Wiki inayofuata nikaenda shule kama kawaida tulikuwa na ratiba baada ya vipindi vya asubhi na Ilikuwa ni wiki ya kufunga ni Michezo jioni tunashindana baina ya madarasa hivo ni eneo la wazi watu wa maeneo ya karibu wanakuja kuangalia mpira
Nilikuwa mshangiliaji mzuri Sana Sina hili Wala lile naona wenzangu wamenikazia macho sana nikaona sio kesi nikaendelea zangu kushangalia rafikiyangu akanifata akanambia angalia kule juu
Aisee nilishtuka H huyu hapa kapendeza hata ukae Kona ipi unaona kijana wa watu alivosmart kiroho kikaanza kudunda
Wakati nashangaa shangaa nikaletewa ujumbe kwenye kikaratasi
"Nataka kuongea na wewe kipenzi"
Nikasoma.nikatabasamu hakuondka Hadi mpira ulivoisha kengele ikagongwa tukaruhusiwa Nikapewa ujumbe nasubiriwa njia fulani na H nipite huko sababu kwetu hakukuwa mbali na shule hizo hiyo njia ni mzunguko kama.dakika 25 had kufika kwetu
Nikapita ile njia kama nikivoelekezwa nikamkuta H kasimama ananisubiri akanipa mkono kunisalimia nami nikapokea ndo Ilikuwa siku ya kwanza tunapeana mkono kma hivo tukaanza story huku tunaelekea nyumbani ilikuja story za kawaida za shule nilipokaribia home akaniacha akaondoka akasema atakuja siku inayofuata
Siku ya pili akaja Tena ikawa hivo nakumbuka Ilikuwa ijumaa siku ambayo siis tulifunga shule nae alikuja akawa amekaa kule njiani ananisubiri aisee nikagundua Kwa yule Kaka sichomoi Yani akiniangilia ni kama naishiwa pozi
Siku alijipanga naona nilikuwa nimechelewa kutoka
Alivoniona akanihug mm Kwa aibu aibu nikakubali lakini ni kama network zilikata
Nilikiwa akanishika mkono akaanza maneno yake Yale ya kwenye barua nikawa nimesimama nimejinamia muda wote namuangalia Kwa kuibia😃😃😃
Akanambia vipi mbona uko hivo nikamjibu amna kitu nilikuwa kimya mda wote akasema nataka kuongea na wewe Leo Hadi jion nikamwambia sawa hakuna tabu hatukuwa na sehemu ya kwenda wakat ule tukatafuta sehemu tukakaa muda huo mm mgeni wa kilakitu kwenye mahusiano naona aibu tu siwez hata nilichokuwa nashangaa spidi ya damu kutembea mwilini imeongezeka confidence Iko low akiningalia ni kama natamani kukimbia lakn siwez 😂😂😂