Nilichokikuta ukweni imebidi nimsamehe mume wangu

Nilichokikuta ukweni imebidi nimsamehe mume wangu

Siku zote nimekua nikilalamika humu mme/mwenzangu kutohudumia nyumbani na kuhamishia nguvu kwao ila nilichokiona mpaka nimemuonea huruma

Iko hivi mi na mwenzangu tulikua tunaishi pamoja tangu mwaka Jana mwaka huu wazazi wakaamua wakamilishe taratibu zote ikabaki ndoa tu sasa katika maisha na mwenzangu wajibu wake ndani umekua mdogo maendeleo hakuna hafanyi

Nimeenda kwao likizo nimechoka mwili na roho nimepoteza ndoto za kua na maisha mazuri kabisa jamaa ukoo mzima iwe shangazi, mjomba,Dada zake hata walioolewa yeye ndio anawahudumia

Nimemuonea huruma maana sio ombi nilazima familia ile dada zake wavae aanunulie nguo kila siku ikifika mwisho wa mwezi hela zote zinaenda kwao ikifika tarehe 10 mshahara umeisha nilikua nachukia namuona hana akili za maendeleo lakini kwa hali nilivyoiona hata yeye hana jinsi

Jamani nishauri nifanyeje tue na maendeleo na sisi? sababu kipato changu ni lak 3 binafsi mwenzangu yeye anapokea mil 1.4_5 lakini majukumu ni mengi kwao hawezi kufanya

Nifanyeje jamani?
AHAKIKISHE WAZAZI WAKE WANAPATA CHAKULA NA MAVAZI. NA PIA WALIOKUWA WANAMPA MSAADA WAKATI WA MAsomo. Wazazi nguvu za kufanya kazi zinaendelea kupungua
 
Nilichogundua jamaa hana jinsi hata ya kujitetea kila kitu anakubali,,, kuna dada zake wametoka kwa wame zao wamekuja kusalimia wakamwambia hatuna nauli ya kurudi wala hatuna cm za mawasiliano jamaa katoa hela kawapa......na nguo kawaliwanunulia. , jamaa hana cha kujitetea
Tatizo kubwa zaidi la huyu mumeo mtarajiwa sio ndugu ni kujitambua na yeye mwenyewe kujua anachokitaka kwenye maisha
 
pole sana mkuu. mshawishi akopee kwenye hiyo pesa yake at least iwe inakatwa lak6, hope mtachukua pesa nyng tu fanya maendelea thn ww simamia family kwa hicho kidogo chako, Then yeye inayobaki atajua namna ya kuibalance kwao wapate, abakize yake ya kutumia kazini na pia naamini hawezi kukubali yy miaka nenda rudi haachi japo buku nyumbani.
 
Unaeza kuta dada zake waliacha shule au kutopelekwa shule kabisa ili baba yake aweze kumsomesha yeye. Pengine dada zake ndio waliamua kuacha kwenda shule wakaenda shamba ili wamlipie ada kaka yao.

Usilolijua liache lipite

Mmh...basi kama ni mtihani, huu hatakaa afaulu kwa mshahara.....
 
Yeye anaona sawa tu tens Siku hizi baada ya kuona namshaur sana kuhusu maendeleo kanificha kipato chake so anaona Mimi ni adui
Basi hapa ndiyo tatizo lilipo. Tatizo sio ndugu zake. Nafikiri watu wajikite kwenye kukushauri namna ya kumuwezesha huyu bwana kujitambua na kujua umuhimu wa maendeleo yenu na watoto wenu watarajiwa.

Kwa bahati sana sina ushauri wa namna ya kukuwezesha kufanikisha hili, ila nina imani kuna watu humu wanna hekima. Ngoja niwaachie wao wakupe busara zao.

Ukikata huu mzizi wa tatizo utakuwa umetatua tatizo kwa asilimia 90, hizo 10 ndo hao ndugu ila zinatatulika kirahisi sana Kama mzizi utakatwa na kuchimbuliwa.
 
Pole dada, nmekumbuka siku kadhaa zilizopita ulileta uzi humu.jitahidi kumshawishi apange budget Vizuri., inasikitisha Kama hadi dada zake walioolewa anawahudumia yeye,,Sasa wao kazi yao ni kula tu hela zake??

Hata Kama anatoa huduma basi iwe Mara moja moja,, too much is harmful.
Nyinyi pia mnapaswa kuenjoy matunda ya kazi yenu
 
Siku zote nimekua nikilalamika humu mme/mwenzangu kutohudumia nyumbani na kuhamishia nguvu kwao ila nilichokiona mpaka nimemuonea huruma

Iko hivi mi na mwenzangu tulikua tunaishi pamoja tangu mwaka Jana mwaka huu wazazi wakaamua wakamilishe taratibu zote ikabaki ndoa tu sasa katika maisha na mwenzangu wajibu wake ndani umekua mdogo maendeleo hakuna hafanyi

Nimeenda kwao likizo nimechoka mwili na roho nimepoteza ndoto za kua na maisha mazuri kabisa jamaa ukoo mzima iwe shangazi, mjomba,Dada zake hata walioolewa yeye ndio anawahudumia

Nimemuonea huruma maana sio ombi nilazima familia ile dada zake wavae aanunulie nguo kila siku ikifika mwisho wa mwezi hela zote zinaenda kwao ikifika tarehe 10 mshahara umeisha nilikua nachukia namuona hana akili za maendeleo lakini kwa hali nilivyoiona hata yeye hana jinsi

Jamani nishauri nifanyeje tue na maendeleo na sisi? sababu kipato changu ni lak 3 binafsi mwenzangu yeye anapokea mil 1.4_5 lakini majukumu ni mengi kwao hawezi kufanya chochote

Nifanyeje jamani?
Huyo inawezekana aliweka maagano na ukoo sasa anza kwanza kuvunja hizo kamba za maagano Ndiyo salama la sivyo madhabahu ya ukoo inamwita muda wote.
 
Siku zote nimekua nikilalamika humu mme/mwenzangu kutohudumia nyumbani na kuhamishia nguvu kwao ila nilichokiona mpaka nimemuonea huruma

Iko hivi mi na mwenzangu tulikua tunaishi pamoja tangu mwaka Jana mwaka huu wazazi wakaamua wakamilishe taratibu zote ikabaki ndoa tu sasa katika maisha na mwenzangu wajibu wake ndani umekua mdogo maendeleo hakuna hafanyi

Nimeenda kwao likizo nimechoka mwili na roho nimepoteza ndoto za kua na maisha mazuri kabisa jamaa ukoo mzima iwe shangazi, mjomba,Dada zake hata walioolewa yeye ndio anawahudumia

Nimemuonea huruma maana sio ombi nilazima familia ile dada zake wavae aanunulie nguo kila siku ikifika mwisho wa mwezi hela zote zinaenda kwao ikifika tarehe 10 mshahara umeisha nilikua nachukia namuona hana akili za maendeleo lakini kwa hali nilivyoiona hata yeye hana jinsi

Jamani nishauri nifanyeje tue na maendeleo na sisi? sababu kipato changu ni lak 3 binafsi mwenzangu yeye anapokea mil 1.4_5 lakini majukumu ni mengi kwao hawezi kufanya chochote

Nifanyeje jamani?
Inakuhusu hiyo.View attachment VID-20181006-WA0016.mp4
 
Kupanga ni kuchagua hata sisi hatujatoka kwny familia nzuri ila unafanya kitu kutokana na uwezo wako...mm huwa natoa msaada kwa watt ambao wazazi wao wamefariki haswa linapokuja suala la ada huwa kama ndugu tunachangia kwa anayeweza.

Issue ya kumnunulia shangazi mpk chupi sitikuja kufanya mpk nakufa kila mtu apambane na maisha yake tu
Mkuu tunafanana
 
Dhaaa........huo nao ni upofu, yaani mtu umesota kusoma umepata kazi kisha unaanza kununulia nguo dada zako, hii ndio akili gani sasa. Jambo analopaswa kufanya ni moja tu. Aachanr na familia na ashughulike kwa kiasi tu na baba na mama yake pekee kwa kiwasaidia makazi bora chakula wapambane wenyewe. Hao ndugu wapambane na hali zao tu. Hiyo lazima kuwasaidia imewekwa na nani. Otherwise mtayumba sana na huyo mwanaume asiye na msimamo
Labda familia iliuza shamba ili jamaa asome [emoji23] [emoji23]
 
Sijui kwanini watu wa ajabu wanapata wake wanajielewa.Yaani sielewi mtu unashindwaje kumsupport mke wako kwenye jambo lenye faida kwa wote.
 
Kuzaliwa familia maskini haina uchaguzi Ila kuolewa kwenye umaskini ni uamuzi wako.sidhani kama tuna cha kukushauri hapo.Mimi ni maskini ila siolewi Na maskini labda niwe tajiri kwanza ndo niolewe Na maskini.
 
Pole kwa changamoto uliyonayo, ndoa zina changamoto tofauti ni aina tu.

Mtazamo wa mmeo juu ya hiyo hali na future ya familia yenu ukoje? Naamini mmeshaliongelea hili kwa kina tu, maana hofu yangu unaweza ukaanza kujiwekeza lkn pindi utakapoanza pata faida akataka hata hizo aanze kupeleka huko.

Lakini kama na yeye anakubali hilo ni tatizo na kikwazo kwa maendeleo ya familia yenu basi akipata ushauri anaweza kubadilika na kuona abalance vp matumizi.
 
Majukumu sio dhambi mwambie afanye yale yanayo wezekana apo mtaweza kusave kiasi kitakacho wawezesha kupiga hatua kimaendeleo
 
Back
Top Bottom