezekana bila huyo mambo yasingekuwa hivyo unavyoyaona; pia mkumbuke pia hatma za watoto wenu.

Na sisi wa jumuiya😀 pia tuwaombee na tuwashukuru kwani bila wao tusingeonekana huku mtaani.

Niliowakwaza mtanisamehe, ni hayo tu.
Kuna siku unaamka mfukoni una elfu tatu!!!!Bado hujaacha kodi ya meza,bado hujaacha emergency money home na bado hujui huko uendako itakuaje!!!Lakini ukimuangalia mkeo unaempenda na watoto wako na watu wanaokutegemea unajikuta unapata nguvu ya kwenda kupambamia kombe!!!!Wanasemaga hakuna kama mama ila nilipokua baba nikaelewa uzito wa kubeba majukumu kama mwanaume!!!Who feels it knows it
 
[emoji123]
 
Kwanza pole saana kwa kupoteza mzazi wa kiume.

Pili tunaomba sanamu la posta litolewe uwekwe wewe. 😂

Tatu.
Peponi usiwe mbali na mimi.
 
Asante
Nimeshaomba. Wawek plot mbili kwaajili yngu na Yako😂
Kwanza pole saana kwa kupoteza mzazi wa kiume.

Pili tunaomba sanamu la posta litolewe uwekwe wewe. 😂

Tatu.
Peponi usiwe mbali na mimi.
 
Mungu awabariki wanaume wote watafutaji[emoji120]
Unakuta mtu anachakarika,hapumziki,ili tu familia iwe pazuri.
MUNGU akubariki na abariki wanawake wote wenye subira , imani , heshima na uvumilivu kwa wanaume . Wanaojua changamoto na magum wanayopitia wanaume ili familia ziishi vizuri. Mna nafasi yenu ya pekee maana kwa dunia ya sasa mpo wachache sana[emoji173]
 
Back
Top Bottom