Nilivyotelekezwa na rafiki yangu Queens Bridge, New York nikiwa sina hata 100 mfukoni

Nilivyotelekezwa na rafiki yangu Queens Bridge, New York nikiwa sina hata 100 mfukoni

India wanazo sana hizi classes na ulaya zipo hizi, ndio maana ukiona mwafrika yupo kaoa mzungu ujue huyo mzungu wa lower classes. High classes kuolewa na kapuku mweusi mbeba mabox haipo hio, maana kwanza mtakutana wapi?? Sasa mbongo kakulia huko kazuramimba kaja Daslama mtu mzima kama baba Levo unaparamia mtoto aliekulia O'bay lazima watoto wa mjini watakusaidia tu. Ndoa ni kuangalia mtu mnaeendana nae, tena uwe umemzidi vitu vingi sana. Haya tuendelee na story yetu ya New York huko, huu mchezo wa kuwakimbia wabongo mamtoni upo sana. Mtu unawasiliana nae toka Dar ukishuka JFK unakuta hola ukipiga simu zinaenda voice mail..Tumezipitia hizi haahaahaa.
Na sie watu wa dar hii michezo tunawafanyia sana watu wanaotoka buzirayombo
 

Attachments

  • Screenshot_20230126-165646.png
    Screenshot_20230126-165646.png
    21.7 KB · Views: 25
Jamani hapa story ni kwamba popoma ni Mtoto wa Mjini daslamu🤣🤣🤣 na kwamba yupo Daslamu toka miaka ya tisini. Hakuna cha QB wala Jamaica Queens wala BK(Brooklyn)

Mkuu ( kama wewe Sio popoma) umejivunjia heshima sana.

Huyo popoma hata mwandiko wake tu unaonekana ni bushman.
 
Miaka ya tisini na mwanzoni nwa miaka ya 2000 kulikuwa na wimbi la vijana kuzamia South Africa,Ulaya au Marekani.

Zilitumika njia zote haramu na halali ikiwemo kuzamia meli mpaka bendi ya Orchestra Vijana Jazz wakatunga wimbo wa Ngapulila.Hemed Maneti na Eddy Sheggy waliimba si mchezo RIP

Mtaani kwetu Chole Road Oyterbay tukiishi na vijana kama akina Tonny na huyu Gentamycin wa jf ,karibu kila nyumba ilikuwa na kijana yuko nje ya nchi.msimchukulie poa Genta,yupo Newsroom kwenye Media House moja kubwa hapa bongo

Kulikuwa na watu wakifanya udalali na michongo ya kupeleka watu nje ,enzi hizo tukiwaita wasanii, kijiwe chao maarufu kilikuwa Shaaban Robert Street ulipojengwa ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere.

Mwaka 2001 nikasema liwalo na liwe lazima niondoke nchini, nikamshirikisha mzee akakataa, hapo nina vyeti vangu vya form six na division two ila nilikosa admission ya UDSM kwa kozi ya sheria baada ya kufeli mtihani wa multiculation, wazee wenzangu akina pascal Mayala wanaukumbuka huu.

Enzi hizo hata kama una division one huwezi kujoin UDSM bila kufanya huu mtihani wa multiculation, na ukiufeli imekula kwako. Ovyo kabisa sijui profesa Luhanga aliwaza nini, kipindi hicho hakuna bodi ya mkopo, ukipata admission ni kama unasomeshwa bure na serikali bila deni

Nilikataa kusoma Tumaini University na vyuo vingine
maana enzi hizo ukitamka neno Chuo Kikuu akili yako inakupeleka UDSM, niliona ndio chuo pekee ninachostahili kusomo, akili ya utoto ilinisumbua.

Nikaona hapa lazima nikasome nje ya nchi,

Mzee akikuwa amenitafutia tempo kwenye ofisi moja huko Posta, ni nikajuana na hawa wasanii, madakali wa kupeleka watu nje.

Hiyo tempo ilikuwa inanilipa sana kwa hiyo michongo yote nilijigharamia, Chuo kikatafutwa, bank statement ikatafutwa ya mchongo, admission letter na form muhimu sana ikiitwa I-20.nikafanya na mitihani ya TOEFL nikapata marks nzuri tu

Nikapewa twisheni ya maswali yanayoulizwa ubalozini.kipindi hicho ubalozi wa USA uko Kinondoni huko ndani ndani karibu na nyumba ya Reginald Mengi

Siku moja kabla ya kwenda ubalozini yule msanii akaniambia tukutane Mwananyamala niende na kiasi cha shilingi 20,000. Sikujua kazi yake ila nikaitikia wito

Kwa mara ya kwanza nikakutanishwa na mganga uso kwa uso eti ana dawa ya kuwapumbaza maofisa wa Ubalozi wa Marekani wasininyime viza. Nikagoma ila msanii akaniambia shauri yako ukikosa viza usinilaumu, unadhani Ulaya watu wanaenda kizembe nikakumbuka gharama nilizotumia kwa shingo upande nikakubali kuoshwa, kesho yake nikaenda ubalozini kuomba viza.

Kama Mungu maswali yote nilikuwa na majibu yake na document zilikuwa zimekamilika nikagongewa viza yangu safiii.

Ikumbukwe hapo mzee hafahamu kitu kuhusu huu mchongo,

Sasa kule USA kulikuwa na rafiki yangu akiishi New York maarufu kama Mudy White mtoto wa Sinza alitangulia kwenda kule mwaka mmoja kabla, tulikuwa tukiwasiliana kwa email na simu, akaniahidi kuwa atanipokea na akanipa address ya nitakapomkuta.

Ikumbukwe sikuwa na school fees ila nilitegemea nikifika kule nibebe box then nipate ada nijisomeshe.

Kufupisha story,siku ya siku nikatua uwanja wa John F Kennedy ambao upo New York, Nikampigia simu jamaa akasema panda MTA njoo Queensbridge.

MTA ni kama mabasi yetu ya mwendokasi, nikafika eneo la tukio piga simu weeee kwenye call box simu haipokelewi, giza likaingia nikaambaa ambaa Jamaica Avenue nikalala kwenye kibaraza cha duka
Mfukoni nina dola pungufu ya 50,ambazo kwa USA ni kama huna kitu, tena ukiwa mgeni na huna pa kulala.

Kesho yake nikaingia mtaani nikajichanganya kwa kufanya vibarua vya hapa na pale nikazoea mazingira nikawa mwenyeji

Nikapata demu wa kizungu nikazaa nae watoto wawili, chuo sikusoma, kuna siku akanitukana nikampiga kofi akapiga simu polisi msobe msobe nikalala selo .
Ikagundulika mimi nina student visa ila sisomi,sijui yule mama alinichongeaje.mara paa nikatunukiwa .

Nilirudi bongo na mapumbu yangu tu na picha nilizopiga nikiwa USA

Namshukuru muddy white alinifundisha kupambana huenda angenipokea ningebweteka

Nilikataa kusoma Tumaini University ila kwa sasa sina degree sina mke,nabangaiza tu mjini na umri umekwenda ila nafurahia maisha
Qb ya Bunda vijijini. Popoma tena🤣🤣🤣
 
Yule mwanamke wa kizungu alifanya niwachukie wanawake wote,nikapata mwanamke wa kichaga baada ya kurudi nchini nae alinizingua sana,nina chuki na wanawake na sitokuja kuoa
duhu wote hawafanani lakini mkuu
 
Hizi story za kuzamia zimenikumbusha jamaa tunafahamiana kiasi, kaenda States 2019 hapo kama daktari na hata stethoscope hawezi kuitaja achilia mbali kuijua.

Mwingine kasepa Canada mwaka jana, kufika inabidi ajifanye kakimbia vitendo vya unyanyapaa na ukatili kwa mashoga. Na mshkaji ni muislam safi, na hajui kitu kabisa kuhusu hizo mambo.
Hii ya kujifanya shoga inalipa sana siku hizi mambele

Ningekuwa kidume tayari ningejigeuza cocastic nile bata Canada

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Kwa ambao hawajawah kusoma au kufika nje watajua ni chai. Nishaona wa Nigeria kibao wanalala Central Station hadi wapate mademu wa kuwabeba wapambane maisha yaende.
Nlishasema siwezi kwenda nje bila ramani maalumu....neverrrr. hakuna kitu kigumu kama kuwa kwenye nchi za watu halafu uwe homeless and paperless na zaidi jobless
Wale homeless wa Philadelphia nikiwaona huwa nashangaa sana...afu wooote mateja *****

Nasema duuh hii ni marekani au naota[emoji848]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Pole ila mimi ninaiangalia upande wa pili wa coin, mkuu sasa umeona ni jinsi gani wenzetu walivyokua very seriously na hii GBV, once u rise your hands kwa ke hiyo ni treason case, sasa umepoteza watoto na opportunity nzuri na upo black listed USA nzima, hapa kwetu tunaona wanawake kama playing toy's zetu, pole na jipange upya, apologize kwa mzazi mwenzako then mwombe akawaone home dept ili wakuondoe kwenye list ya ukatili towards women, maana hii mkuu ndio kikwazo kikubwa wewe kurudi USA
...wadada wa kibongo someni hii kwa pupa nje mlete midomo mirefu.. utachezea kelebu na bongo sifukuzwi sababu ni nchi yangu.!
 
Wale homeless wa Philadelphia nikiwaona huwa nashangaa sana...afu wooote mateja *****

Nasema duuh hii ni marekani au naota[emoji848]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Ukiacha mateja wapo ambao wanapambana kulala nje na kwenye clubs na bar Mwisho wa siku wanapata wenza wanaoa wanasoma wanapata kazi na karatasi juu.
Me hyo subira sina
 
Back
Top Bottom