Nilivoachwa kikatili na mpenzi wangu wa kwanza

Nilivoachwa kikatili na mpenzi wangu wa kwanza

Hii wiki Niko very happy ngoja niwape kisa nilivyoachwa na mpenz wangu wa kwanza😃😃

Miaka mingi nyuma nilikuwa na rafikiyangu ambae ni jirani yetu pia alinizi kama miaka miwil umri, alikuwa anansoma shule ya boarding hivo tulikuwa tunaonana kipindi cha likizo.

Rafik yangu alikuwa ni wale watoto kwenye zile familia maarufu mtaani tumuite Irene
Siku moja tukiwa tunapiga story akanambia ana ujumbe kutoka Kwa H tumpe Hilo jina
nikamwambia anipe akaingia ndani akaja na barua 😃akasema Itabid nirudishe majibu kunamtu apewe aende nayo maana hayupo Kwa Sasa

Nikaichukua nikasema hebu nikaifungue nikiwa home bhana nafungua nakutana na ujumbe maridadi kweli kweli.

Barua ya mapenz iliyoshiba kweli kweli maneno matamu mwanzo Hadi mwisho nakupenda nying sana huku mwisho na dedication za kutosha nlisoma Ile barua huku natabasamu vibaya mno 😃😃

Kuhusu H
Ni mkaka fulani mpole sana ni binamu wa rafikiyangu hivo nilikuwa namuona maranyingi akija kutembea kwa shangazi yake huku mtaani kwetu.

Alikuwa anasoma shule moja ya kubwa ya seminary hapo mkoani babayake alisoma pamoja na mama yangu enzi hizo hivo namfahamu japo hatukuwa na ukaribu

Ile barua nilifurahia mno H alikuwa kijana smart sana,na hii ndo Ilikuwa mara ya kwanza kwangu kuvutiwa na mvulana nikamwambia akamwambie anipe muda nifikirie nitampa majibu wakat huo H alikuwa likizo Dar Kwa nduguzake wengine so barua alimpa rafikiyake wakiwa shule Ili inifikie Kwa urahisi na sikuwa natumia simu kipindi hiko.

Bas bhana feeling Kwa H zikaanza japo sikuwa naelewa Kwamba mapenzi ndio yalivo nikawa naona ni busara kuisoma Ile barua Kila mara Kwa kuirudia rudia😃😃😃

Baada ya wiki 2 nikaenda kwao na Irene Ile nafika sebuleni namkuta H kajaa tele nikaona aibu sana akanisalimia nikakaa kwenye kochi kiroho kinadunda sana nikaona hapa siwezi nikaaga nikaondoka muda huo H akanikata jicho la wizi wizi 😃

Wazazi wao hawakuwepo mda huo mara Irene akaniita niende kuongea na H

Akatoka nje nikamfuata tukakaa sehemu nyuma ya nyumba ya shangazi yake

Akauliza kuhusu jibu lake nikaanza kujizungusha zungusha nikakataa H alilalamika sana nikaona machozi yanaanza kumtoka 😭

Akabembeleza sana mwisho nikakubali wakat huo tumekaa mbali kidogo hivo hatukushikana hata mkono H akaaga akaondoka.

Safari ya mapenzi ikaanza
Kimbele mbele kikazidi 😃😃
Ilikuwa siku chache aondoke shule na Huwa akiwa shule hatumii simu mm pia sikuwa na simu kabisa akaja kuniaga akaondoka

Inaendelea sio ndefu
Noma sana!
 
Wiki inayofuata nikaenda shule kama kawaida tulikuwa na ratiba baada ya vipindi vya asubhi na Ilikuwa ni wiki ya kufunga ni Michezo jioni tunashindana baina ya madarasa hivo ni eneo la wazi watu wa maeneo ya karibu wanakuja kuangalia mpira

Nilikuwa mshangiliaji mzuri Sana Sina hili Wala lile naona wenzangu wamenikazia macho sana nikaona sio kesi nikaendelea zangu kushangalia rafikiyangu akanifata akanambia angalia kule juu
Aisee nilishtuka H huyu hapa kapendeza hata ukae Kona ipi unaona kijana wa watu alivosmart kiroho kikaanza kudunda

Wakati nashangaa shangaa nikaletewa ujumbe kwenye kikaratasi

"Nataka kuongea na wewe kipenzi"
Nikasoma.nikatabasamu hakuondka Hadi mpira ulivoisha kengele ikagongwa tukaruhusiwa Nikapewa ujumbe nasubiriwa njia fulani na H nipite huko sababu kwetu hakukuwa mbali na shule hizo hiyo njia ni mzunguko kama.dakika 25 had kufika kwetu

Nikapita ile njia kama nikivoelekezwa nikamkuta H kasimama ananisubiri akanipa mkono kunisalimia nami nikapokea ndo Ilikuwa siku ya kwanza tunapeana mkono kma hivo tukaanza story huku tunaelekea nyumbani ilikuja story za kawaida za shule nilipokaribia home akaniacha akaondoka akasema atakuja siku inayofuata

Siku ya pili akaja Tena ikawa hivo nakumbuka Ilikuwa ijumaa siku ambayo siis tulifunga shule nae alikuja akawa amekaa kule njiani ananisubiri aisee nikagundua Kwa yule Kaka sichomoi Yani akiniangilia ni kama naishiwa pozi
Siku alijipanga naona nilikuwa nimechelewa kutoka
Alivoniona akanihug mm Kwa aibu aibu nikakubali lakini ni kama network zilikata
Nilikiwa akanishika mkono akaanza maneno yake Yale ya kwenye barua nikawa nimesimama nimejinamia muda wote namuangalia Kwa kuibia😃😃😃
Akanambia vipi mbona uko hivo nikamjibu amna kitu nilikuwa kimya mda wote akasema nataka kuongea na wewe Leo Hadi jion nikamwambia sawa hakuna tabu hatukuwa na sehemu ya kwenda wakat ule tukatafuta sehemu tukakaa muda huo mm mgeni wa kilakitu kwenye mahusiano naona aibu tu siwez hata nilichokuwa nashangaa spidi ya damu kutembea mwilini imeongezeka confidence Iko low akiningalia ni kama natamani kukimbia lakn siwez 😂😂😂
kumbe ni tamthilia/soap opera
 
story yako inanipa huzuni sana, hasa pale ulipokuwa ukimlilia kwa simu na yeye akawa mkatili zaidi ya pilato
 
Back
Top Bottom