Nilijikuta naishi maisha ambayo sikuyategemea ila sina jinsi

Hapa kuna vitu viwili: Msamaha na Ndoa.

Msamaha hauna maana kwamba nakubali, bali kutoa nafasi ya kujifunza na kuendelea. Na hii si kwa anae samehe au anae samehewa, ila wote.

Kwa maneno mengine, anae kataa kusamehe na anae kataa msamaha, wote wanafanya kosa na hivyo wanaharibu hali yao ya ndani. Kwa hiyo wana haribu uhusiano; uhusiano kwanza na Mungu na pili na jamii.

Kuhusu ndoa. Kwa uelewa wangu, ndoa ni jambo la akili, ambapo ikishafungwa haiwezi kufunguliwa kwa sababu yoyote; labda kama hakukuwapo na ndoa.

Kwa hiyo, kama hawa ndugu walikuwa kweli wana ndoa, itabaki hivyo daima kwenye akili na hilo haliwezi kubatirishwa.

Kitu ambacho tunatakiwa kujua ni kuwa, mambo yote mema au maovu, mazuri au mabaya yanayoweza kutupata kwenye ndoa, tunapaswa kuyapokea na kuyavumilia kwa unyenyekevu.
 
pole sana, kama hajakuletea mambukizi ya VVU shukuru MUNGU
 
Pole.
Kwa hiyo tukuchangie upate Vyumba viwili?
Sasa sisi tutakuwa na uhakika gani kama wewe ni KE kweli?

Au ni mtu unatafuta tu namna yakuishi?
Hukuna mahali amesema tumchangie, ndugu pole Sana na mitihani ya maisha. YATAPITA
 
Baba Yao kasema yupo tayari kulea watoto wake na kuwahudumia so Cha muhimu watu mlio Katika ndoa wake kwa waume tulize de libolo kwa mke mmoja mlee watoto wenu na sio kila siku mnawaza uzinzi tu mwisho mnawatesa watoto kisa ndoa zenu fake
 
Pole.
Kwa hiyo tukuchangie upate Vyumba viwili?
Sasa sisi tutakuwa na uhakika gani kama wewe ni KE kweli?

Au ni mtu unatafuta tu namna yakuishi?
Hukuna mahali amesema tumchangie, ndugu pole Sana na mitihani ya maisha. YATAPITA
Wanawake ni wanafiki sana na mnapenda kutafuta huruma wakati nyie ndo mnaanzaga kuvuruga nyumba hadi mwanaume anaamua kutokomea kusikojulikana
Kama wanawake wanavuruga mbona unaenda Tena Kwa mwanamke mwingine.Kwanini usikae pekeako?
 
Kama mzazi mwenzio kaonyesha nia ya kiwasaidia watoto wake kwanini unamzuia? Huoni kama unawanyima haki yao ya msingi
Kuwasaidia watoto ni mpaka akutane na mimi faragha? Mwenye nia ya kuwasaidia watoto angewasaidia tu, ndio maana nikikataa analeta maneno kama nilyosema kuwa nina jeuri, kiburi, nitakuwa na mwanaume ambaye ananipa kiburi, na kusema hatawasaidia kwa kuwa nakataa.

Nadhani hamjaelewa, lengo la msaada wake ni mpaka akumbushie na mimi maana yake apashe kiporo, nimeandika bila kufunguka nikajua mnaweza kuelewa.

Mimi na yeye tulishamaliza safari, siwezi kuruhusu hicho kitu kitokee abadani asilani eti ili watoto wapate matunzo.
 
Siwezi kuhukumu moja kwa moja ila kwa hii tabia ya kubeba vyombo waswahili mnazo sana na ni tabia ya dhiki sana
Mwanaume gani wa kubeba vyombo na vitu wanavyotumia wanao?

Mwanaume akapambane na maisha yake ila watoto wana haki na baba mda wote
Hata kama yametokea maudhi na hata mwanamke akaropoka kwa hasira na kusema tu ' kwanza watoto sio wako' kuna DNA na pia unaangalia maneno yametoka kwa sababu zipi

Nakupa pole pia pambana tu na maisha yako na yeye ni lazima ukubali yaishe ili awasaidie watoto wake kwa hali na mali

Kweli kakosea kuondoka hivyo ila ameomba akusaidie na wewe umekataa ni kosa

Watoto pia watasikia mengi na hata kujifunza mengi kutoka kwako na usirogwe ukawa na mchepuko nao wakajua maana ndio yatakuwa majibu ya familia zote na wao watakuchukia sana

Uamuzi ni wako na wewe unajua vizuri kesi yenu
 
Pole sana dada upo mkoa gani? Naomba location yako hata pm kama hapa itakuwa ngumu. Kesi kama yako nimewahi ishuhudia kwa ndugu wa karibu kabisa, baba kamkataa mwanae na mkewe, mke kapambana kasomesha mpaka mtoto kapata kazi ndio baba anajitokeza kuomba msamaha ya kuwa ni ujana ulimsumbua. Kukwepa majukumu ni mbaya sana.

Huu ni wakati sahihi wa wana jf kuunlock ID's kusaidia wale ambao itathibitika ni wahitaji wakubwa.
NB: KAMA ITATHIBITIKA.
Acha mama tuitwe mama jamani[emoji24][emoji24]
Mmshike mkono mwenzenu ikiwezekana.
 
Inafika sehemu unakatana na kitu mpaka unajiuliza mara mbili mbili,ila haya yote ni maisha,kutoka kwenye Imani ya dini ni kwamba Mwenyezi ndio mpangaji
Nataka kusema wewe ni Mwanamke wa Shoka

Sent from my V2204 using JamiiForums mobile app
 
Cha muhimu watu mlio Katika ndoa wake kwa waume tulize de libolo kwa mke mmoja mlee watoto wenu na sio kila siku mnawaza uzinzi tu mwisho mnawatesa watoto kisa ndoa zenu fake
Kwa Mimi nikiwa km Jaji Mfawidhi wa JF ingawa wanasema ili uamue kesi pasina kuacha shaka yoyote yakupasa usikilize pande zote mbili, kwa kutumia principle ya 'judge as Caesar's wife' naona kwa mujibu wa mleta mada, mwenye tatizo ni yeye mwenyewe na sio mwanaume wake kwa sababu moja kuu na yenyewe sio nyingine bali ni kutokua muwazi na anatumia vificho hasemi ukweli maana kuna madudu aliyofanya nyuma ya pazia anayajua yeye mwenyewe na hawezi kuyaweka open hapa na kuthibitisha hilo moja ya madudu ni kumzuia mwanaume kuhudumia watoto wake hilo ni kosa haijalishi amekukosea kiasi gani Ila km watoto ni wake wana haki ya kupata huduma kutoka kwa baba yao, ugomvi wenu ni wenu sio wa watoto mtoa mada tuliza Wenge pokea matunzo ya watoto yakikushinda utaanza kulia kwenye vyombo vya habari kumbe wewe ndio mwenye kiburi, majivuno na kujiona unaeleza amekutafuta sana Ila umekua ukimkwepa hadi ameamua kukata tamaa kwa hio wewe ndio unaewatesa watoto sio mwanaume wako, unasema unalala na watoto wa kiume chumba kimoja uenda ya kua mwanaume wako ameliona hilo na anahitaji kukusaidia Ila ukamletea kiburi, jeuri na kujiona kua peke yako unaweza na hauhitaji msaada wake

Conclusion: jitafakari wewe mzazi km ulizaa nae kweli hao watoto angalieni namna ya kuwatunza hata akiwataka awatunze yeye ili usiishi nao chumba kimoja angalia jinsi ya kusolve hilo tatizo, sio kuongeza tatizo kwa chuki na Mambo yaliyopita

Nb: najua hujaja kuomba msaada
 
Baba Yao kasema yupo tayari kulea watoto wake na kuwahudumia so Cha muhimu watu mlio Katika ndoa wake kwa waume tulize de libolo kwa mke mmoja mlee watoto wenu na sio kila siku mnawaza uzinzi tu mwisho mnawatesa watoto kisa ndoa zenu fake
Baba yao kama walivyo wababa wengine wapuuzi, alikua anatafuta njia ya kujirudi Kwa mwanamke aendelee kupasha viporo.


Lkn pia inawezekana mpaka akataka kujirudi nisababu alipokuja mambo yalibadilika.


Ni chaguzi sahihi sana ALOFANYA mtoa Mada hata kama ana shida ya Uchumi.



Kuhusu wababa kutulia kwenye Ndoa zao, hapa suala ni Akili ya Mwanaume mwenyewe , Kuna hao wanachepuka na kusahau familia, alafu Kuna Mimi, nachepuka lkn Huniambii kitu Kwa Wife na wanangu na wanangu wengine.
 
Nimeshatoa mkono wa pole.
 
Mmmmmmhmn ila aisee kuna watu wana laana aisee. Sasa unamuacha mtoto wa watu na mizigo namna hii alafu yeye yupo huko somewhere na mipumbu yake anajiita mwanaume.

Huyu ilitakiwa akamatwe na polisi kabisa awekwe ndani na alipishwe pesa ndefu isiyopungua milioni 5. Halafu apewe masharti ya kulipa kodi, kutoa matumizi ya watoto na mke.

Jamaa mpumbavu sana huyo aisee.
 
m
Mtoa Mada ni Moja ya Wanawake wakweli na wawazi wa kiwango Cha juuu sana, Naam nandio sababu aliamua kusimamia maamuzi yake yakutorudiana na Jamaa Kwa sababu mtoa Mada anajijua ni mtu safi .


Wanhekua ni wale Wanawake wma waruwaru kiguuu na njiaaa, Siku jamaa alomtafuta, kwake angeona ni ahueni ya juuuu sana kwaivo asingzungusha.


Sheria ya mtenda maovu Huwa Iko hivi " Huwa yeye ni mwepesi wa kufurahia Msamaha unaompa as long as anajijua alikosea".
 
Hapana angekua ni mkweli asingeficha kisa Cha kukimbiwa na mwanaume wake, uongo uanzia hapo maana anaficha source ya tatizo lake
 
Mimi namlaumu mwanaume mwezangu kwakumwacha mke na watoto kama shida ni mwanamke angesaidia watoto.Yasije yakawa ya diamond na Omy Dimpoz.wtoto wemefanikiwa ndo baba unajitokeza. Hata huyo unaesema sio wako akikua bado atakutambua kama babaeke. Mimi naamini kwenye hizo familia zetu ,tunatunza watoto ambao kibaolojia sio wetu, lakini kwakuwa kapatikana katika familia yako huyo ni wako labda mkeo aseme sio wako. HEBU CHUKUA MUDA KUJIULIZA HIVI MTOTO HUWA ANAMCHAGUA BABA AU ANAMCHAGUA AKAZALIWE WAPI NA WAZAZI GANI. Mama pekee ndio mwenye uwezo wakuamua nizae na nani na MTOTO awe wa nani.Baba wewe kazi yako ni kulea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…