Nilifadhaika sana kupata watoto wa kike tu

Nilifadhaika sana kupata watoto wa kike tu

Hali hii hutokea katika ndoa nyingi. Mke anazaa watoto wa jinsia moja tu mfululizo, ama wa kike au wa kiume tu. Wazazi wengi huwa wanapenda wapate watoto wa jinsia zote. Kwa sababu hiyo inapotokea wanapata watoto wa kiume tu au wa kike tu huanza kutafuta njia ya kutatua 'tatizo' hilo. Wengine huenda kwa madaktari kutafuta ushauri wa kisayansi na kufanikiwa kupata mtoto wanayemtaka; lakini wengine ushauri wa kisayansi bado hauwasaidii kupata mtoto wa kiume au wa kike.

Wazazi wanapofikia hali hiyo wengine huenda kwa waganga wa kienyeji na huko huishia kuchanganyikiwa tu kutokana na masharti magumu wanayoambiwa na mganga. Jaribu kuwaza mtu anaambiwa apeleke kwa mganga kinyesi "fresh" cha tembo ndio apate dawa!

Nakumbuka mme fulani alisababisha mgogoro katika ndoa yake baada ya kumgombeza mke wake kwanini anazaa watoto wa kike tu. Na waume wengine huamua kuwaacha wake zao au kuoa mke wa pili ili wajaribu kama watapata watoto wanaowataka kwa njia hiyo. Njia zote hizo zinaposhindikana hubaki na huzuni isiyokoma.

Mimi pia nimepitia hali hiyo. Mara ya kwanza mke wangu alipata mtoto wa kike. Mara ya pili akajifungua tena mtoto wa kike. Tulikuwa tunajitahidi angalau tupate mtoto kila baada ya miaka miwili. Mara ya tatu mke wangu akazaa tena mtoto wa kike. Hee nikaanza kufadhaika, maana nilitamani na mimi niwe na mtoto wa kiume. Sikumlaumu wala kumgombeza mke wangu kwanini anazaa watoto wa kike tu kwa sababu najua kisayansi mwanaume ndiye anayehusika zaidi kufanya mtoto wa jinsia ipi azaliwe.

Katika kutafakari nifanyeje nikakumbuka yale maneno ya Mungu yasemayo "Ombeni nanyi mtapewa" Nikakumbuka pia habari za mama mmoja katika Biblia aliyekuwa hapati kabisa watoto lakini baada ya kumwomba Mungu akapata.

Kwa sababu hiyo na mimi nikaanza kumwomba Mungu kwa juhudi kwamba mke wangu atakapojifungua mtoto wa nne, awe wa kiume. Ndugu zangu, Mungu hana upendeleo, alisikia maombi yangu na kutupatia mtoto wa kiume. Kinachotakiwa tu ni kuhakikisha mahusiano yetu na Mungu ni mazuri na kuomba kwa imani, pasipo shaka. Yote yawezekana kwake aaminiye(Mk 9:23).
Hongera
 
Rais was marekani Obama Ana watoto wawili tu Tena wakike na haangaiki wala nn Africa tu ndio Jambo hili liko
 
Kupata watoto jinsia moja hupelekea ndoa kuwa na idadi kubwa ya watoto. Mfano hapa ninapoishi familia moja ilifikisha watoto kumi na moja wa kiume tu. Katika kutafuta Mtoto wa kike yule mama alibeba mimba mara ya 12, alipojifungua alipata mapacha wawili, wote wa kike.
Bora kuchanganya jinsia zote. Maana kama ni wakike wote wakikuwa na kuolewa basi kwako kunakuwa hakuna wakurithi. Na wakiwa wakiume kwa mfano Mama umekuwa Mzee/ ukaumwa Mtoto wa kiume hawezi kumtunza Mama kama anavyotunzwa na Mtoto wa kike.(pia kinyume chake kwa Baba).

Wale wanaosema watoto ni watoto hawajawahi ona jinsi mwisho wa uzee unavyokuwa mbaya hasa ukiwa na watoto wa jinsia moja tu.
 
Hongera sana mkuu.
Back to me ... Asante kwa kunipa njia nzuri ya kupata jinsia ya mtoto nimtakaye maana hapa mimi natungua ya kiume tu na niliahidi kimoyo moyo nitamzalisha Hadi kieleweke..
Sasa naanza maombi Rasmi
 
Hongera sana mkuu.
Back to me ... Asante kwa kunipa njia nzuri ya kupata jinsia ya mtoto nimtakaye maana hapa mimi natungua ya kiume tu na niliahidi kimoyo moyo nitamzalisha Hadi kieleweke..
Sasa naanza maombi Rasmi

Mnavyoomba watoto wa kiume tu wakikua watamuoa nani?
Angalieni mambo mnayo yaomba...dunia itajaa madume matupu muishie kuoana wenyewe kwa wenyewe halafu muanze kulialia kwa Mungu
 
Nakuhakikishia kuwa huyo mtoto wa kiume anakuja kuwa zigo na utajuta kumzaa!
Hilo wazo lako sahau, mkuu. Mimi naishi kwa kumtegemea Mungu na ahadi zake.

Ni vizuri ujue kwamba tukiisikia sauti ya BWANA, Mungu wetu, kwa bidii, na kuyafanya maagizo yake yote, Mungu ameahidi kutubariki pamoja na watoto wetu.

"Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo...baraka hizi zote zitakujilia na kukupata...Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako..." (Kum 28).

Mungu sio mwanadamu hata aseme au aahidi uongo.
 
Kwa utafiti mdogo nilioufanya..watoto wa kike huwakumbuka sana wazazi kuliko wa kiume.wenye watoto wwngi wa kike na ukifanikiwa kuwalea vizuri ukawa nao karibu..aisee utaishi zaidi ya mfalme..maana utalelewa na wanao na waume zao..hutokuwa mpweke maishani
 
Yaani mimi nihangaike kwa madaktari kusaka jinsia ya mtoto? Mimi huyu huyu nizurure kwa waganga kutaka jinsia fulani ya mtoto!!??? Yaani mimi nijisikie vibaya kuzaa watoto wa jinsia fulani!!?? Mimi huyu?
Umbumbumbu na laana ya hali ya juu sana, kuna watu hawana watoto wanaposoma maoni yenu hapa wanasikitika sana

MTOTO NI MTOTO(Nimesisitiza kwa herufi kubwa)

Halafu nina bahati na watoto wa kike tu na niko normal kabisa, mwanamke anapambana na ushauri wa kitaalamu ili apatikane wa kiume mimi ndo kwaanza nafelisha makusudi tu, akisema tarehe hizi nile vizuri, nisifanye sana mazoezi, nipumzike vizuri ndo kwaanza sina habari mwendo ni uleule
Akisema sijui siku ya ngapi tukit.iana tunapata wa kiume ndo kabisaa hiyo siku navuruga ratiba

Siwezi kutumia nguvu kubwa kusaka jinsia ya mtoto never!!!!! Acheni hizo kuna watu hawana watoto wanatamani wapate hata mlemavu

Yameniuma sana baadhi ya maoni hapa, ukute wanachagia watoto wadogo
Mungu aliumba mwanaume na mwanamke. Kwanini tusifurahie kuwa na watoto wa kike na wa kiume? Mimi nilipopata wa kike tu sio kwamba nilichukia, la hasha; ila nilitamani nipate na wa kiume. Na kwa kumpata wa kiume, furaha yangu ilitimilika. Yesu alisema tuombe, tutapewa, ili furaha yetu iwe timilifu.

Yn 16:24​

Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Watoto ni watoto , Mimi hata nikibahatika kupata wa kike wote nitashukuru sana Mungu
 
Mungu aliumba mwanaume na mwanamke. Kwanini tusifurahie kuwa na watoto wa kike na wa kiume? Mimi nilipopata wa kike tu sio kwamba nilichukia, la hasha; ila nilitamani nipate na wa kiume. Na kwa kumpata wa kiume, furaha yangu ilitimilika. Yesu alisema tuombe, tutapewa, ili furaha yetu iwe timilifu.

Yn 16:24​

Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu
Kutoridhika tu
 
Nakuhakikishia kuwa huyo mtoto wa kiume anakuja kuwa zigo na utajuta kumzaa!
umekosea sana ndg.
sio sawa kumtabiria mtoto wa mwenzio mambo mabaya. ndio kwanza mtoto wake bado mchanga.

hata wewe hao watoto wako wa kiume uliozaa wanaweza kuja kuwa mashoga wakiwa watu wazima na hao wa kike wanaweza kuja kuwa wasagaji.

na kama bado hujabatika kuwa na watoto mpaka umri huo, basi anza sasa kujichunguza na kujitathimini maana unaweza kuwa ni mwanamke tasa/mwanaume hanithi.
 
Mie hajaniombaga msamaha ila mie ndo imekuwa reference hom...wanaishi kama baba yao hatakuja kufa mtu ana 80's! Full mipombe..
Kuna kipindi niliomba pikipiki ilikuepo tu hm..dingi akasema hv hujui ww umeshaolewa huna chako hapa? Nililiaa[emoji1787][emoji1787]!
Ss hv wananiletea tu kesi..oh ongea na dadako na mdg wako wameanza vutana kuhusu nyumba za dar..mie nasema baba mm nilishaolewa hayo hayanihusu..na kweli hayanihusu sipend kbs kupigana kisa mali za mzaz .ujinga sana! Bas kila mara ananiambia ongea na bro ako mwambia maisja anayoishi sio kbs ntakuja kufa namwambia mie nishaolewa sina hadhi ya kuongea naye tunaishia kununiana tu ..! MUNGU FUNDIII
Na unaridhika kununiana na mzazi mkuu?
 
Back
Top Bottom