Kiuhalisia hii habari siyo halisi kwa vigezo vifuatavyo:
Kutembea na huyo mzee na kisha kuchumbiwa na kijana bila kujua siyo kosa.
Binti kwenda kutambulishwa kwa wazazi na kukuta hawara yake ndiye mkwe, jambo hilo na uchumba huo ungeliishia hapo hapo na thread hii ingeliletwa kwa kichwa cha habari kingine na si hiki.
Lakini binti kukomaa kuendeleza uchumba huo na kutafuta ushauri toka kwa hadhira, ndiyo inathibitisha kuwa jambo hilo ni la kufikirika, halipo ni chai ya strungi yenye tangawizi nyingi kabisa.