Nilichokutana nacho leo kwenye Mataa ya Morocco kimenitafakarisha sana Kuhusu Askari Polisi wa Tanzania

Nilichokutana nacho leo kwenye Mataa ya Morocco kimenitafakarisha sana Kuhusu Askari Polisi wa Tanzania

Leo, tarehe 30/10/2026, majira ya saa 12:00 asubuhi, nilikuwa napita maeneo ya mataa ya Morocco. Kama tunavyofahamu, kutokana na shughuli za ujenzi zinazoendelea katika eneo hilo, mara nyingi nyakati za asubuhi taa za kuongozea magari hazifanyi kazi, hali inayosababisha madereva kutumia utashi wao na wakati mwingine mwenye nguvu ndiye anayepita.

Nikiwa hapo, nilishuhudia kundi kubwa la waendesha pikipiki (Bodaboda) wakiwa wamesimama katikati ya barabara. Walikuwa wakishirikiana kumbeba dada mmoja na kumtoa barabarani, ambaye inaonekana alikuwa amepata ajali ya pikipiki. Pikipiki moja ilikuwa imelala chini, ishara kwamba kulikuwa na ajali iliyotokea.

Kilichonisikitisha zaidi ni kuona kundi la askari, wasiopungua ishirini, wakiwa upande wa pili wa barabara wakiendelea na shughuli zao, huku wananchi wakihangaika kumsaidia majeruhi katikati ya barabara na magari yakiendelea kupita, jambo lililowaweka kwenye hatari zaidi.

Kwa kweli, nilijiuliza: Je, katika mazingira kama haya, si jukumu la askari kusaidia kudhibiti magari, kulinda eneo la ajali na kuwezesha majeruhi kupata msaada wa haraka?

Huu si wakati wa kulaumiana, bali ni wakati wa kukumbushana wajibu na utu. Maisha ya binadamu yana thamani kubwa.

It's so Bad!!!
Hizo MALI ZA CCM zilijua kabisa kuwa huyo dada na waendesha pikipiki siyo wana CCM.
 
Back
Top Bottom