Kunatukio nilisahau
Baada ya Ile siku ya tukio na kuachwa nilikutana na yule kaka nilosimama nae pale kwenye sherehe nae alisikia hiz tetesi nilimlaum nikajua yeye ndio kaongea uongo akasema nitampata alisema sababu story mtaani Ilikuwa hiyo tu mm kuliwa na kuachwa na H 😂😂😂
Baada ya masaa hiv nikaja kuitwa na Irene yule kijana alimpata aliesambaza hizo habari za uongo alafu yule kijana aliekuwa ananiaproach alikuwa Mkubwa kuliko sisi hivo Ilikuwa rahis kumpata nikamkuta kamshika shati kisawa sawa
Nilivofika akasema aniambie alichosema akakubali yeye ndio alisema baada ya kuona tumesimama pale akawaambia watu hiyo taarifa lakin hakuwa na uhakika kama tulitoka pamoja
Jamaa akamzimua makofi mawili matatu mda huo vijana wa pale mtaani walikuwa kma 7 hivi wakamzomea ikawa nafuu yangu lakini nilishapoteza tayari
Baada ya miak kupita nikawa na mahusiano mengine ila nilimpenda sana H baada muda hasia zikaanza kupungua nikawa najihis nakuwa sawa hata kumfikiria kukapungua namba yake ya Simu ikaanza kufutika
Nikawa namuona H ila sikufanikiwa kuongea nae chochote akaenda kusomea udaktari nikaambiwa,nami nikaenda chuo
Sikumoja nipo likizo nikapigiwa simu namba ngeni
Nikapokea
Halloo nikauliza nani akasema ni H
Mmh nikamuuliza kama yukoo poa akasema yupo sawa akaomba kuniona siku ya pili nikamwambia kama nitakuwa na nafasi nitamjulisha nikapotezea japo nilikuwa na shauku ya kumsikia anachotaka kuniambia
Siku ya pili sikumtafuta siku ya Tatu akanipigia akasema yupo mtaani kwetu nikamwambia sawa nikaenda kumuona akasema amenikumbuka
Akasema usiku ule alipigiwa simu na watu akaambiwa kuwa nipo na yule kijana pia kuwa ni mwanaume wangu na nilitoka nae usiku ule roho ilimuuma sana na kibaya zaidi akaambiwa kuwa nililala na yule kijana alafu yule kijana ni wale mabishoo wa pale mtaani na ni Mkubwa kuliko sisi Hilo lilimuumiza Zaidi
Lakin Bado ananipenda tuwe pamoja 😀😀😀
Nikamuuliza sababu ya kutonisikiliza akasema ni hasira na maumivu alihis kile kitu ni Cha kweli ila anajutia