Nilivyoyaona maendeleo ya Tanzania baada ya kuwa Ulaya kwa zaidi ya miaka minne

Mtoa mada unachekesha yaan kwenye hii Africa Kampala na Nairobi ndo za kutolea mfano? kwanza unaijua nairobi wew huwa ukisikia kibera haraka haraka unafikiria ni kongo
 
Ambao atujawahi kwenda ughaibuni gonga like halafu pita mbele
 
Mkuu wangu kwa suala la mbu
Nikujulishe mbu wanapatikana kwenye tropical climate , Africa karibu yote iko kwenye tropical area kasoro the most south na the most north ambazo ni subtropics

Kushangaa mbu Africa naona ni kukosa tu uelewa mbu anazaliana KWA wingi Africa sababu ya hali ya hewa ,Ulaya hakuna mbu si KWA sababu wamemdhibiti hapana ni KWA sababu hali ya hewa hairuhusu kuzaliana huko

Kushangaa ugonjwa wa malaria Africa ni sawasawa na kushangaa ugonjwa wa Frost bite Ulaya , Africa KWA namna yoyote hatuwezi kuugua FROST BITE sababu ya hali ya hewa huo ni ugonjwa wa maeneo ya extreme cold wala Ulaya huwezi kukuta malaria maeneo yao mengi ni frigid na malaria inastawi kwenye tropical climate
 
Ungefika Chato Mkuu, miaka minne ambayo wewe hukuwepo tumeitumia kujenga Chato na sasa ni mji wa kitalii
 
Mkuu uliyoyaongea ndiyo wengi wetu tuishio nje tunavyooona. Hatudharau kwetu, nyumbani kwetu ni kuzuri kutokana na utamaduni wetu, amani bado ipo na tunajaliana hata km kiunafk, ila kimaendeleo bado tupo nyuma saaaaana.
 
Hata huko Marekani ukibebewa mzigo..
Unatazamwa kusubiria tips..
Hata restaurant tu au bar wana hadi policy za tips...wengine ni sehemu ya malipo..

Hilo la kubebewa mzigo na kutoa asante nafikiri lipo dunia nzima..
 
Watanzania kwanini huwa mnakuwa wakali mkiambiwa ukweli.
 
Kwa ijumla miji ya Tanzania kimpangilio, ni ovyo sana.

DSM, sijui utailinganisha na mji gani!!

Achilia mbali miji ya Ulaya, hata ukilinganisha na miji ya Afrika tu, DSM si lolote, si chochote.

Hayo madaraja yanayoitwa flyovers, si chochote. Nilienda wakati fulani Bamako, Mali, nchi ambayo karibia robo tatu ni jangwa, ina mpangikio mzuri, mara 10 zaidi ya Dar. Flyovers wala siyo kitu cha kuongelea, ni kitu cha kawaida, na sijui zipo ngapi!!

Ukienda tu hapo Maputo, mji umejengeka na kupangwa hasa, japo pembeni kabisa huko, ni takataka. Lakini kati kati ya mji, ni mji hasa. Tunajisifu na daraja la Nyerere, letu ni fupi kuliko la Maputo.

Nenda Harare, Dar ni takataka.

Sisi tatizo letu, mafanikio kidogo, kelele ni nyingi sana.
 
Wabongo tukiambiwa ukweli tunalialia Sana.
Tembeeni nchi za watu muone tulivyo nyuma.
Siku moja nenda katembee hata hapo windhoek - Namibia uje kusimulia hapa wenzenu wanavyoishi.

Hakuna mtu anapenda kuishi maisha ya kijinga ya uswahili. Sema ni umasikini tu tunashindwa kuishi maeneo mazuri usijitetee eti unapenda uswahilini sema huna hela ya kuishi sehemu Bora.

Diamond kazaliwa Tandale ila leo anaishi mbezi beach kwani Tandale hapaoni.

Mama Diamond anaishi zake madale.

Mbosso alikuwa anaishi huko uswazi mbagala Ila sasa hivi anaishi zake Mbweni.

Lavalava Yuko upanga.

Hawa ni mastaa wachache ninaowajua walikuwa wanaishi Uswazi ila baada ya kuzipata wamehama Uswazini na kutuacha sisi masikini.


Maisha ya uswazi Ni umasikini tuache kujifariji na vitu vya kipumbavu.
 
Ni mawazo mazuri, lakini mkuu Hivi Kampala kuna Flyovers? Kuna sehemu umesema ile ya Kijazi kwa Kampala ni kichekesho!
Kampala zipo, zaidi ya 15, ukitaka kuziona usiingie katikati ya jiji ukiwa unatokea Masaka, nenda moja kwa kwa njia ya pembeni ukiwa unaelekea Namboole Mandela Stadium.

Au ukiwa unaenda Entebbe airport basi nenda na Express Road from city centre.
Mtoa mada unachekesha yaan kwenye hii Africa Kampala na Nairobi ndo za kutolea mfano? kwanza unaijua nairobi wew huwa ukisikia kibera haraka haraka unafikiria ni kongo
Nairobi nimekaa miezi 3. Napajua kila kitu. DSM kwa Nairobi inabidi tujipange. Huu ndiyo ukweli japo ni mchungu sana.
 
Kuna rafiki yangu mmarekani aliwahi kaniambia Mnawezaje kuishi sehemu mko congested namna hii
Kuna wakati nilikuwa na jamaa waliotoka Ulaya. Tulikuwa kwenye chopa iliyokodiwa toka South Africa. Wale bwana ilikuwa mara ya kwanza kutembelea nchi ya Afrika, nje ya Afrika Kusini.

Tulitua eneo moja mkoani Tabora. Nikawaona wameduwaa. Nikawauliza kuna nini? Wakasema, hawa watu maisha haya wanaoyishi, nikisoma vitabu vya historia kule kwetu, inaonekana ni aheri maisha ya karne ya 18 Ulaya.

Ndiyo maana wenye akili wakimsikia mtu akisema kuwa Tanzania ni tajiri, tupo vizuri - hawawezi kuelewa kama huyo mtu ni mzima kabisa!!
 
Kwanini tunapiga kelele kwa vijiendeleo kidogo tunavyovishuhudia katika nchi yetu? Tunafanya hivyo kwa sababu kwa muda mrefu sasa watanzania (na waafrika kwa ujumla) tumezoea kusikiliza negative publicity kuhusu nchi zetu, watu wetu na maisha yetu kwa ujumla.

Siku zote wazungu kupitia vyombo vya habari vyao wamekuwa wakiitaja Afrika kama "dark continent", "poorest continent", n.k, n.k. Juzi juzi mke wa Bill Gate hadi aliitabiria Afrika kuwa maiti zitakuwa zikiokotwa barabarani kwa sababu ya corona.

Unaweza kudhani hizo negative publicity hazina lengo. Zina lengo, na lengo lake kubwa ni kutengeneza mazingira ya kinyonge kwa waafrika, na sisi kuendelea kuzidi kujiona duni, na utu wetu kudharirika. Mtu ajionavyo mwishowe huwa hivyo.

Nimefanya kazi na wazungu -- kitu kimoja nimejifunza kwao huwa hawakiri udhaifu hata kidogo hata kama wana udhaifu. Labda nikupe mfano labda utanielewa. Nilipata kufanya kazi katika taasisi fulani ya elimu ya juu nchi fulani ya wazungu (sitaitaja). Mi nilienda huko na mindset kwamba kwa vile wazungu wapo juu basi kutakuwa na mambo mengi ya kujifunza kwao kuliko wao kujifunza kwangu. Ila baada ya kukaa nao kwa muda kama mwezi nikagundua kumbe kuna mambo mengi waliyohitaji kujifunza kwangu kutokana na ujuzi na uzoefu wangu wa awali, kwa aina ya projects tulizokuwa tunazifanya. Sasa tabu ikaja pale walipokuwa wanahitaji kupata solution ya kitu fulani, ila hawataki kujionyesha kwa mtu mweusi (mimi) kuwa hawawezi niwasaidie. Mi nilikuwa nawacheki tu jinsi wanavyojizungusha maana maisha yao yote wamezoeshwa kujiona wao wapo juu na mweusi chini, but this time around on their nose kuna mweusi yupo juu na wao wapo chini. Anyway, long stori short ni kwamba hata siku moja hawakuwahi kunitamkia wazi kwamba hawawezi. Lengo ni kumaintain image yao waliyoicultivate kwa miaka mingi ya invincibility of white man mbele ya mtu mweusi hata kama ukweli upo wazi kwamba hata wao wana madhaifu yao mengi.

Sasa wewe endelea kujidunisha eti tu kwa vile unaishi katika nchi isiyo na nyumba nzuri kama za ulaya, na kujitamkia udhaifu. Kuna takataka moja ishawahi kuimba eti "bongo bahati mbaya". Stupid!
 

mkuu mi naongelea hii nairobi ya kenya
 
Duh, hiyo ni miaka minne tu ya kukaa ulaya unakuja na maneno ya shombo kiasi hicho!? Hivi nani aliyekuroga wweee mwana usi kwenu!
 
Kuna majitu ni mapumbavu na tatizo kubwa la Tanzania ni raia wake hawana exposure. Jitu mpaka limeota mvi halijawahi kuwa na Passport au halijawahi hata kutembelea walau nchi moja aone Wenzetu wanavyoishi.

Mtu amezaliwa Buza, amekulia Buza, amesomea Buza, ameoa au kuolewa buza. Safari yake ndefu Sana ni mlandizi. Huyu mtu usishangae akakwambia anapenda kuishi uswazi. Hana exposure ya nini maana ya maisha bora. Yale matakataka ya uswazi kwake anaona ni maisha Bora , hajawahi kutembelea nchi za wengine aone miji ilivyopigwa pavements mji mzima.


Mwingine anakuja humu eti "Mimi najivunia maisha ya uswazi" hahahahaha Jinga kabisa sema huna hela za kuishi kwa wanaoishi. Wewe unadumu , huishi.

Kuna Tofauti ya kudumu na kuishi.
 
Mimi sijidunishi. Naipenda nchi yangu. Nimekuja huku chumbani, japokuwa kuna wa mataifa mengine wanaweza kusoma, kuteta ili ikiwa kuna viongozi basi wachukue hatua. NAIPENDA SANA TANZANIA MPAKA KUNA KIPINDI NATOA MACHOZI YA WIVU NIKIONA MIJI YA LEVEL YA KIDUNIA INAVYOPENDEZA ILI HALI SISI TUKIWA NYUMA
 
Wabongo acheni upumbavu kwani unataka sote tuwe na mtazamo sawa.

Heshimu mtazamo wa mwenzio ng'ombe wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…