Niliporudi kutoka Uswisi baada ya kukaa kule wiki mbili niliona Dar ni chafu sana

Wiki mbili tu?!
 
Lema II
 
Sijawahi kupachukia Tz, ndio sipendi rushwa na uzembe wa kutokujituma, Ila kama nchi, sijawahi kuichukia. Miaka yangu ya mwanzo ughaibuni ilikuwa nikirudi Dar, najipima kama bado naweza kupata kiti kwenye daladala.
 
Huku wanafurahia kupata pombe na sukari!
 
Dar ni jiji la hovyo ila ndo jiji lenye michongo
 
Bro hapo ni wiki mbili tu🧐
Ungekaa 2 years sijui ingekuwajeπŸ™†β€β™€οΈ
 
Umeongea ukweli mchungu
 
Siyo hadi Uswisi, hata ukienda Mbeya tu nakurudi.

Kama umekulia Dar huwezi kujua, ila tuliokulia mikoani tunajua Dar ni pachafu kuliko mikoa yote.
 
Bila kwenda nchi iliyoendelea huwezi kujua umaskini wetu na shida nyingine zilizopo utaona sawa tu.
 
Suala la usafi na Tanzania halijawahi kuwa na umuhimu.

Sheria ndogo za Halmashauri zinatungwa, pesa za taka zinakusanywa zikifika kwenye FUKO La Halmashauri zinafanya matumizi mengine YA KULIPANA POSHO MADIWNI na Wakurugenzi, siyo TAKA TENA.

NI mwendo wa mihemko tu, mwanasiasa, mtu au taasisi wakiamka anajifanya kufanya usafi. Taka zinakusanywa zinakaa hapo mpaka zinasambaa Tena Hali inarudi zero.

Kwa mfumo huo usitegemee MIUJIZA miji kuwa Safi.
 
Lema mwenyewe kafunguka akili baada yakwenda ulaya
Unajua Mkuu, kama watanzania wangekuwa watu wa kusafiri nje ya nchi kwa wingi tungepata mabadiliko ya kifikra zaidi kuliko kutegemea TV picha mgando na video. Uhamiaji nao wanachangia kuweka vikwazo watu wapate pasi wakajifunze ilmu Dunia 😁 !.
Wanaotoka sana ni viongozi ambao licha ya kupata fursa ya kujifunza mazuri ya nje, wanaishia kujenga mahekalu na kuboresha makazi yao tu. Ubinafsi ufisadi na uroho wa madaraka ndio sala.
Lema yuko sahihi kwenye angalizo lake ingependeza sana viongozi wote wenye uzoefu na safari za nje wakafunguka pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…