Nilivyoyaona maendeleo ya Tanzania baada ya kuwa Ulaya kwa zaidi ya miaka minne

Kuna rafiki yangu Mmarekani aliwahi kaniambia Mnawezaje kuishi sehemu mko congested namna hii.

Itakuwa hamjaelewana alichokuwa anamaanisha huyo rafiki yako.

Labda azungumzie mpangilio wa Makazi lakini kama anazungumzia 'congestion' kama ninavyoielewa mimi,
Sijui katokea Jimbo gani la Maporini huko.

Muambie atembele New-York atajua ladha ya hiyo inayoitwa 'Congestion' halisi..
 
Kwetu Mwanza. Nitapaongelea siku ingine. Lengo siyo kujionesha, ama kwamba napachukia nyumbani. TANZANIA NI KWETU. LENGO LANGU NI KWAMBA TUNATAKIWA KUJITATHMINI. KUDHANI TUMEFIKA KUNATUPOTOSHA.
Watu wanalazimisha kuigeuza Nyeusi kuwa Njano.

'Wako Jacko' alivaa Mask alivyotua tu Kwa Bi.Mkora,
Hiyo ni zaidi ya miaka 30 iliyopita.
Sijui kuna anaekumbuk? au wengine mlikuwa kwenye 'flais' za Wazazi bado enzi hizo??
 
Kuwaambia watu ukweli unaoonekana kama matusi ya mjivuni anayetukana kwao baada ya miaka michache ya kukaa Ulaya kunataka diplomasia ya hali ya juu sana.
 
Dunia yote inaangalia west kama reference ya maendeleo. Si China wala Russia wanafanya hivyo. Technology ya China miaka yote imekuwa ni copycat. Viongozi wetu wote wamekuwa wanafanya reference ya Ulaya
Wewe ulitaka nitumie model ipi ya maendeleo?
Kwa hiyo unaniambia tangu watu waumbwe hapa duniani hakukuwa na maendeleo hadi tusubiri miaka ya karne ya 20 na 21 tudese kwa kikundi fulani cha watu wanaoishi West kujua nini maana ya maendeleo? Mbona hizo ni fikra duni sana yaani....! Yaani wewe kwa akili zako mababu zetu wa karne na karne zilizopita hawakuwa kupata ladha ya mafanikio, yaani ni sisi tu tuliopata bahati ya kuishi karne ya 21 kujua nini maana ya maendeleo. Tena kwa definition yako narrow ya maendeleo ni maendeleo ya West, vinginevyo hujaendelea au kufanikiwa!

Narudia, hivyo ndivyo wakoloni wanavyotaka ufikirie. Acha hizo mambo - kuwa na 'jeuri' basi hata kidogo, jithamini, reference ya maendeleo yako iwe wewe mwenyewe. Usiwapuuze wachina au warusi hata kidogo. Hao wamethubutu kudhibiti Western Supremacy Mentality, na uchina au urusi zinaamini katika mambo yao. Yawe ya kisasa au ya asili. Umebaki wewe na wenzako wengine katika Afrika.
 
Wewe ni mpumbavu kama wapumbavu wengine mtumwa kabisa wewe ondoka nchini kwetu nenda usirudi hapa. Tuache na umaskini wetu nyani wewe.
 
Tena ukute huko umeolewa, fala wewe. Unafikia hoteli hupajui kwenu, hujitambui kabisa wewe.
 
Mwamba analalamika ulaya hakuna neti lakini halalamiki ulaya hakuna mbu
 
Maskini, nani kakuambia kwamba wajerumani walitawala Tanganyika had 1940 ? Kwa taarifa yako mjerumani aliondoka Tanganyika baada ya kushindwa vita kuu ya kwanza ya dunia mwaka 1918.
 
Mi kuna jamaa ajawahi kurudi Tanzania kwa miaka 20 toka atoke bongo alisema nchi ipo tofauti sana na alivyoiacha ina muonekano mzuri hasa kwa daslm ilimfanya aanze ujenzi mkubwa huko mbezi beach kwa ajili ya makazi yake ya kudumu...
 
Kuwaambia watu ukweli unaoonekana kama matusi ya mjivuni anayetukana kwao baada ya miaka michache ya kukaa Ulaya kunataka diplomasia ya hali ya juu sana.
Ukweli uambatane na ushauri namna ya kufikia hicho kiwango mnachokiona huko ng'ambo! Ukweli huku unachombeza kwa lugha zisizo na staha, tunarudi kwenye lugha za kuudhi.
 
Mwamba analalamika ulaya hakuna neti lakini halalamiki ulaya hakuna mbu
Hapo ndipo nilipoanza kuona 'mwamba' anatembea ameinama kisa eti akisimama mbingu itamuumiza utosi wake!
 
Rwanda kwenye usafi wako vizuri mkuu,kwa jiji kama dar nilitegemea mtu kama kunenge angesimamia usafi na vile kujaribu kupunguza wafanyabiashara wadogo wadogo kwa kuwatafutia maeneo mengine ya kufanya biashara
 
Kuna ukweli fulani hivi...

Ukienda nchi za wenzetu ukakaa muda kidogo na ukirudi hapa... dah!! Unapaona pa hovyo sana...
Jamaa mzushi tu,wengine tunaishi kwa watu toka 2005 na tukirudi nyumbani unaona kuna kijihatua kimepigwa,shida ya dar uchafu tu na vile vibanda vya wafanyabiashara vilivyozagaa bila mpangilio kila mahali ndio vimeharibu
 
Summer ulaya kuna mbu tena ile mimbu mikubwa unaweza kudhani spider,uzuri wake mbu wale awaambukizi malaria
 
Acha ulimbukeni!! Ndiyo najifariji kwani kujifariji dhambi??? si ndivo nilivyo?? Siwezi jikataa kamwe uswahilini kwetu piga ua galagaza! naweza pabadilisha pakawa pazuri washamba mnaita uzunguni!

Hiyo sinza, mbezi beach, msasani yalikuwa mashamba ya mpunga.enzi hizo!

Nimekaa Evertone green, Downing street maisha yangu ya utoto lkn mabatini Mwanza sikupabagua hata chembe na leo hii ni zaidi ya palivo kuwa.

Siyo siri Watu mliokulia mashambani mna shida sana.mkiona vimiji vidogo vidogo!

Hao ni wanaume wenzako walijenga miji yao na wewe kajenge kwenu pawe pazuri uwazidi.
Nenda Machame, kanyigo-Bukoba! Kenyamanyori-Tarime.kirigiri ni zaisi ya Ulaya. Kericho rural area -kenya.

Quachasnake -lesotho. Ubirunga-wastern cape nk huko ni zaidi ya Ulaya.

Hutarudi na ujinga huu hapa tena kajenge mwenyewe kwenu usibabaike na vimiji vya watu.
Humu humu tu tumejitahidi sana kuliko hata hayo majinga yako.

Wachaga hoyeee!! Wakurya. wajita wahaya hoyeeeee!!! huko ni zaidi ya huo utoporo wako! Huku ukijichanganya tu umekiwa km wao! Hkn ubaguzi mkioleana ndo kabisaaaa! Ni shimbonyi ahafoo tuuu!! Mpaka basi.

Najua kule kwenu ukerewe mnalogana sana. Ndo maana unatamani vimiji vya wenzako!

Dsm yetu iache km ilivo!!! Tunapenda kwa jinsi tulivyo usituletee ulimbukeni wako huo!!!

Tumetoka mbali na siasa zetu za jiji!!!! Endelea kubeba ma box.
 
Naona unaleta stress zako kujibu Mambo usiyoelewa.


Hoja hapa ni maisha ya uswahili na kutokuwa na hela. Umeishi kote huko ila huna hela za kuishi sehemu nzuri.

Diamond kwao Tandale amepabadirisha ila haishi pale uswekeni Tandale. Uswekeni Tunaishi tusiojiwesa. Sema huna hela uishi sehemu nzuri. Usijifafiji eti unapapenda uswazi.

Nina watu zaidi ya 50 nawajua walikuwa wanaishi uswazi ila baada ya kuzipata wamehamia maeneo ya wastaarabu.

Hapa hoja ni Tanzania Ina Maeneo unplanned mengi na sio huo ujinga wako wa kutaja miji Kama umekeketwa. Jikite kwenye mada. Umeishi uswazi ndio maana akili zako zimejaa matope. Licha ya kuishi nje huna exposure yoyote.

Huwa mnadhani kila anaeikosoa Tanzania haipendi au anajiona matawi which is wrong.
 
Uliponiacha hoi ni pale, uliposhanga neti na kupulizwa dawa ya mbu. Kuna siku utakuja kushangaa, kuwa Tanzania hadi leo hakuna magari ya kuzolea barafu barabarani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…