Nilivoachwa kikatili na mpenzi wangu wa kwanza

Nilivoachwa kikatili na mpenzi wangu wa kwanza

Hii wiki Niko very happy ngoja niwape kisa nilivyoachwa na mpenz wangu wa kwanzaπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

Miaka mingi nyuma nilikuwa na rafikiyangu ambae ni jirani yetu pia alinizi kama miaka miwil umri, alikuwa anansoma shule ya boarding hivo tulikuwa tunaonana kipindi cha likizo.

Rafik yangu alikuwa ni wale watoto kwenye zile familia maarufu mtaani tumuite Irene
Siku moja tukiwa tunapiga story akanambia ana ujumbe kutoka Kwa H tumpe Hilo jina
nikamwambia anipe akaingia ndani akaja na barua πŸ˜ƒakasema Itabid nirudishe majibu kunamtu apewe aende nayo maana hayupo Kwa Sasa

Nikaichukua nikasema hebu nikaifungue nikiwa home bhana nafungua nakutana na ujumbe maridadi kweli kweli.

Barua ya mapenz iliyoshiba kweli kweli maneno matamu mwanzo Hadi mwisho nakupenda nying sana huku mwisho na dedication za kutosha nlisoma Ile barua huku natabasamu vibaya mno πŸ˜ƒπŸ˜ƒ

Kuhusu H
Ni mkaka fulani mpole sana ni binamu wa rafikiyangu hivo nilikuwa namuona maranyingi akija kutembea kwa shangazi yake huku mtaani kwetu.

Alikuwa anasoma shule moja ya kubwa ya seminary hapo mkoani babayake alisoma pamoja na mama yangu enzi hizo hivo namfahamu japo hatukuwa na ukaribu

Ile barua nilifurahia mno H alikuwa kijana smart sana,na hii ndo Ilikuwa mara ya kwanza kwangu kuvutiwa na mvulana nikamwambia akamwambie anipe muda nifikirie nitampa majibu wakat huo H alikuwa likizo Dar Kwa nduguzake wengine so barua alimpa rafikiyake wakiwa shule Ili inifikie Kwa urahisi na sikuwa natumia simu kipindi hiko.

Bas bhana feeling Kwa H zikaanza japo sikuwa naelewa Kwamba mapenzi ndio yalivo nikawa naona ni busara kuisoma Ile barua Kila mara Kwa kuirudia rudiaπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

Baada ya wiki 2 nikaenda kwao na Irene Ile nafika sebuleni namkuta H kajaa tele nikaona aibu sana akanisalimia nikakaa kwenye kochi kiroho kinadunda sana nikaona hapa siwezi nikaaga nikaondoka muda huo H akanikata jicho la wizi wizi πŸ˜ƒ

Wazazi wao hawakuwepo mda huo mara Irene akaniita niende kuongea na H

Akatoka nje nikamfuata tukakaa sehemu nyuma ya nyumba ya shangazi yake

Akauliza kuhusu jibu lake nikaanza kujizungusha zungusha nikakataa H alilalamika sana nikaona machozi yanaanza kumtoka 😭

Akabembeleza sana mwisho nikakubali wakat huo tumekaa mbali kidogo hivo hatukushikana hata mkono H akaaga akaondoka.

Safari ya mapenzi ikaanza
Kimbele mbele kikazidi πŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Ilikuwa siku chache aondoke shule na Huwa akiwa shule hatumii simu mm pia sikuwa na simu kabisa akaja kuniaga akaondoka

Inaendelea sio ndefu
Ngono ndio taaluma tunayoijua wabongo!
 
Unayumba sana Kijana fanya kazi kwa uaminifu ili upande vyeo πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Hahaha!!sawa mkuu

Tegemea mambo mema na mazuri mkuu sitakuangusha

Wacha niweke dalili nyemelezi sehemu na eneo husika
 
Back
Top Bottom