Nilifadhaika sana kupata watoto wa kike tu

Hongera
 
Rais was marekani Obama Ana watoto wawili tu Tena wakike na haangaiki wala nn Africa tu ndio Jambo hili liko
 
Kupata watoto jinsia moja hupelekea ndoa kuwa na idadi kubwa ya watoto. Mfano hapa ninapoishi familia moja ilifikisha watoto kumi na moja wa kiume tu. Katika kutafuta Mtoto wa kike yule mama alibeba mimba mara ya 12, alipojifungua alipata mapacha wawili, wote wa kike.
Bora kuchanganya jinsia zote. Maana kama ni wakike wote wakikuwa na kuolewa basi kwako kunakuwa hakuna wakurithi. Na wakiwa wakiume kwa mfano Mama umekuwa Mzee/ ukaumwa Mtoto wa kiume hawezi kumtunza Mama kama anavyotunzwa na Mtoto wa kike.(pia kinyume chake kwa Baba).

Wale wanaosema watoto ni watoto hawajawahi ona jinsi mwisho wa uzee unavyokuwa mbaya hasa ukiwa na watoto wa jinsia moja tu.
 
Hongera sana mkuu.
Back to me ... Asante kwa kunipa njia nzuri ya kupata jinsia ya mtoto nimtakaye maana hapa mimi natungua ya kiume tu na niliahidi kimoyo moyo nitamzalisha Hadi kieleweke..
Sasa naanza maombi Rasmi
 
Hongera sana mkuu.
Back to me ... Asante kwa kunipa njia nzuri ya kupata jinsia ya mtoto nimtakaye maana hapa mimi natungua ya kiume tu na niliahidi kimoyo moyo nitamzalisha Hadi kieleweke..
Sasa naanza maombi Rasmi

Mnavyoomba watoto wa kiume tu wakikua watamuoa nani?
Angalieni mambo mnayo yaomba...dunia itajaa madume matupu muishie kuoana wenyewe kwa wenyewe halafu muanze kulialia kwa Mungu
 
Nakuhakikishia kuwa huyo mtoto wa kiume anakuja kuwa zigo na utajuta kumzaa!
Hilo wazo lako sahau, mkuu. Mimi naishi kwa kumtegemea Mungu na ahadi zake.

Ni vizuri ujue kwamba tukiisikia sauti ya BWANA, Mungu wetu, kwa bidii, na kuyafanya maagizo yake yote, Mungu ameahidi kutubariki pamoja na watoto wetu.

"Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo...baraka hizi zote zitakujilia na kukupata...Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako..." (Kum 28).

Mungu sio mwanadamu hata aseme au aahidi uongo.
 
Kwa utafiti mdogo nilioufanya..watoto wa kike huwakumbuka sana wazazi kuliko wa kiume.wenye watoto wwngi wa kike na ukifanikiwa kuwalea vizuri ukawa nao karibu..aisee utaishi zaidi ya mfalme..maana utalelewa na wanao na waume zao..hutokuwa mpweke maishani
 
Mungu aliumba mwanaume na mwanamke. Kwanini tusifurahie kuwa na watoto wa kike na wa kiume? Mimi nilipopata wa kike tu sio kwamba nilichukia, la hasha; ila nilitamani nipate na wa kiume. Na kwa kumpata wa kiume, furaha yangu ilitimilika. Yesu alisema tuombe, tutapewa, ili furaha yetu iwe timilifu.

Yn 16:24​

Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu
 
Reactions: Cyb
Watoto ni watoto , Mimi hata nikibahatika kupata wa kike wote nitashukuru sana Mungu
 
Kutoridhika tu
 
Nakuhakikishia kuwa huyo mtoto wa kiume anakuja kuwa zigo na utajuta kumzaa!
umekosea sana ndg.
sio sawa kumtabiria mtoto wa mwenzio mambo mabaya. ndio kwanza mtoto wake bado mchanga.

hata wewe hao watoto wako wa kiume uliozaa wanaweza kuja kuwa mashoga wakiwa watu wazima na hao wa kike wanaweza kuja kuwa wasagaji.

na kama bado hujabatika kuwa na watoto mpaka umri huo, basi anza sasa kujichunguza na kujitathimini maana unaweza kuwa ni mwanamke tasa/mwanaume hanithi.
 
Na unaridhika kununiana na mzazi mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…