Nilitahadharisha hapa kuwa 'Kesi' imemkalia vibaya 'Mwamba' na hachomoki kirahisi nikaishia Kushambuliwa

Nilitahadharisha hapa kuwa 'Kesi' imemkalia vibaya 'Mwamba' na hachomoki kirahisi nikaishia Kushambuliwa

Si wanajifanya Wabishi, Wajuaji na wanajua Kutukana na hawapendi Ushauri wa Kimaono kutoka Kwetu 'Philosophers' wa hapa Jamvini?

Sasa Ndugu yao ( Mwamba wao ) anaishia 'mazima' huko Segerea na hawatoamini.

Leo mbona hawanitukani, hawanishambulii na hawanidhihaki kama walivyonifanyia katika hizo 'Threads' zangu Mbili za awali?

chadema ni wajuaji
 
Ukitazama kwa mbali Ni kama hukumu tayari.......Yale mahojiano na BBC ndio ulikuwa matokeo ya kesi hii. Hakuna jipya Ni kupoteza Muda tu .......kikubwa Ni Mbowe kusimama kiume na kumuomba mahakama ifanye Kama itakavyoipendeza. Mawakili wajitoe wale wanaomtetea Mbowe. Wakibaki wale wa upande wa Jamhuri na Jaji nadhani SoMo litaeleweka.
 
Kwahiyo ulitaka aachwe afe na njaa?nyie vijana bure kabisa
Kwa ushahidi upi uliokuwepo wa kumtia hatiani Mbowe? Unamkamata gaidi kisha unamnunulia chakula na kukaa naye meza moja kula chakula huku akiwa hana pingu!? [emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
Sabaya si KATAMKA mwenyewe kwamba SI YEYE bali ALITUMWA na MAMLAKA yake ya UTEUZI!? Acheni kujitoa ufahamu!!!
 
Wafuasi wake pamoja na wale Mnaonichukia pindi GENTAMYCINE nikisema tu Ukweli leo mbona hamnitukani, hamnidhihaki wala hamnishambulii kama mlivyofanya katika zile Threads zangu Mbili za kutoa ( kuwapeni ) Angalizo kama siyo Tahadhari?
Kwa hiyo kwa akili yako finyu,unatafuta kutukanwa au, umezoea kutukanwa.Ujue,anayependa kitukanwa ni mtukanaji.Tafuta barabara mpya.
 
Nilitukanwa sana hapa na Wafuasi wake wakati GENTAMYCINE nilikuwa na nia njema nae tu ili asaidiwe Kiushauri na Kimawazo na Wadau mpaka Wataalam wa Kisheria.

Sasa kuanzia leo tutaheshimiana vizuri.
KwanI Mwamba ni nani zaidi ya Mbowe ambayo amekuwa akiitwa Mwamba na wafuasi wake? Hivyo umemtaja mtu Moja kwa Moja kwenye Uzi wako.
 
Ukitulia kabisa na kama tokea mwanzoni umeangalia Kesi ilivyoanza na inavyoenda huhitaji Akili Kubwa sana kujua kuwa ni Kesi ya 'Kimkakati' zaidi na lazima lililopangwa litokee.

Kwa nia njema tu nikaja na Threads zangu Mbili ( ambazo hata hivyo mpaka leo sijui kwanini ziliunganishwa au kufutwa ) kwa Makusudi kabisa nikitaka Mjadala wa 'Kihoja' uanze ili angalau Mawakili Wasomi wanaompambania waokote okote Mawili Matatu ya Kisheria waongezee na yao waliyonayo ili Mhusika anasurike na 'Kesi Mkakati' inayomkabili GENTAMYCINE nikaishia Kutukanwa, Kushambuliwa na Kudhihakiwa.

Haya baada ya Kilichotokea kwa hatua hii tu ya awali kile nilichokisema na Kukitahadharisha ukiwa na Akili Timamu na Kusoma pia Mazingira na Mtiririko wake mnadhani Mhusika haendi Kuozea Jela na labda ni suala la muda tu?

ANGALIZO

Sijamtaja Mtu katika Uzi wangu huu bali nimeelezea tu hivyo sitaki Kuulizwa namuongelea nani na mtakayemhisi huyo mmemuhusi nyie ila siyo Mimi Mleta Mada.

Taratibu sasa tutaanza Kuelewana JF!!!!
Hakuna haki
 
Hakuna haki
Ila kwa Sabaya Kwenu Haki ilikuwepo? Wanafiki wakubwa nyie. Mkishauriwa na Kutahadharishwa mnaishia Kututukana sasa 'Mwamba' wenu yanaenda Kumkuta na lazima Jela imkute hata ya miaka Mitatu au Minne hivi.
 
Siyo lazima tukubaliane wote kwenye hili la Mbowe na wenzake kuwa haki imetendeka au haijatendeka

Unachotakiwa kukifahamu ni kwamba, kesi ya Mbowe na wenzake ni tofauti kabisa na kesi ya Jambazi Sabaya
Leo mtasema kila aina ya Utumbo wenu.
 
Hakuna Mahakama huru nchi hii.

Hii kesi ilistahili kufuwa siku nyingi tu.

Lengo ni kumuweka ndani wakiamini chama kitayumba na hii ni kwasababu akil zao ni fupi.
Kabisa, hata Sabaya ameonewa sana kwa sababu hatuna mahakama huru, kesi ya Sabaya tungekuwa na mahakama huru ingefutwa na si kumfunga eti miaka 30


Ilisikika sauti moja ya mwanakijiji mmoja [emoji1787][emoji1787]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Halafu 'Makamanda' leo mbona mnachangia 'Kihuruma' sana tofauti na mlivyokuwa mkichangia kwa 'Kunitukana' katika zile 'Threads' zangu Mbili nilizomuanzishia huyu 'Mwamba' wenu ili Kuwatahadharisha?

Yaani kabisa Philosopher King GENTAMYCINE nihisi Jambo au nionye kuhusu Jambo fulani halafu lisije kutokea? Thubutu....!!

Kitu pekee ambacho nawashauri ni Kumpambania tu Mtu wenu 'Mwamba' asifungwe miaka mingi kama ambavyo dalili zinaonyesha ili angalau hata afungwe tu kati ya miaka Mitatu au Minne.

'Makamanda' leo mbona hamnitukani?
Kwanza Mimi sina itikadi ya chama chochote nachangia kama raia aliyeguswa na kesi, kwanini
1.hii kesi matokeo yake yana adhari kwa kesi zijazo ie inaweza kufanywa rejea Sasa kama maamuzi hayo yatakua ya kimkakati kesho au kesho kutwa yatatumika kwenye kesi ya mtu mwingine au hata Mimi
2. Jaji kukataa mapingamizi kwa kufuata maoni binafsi bila rejea ya vifungu vya kisheria inaacha maswali kuliko majibu ie pigamizi la maelezo kuchukuliwa nje ya muda wa kisheria kisa mtuhumiwa alitumika kumtafuta mtuhumiwa mwingine je polisi kazi yake nini?
3.kesi ya kimkakati, je huo mkakati kwa maslahi ya nani?, Kama ni kwa maslahi ya taifa sawa lakini kama ni maslahi ya kibinafsi sio sawa na ni suala la kukemewa bila kujali uko upande gani
 
Jaji kaweka sheria pembeni kaamua vile anvyoona yeye itampendeza kwa maagizo ya aliyempandisha cheo siku chache zilizopita.
 
Back
Top Bottom