Nilivyoyaona maendeleo ya Tanzania baada ya kuwa Ulaya kwa zaidi ya miaka minne

Nilivyoyaona maendeleo ya Tanzania baada ya kuwa Ulaya kwa zaidi ya miaka minne

Nimekuelewa ndugu. Kwa waliotembea wanaweza kuelewa. Ila wengi hata huu uzi wanaona ni majivuno.

TUNA SAFARI NDEFU SANA

Sihitaji kujifunza history ya nchi yangu mara nyingine maana naifahamu na pia nalipenda taifa langu kwa dhati ya moyo. NASIKITISHWA NA MIPANGO MIJI YA NCHI YETU.
Tatizo watu hawatembei

Ova
 
Maona wachangiaji wengi wanamshutumu mtoa mada bila bila sababu za msingi. Kama nchi naona kwenye swala la mipango miji tumekwama. Sio kwa Dar pekee bali miji karibu yote. Kama kitu rahisi kama kupanga mji kunatushinda mengine tutayaweza?
Wengi ni wanafiki Tu ,wasikupe tabu
 
Mbona Zimbabwe ,Namibia na SA zote zimechelewa kupata Uhuru lakini ziko vizuri kwenye mipango miji ?
Kwa tanzania unaweza ilaumu serikali
Lakini #1 ya matatizo hayo ni sisi wenyewe
Ustarabu ni 000000

Ova
 
Downtown dsm hiyoo
CreativityCode

Ova
View attachment 1719811
IMG-20210304-WA0012.jpg
 
Naona unaleta stress zako kujibu Mambo usiyoelewa.


Hoja hapa ni maisha ya uswahili na kutokuwa na hela. Umeishi kote huko ila huna hela za kuishi sehemu nzuri.

Diamond kwao Tandale amepabadirisha ila haishi pale uswekeni Tandale. Uswekeni Tunaishi tusiojiwesa. Sema huna hela uishi sehemu nzuri. Usijifafiji eti unapapenda uswazi.

Nina watu zaidi ya 50 nawajua walikuwa wanaishi uswazi ila baada ya kuzipata wamehamia maeneo ya wastaarabu.

Hapa hoja ni Tanzania Ina Maeneo unplanned mengi na sio huo ujinga wako wa kutaja miji Kama umekeketwa. Jikite kwenye mada. Umeishi uswazi ndio maana akili zako zimejaa matope. Licha ya kuishi nje huna exposure yoyote.

Huwa mnadhani kila anaeikosoa Tanzania haipendi au anajiona matawi which is wrong.
Dume zima unajua maisha ya mwanaume mwenzako tena unamtaja bila aibu.mkewe afanye nini sasa!au ndo walewale?
Exposure yangu ni ukoo mzima wewe lumbukeni ndo umeona kwa mara ya kwanza.ukoo mzima wewe ndo umeenda safisha macho!
Hata niriporudi bongo niliish fresh. Tu. Maisha lazima upande na lazima ushuke popote ni kawaida
Kwa ushamba wako unadhani utakaa hapo hapo.

Kujenga nyumba kwingine si kuhama wewe fungua akilihizo!

Miaka kumi ijayo unapoona uzunguni patakuwa km uswahilini tu

Kariakoo enzi za mkoloni palikuwa mazogoroni
Punguza ulimbukeni wa kikerewe eti ndo unaona ukanjaaaa!
 
Kwanini tunapiga kelele kwa vijiendeleo kidogo tunavyovishuhudia katika nchi yetu? Tunafanya hivyo kwa sababu kwa muda mrefu sasa watanzania (na waafrika kwa ujumla) tumezoea kusikiliza negative publicity kuhusu nchi zetu, watu wetu na maisha yetu kwa ujumla.

Siku zote wazungu kupitia vyombo vya habari vyao wamekuwa wakiitaja Afrika kama "dark continent", "poorest continent", n.k, n.k. Juzi juzi mke wa Bill Gate hadi aliitabiria Afrika kuwa maiti zitakuwa zikiokotwa barabarani kwa sababu ya corona.

Unaweza kudhani hizo negative publicity hazina lengo. Zina lengo, na lengo lake kubwa ni kutengeneza mazingira ya kinyonge kwa waafrika, na sisi kuendelea kuzidi kujiona duni, na utu wetu kudharirika. Mtu ajionavyo mwishowe huwa hivyo.

Nimefanya kazi na wazungu -- kitu kimoja nimejifunza kwao huwa hawakiri udhaifu hata kidogo hata kama wana udhaifu. Labda nikupe mfano labda utanielewa. Nilipata kufanya kazi katika taasisi fulani ya elimu ya juu nchi fulani ya wazungu (sitaitaja). Mi nilienda huko na mindset kwamba kwa vile wazungu wapo juu basi kutakuwa na mambo mengi ya kujifunza kwao kuliko wao kujifunza kwangu. Ila baada ya kukaa nao kwa muda kama mwezi nikagundua kumbe kuna mambo mengi waliyohitaji kujifunza kwangu kutokana na ujuzi na uzoefu wangu wa awali, kwa aina ya projects tulizokuwa tunazifanya. Sasa tabu ikaja pale walipokuwa wanahitaji kupata solution ya kitu fulani, ila hawataki kujionyesha kwa mtu mweusi (mimi) kuwa hawawezi niwasaidie. Mi nilikuwa nawacheki tu jinsi wanavyojizungusha maana maisha yao yote wamezoeshwa kujiona wao wapo juu na mweusi chini, but this time around on their nose kuna mweusi yupo juu na wao wapo chini. Anyway, long stori short ni kwamba hata siku moja hawakuwahi kunitamkia wazi kwamba hawawezi. Lengo ni kumaintain image yao waliyoicultivate kwa miaka mingi ya invincibility of white man mbele ya mtu mweusi hata kama ukweli upo wazi kwamba hata wao wana madhaifu yao mengi.

Sasa wewe endelea kujidunisha eti tu kwa vile unaishi katika nchi isiyo na nyumba nzuri kama za ulaya, na kujitamkia udhaifu. Kuna takataka moja ishawahi kuimba eti "bongo bahati mbaya". Stupid!
umejitambua sana wewe mkuu. Angalia hata Egypt wanatamani Mafaraoh wote wawe wazungu!!

Eti ile misri ya kale ni chimbuko la wazungu.hawatuongelei hataa!
Hakuna egyptologist mwafrica hata mmoja! Ikitokea basi anapewa jukumu tofauti.
 
Dume zima unajua maisha ya mwanaume mwenzako tena unamtaja bila aibu.mkewe afanye nini sasa!au ndo walewale?
Exposure yangu ni ukoo mzima wewe lumbukeni ndo umeona kwa mara ya kwanza.ukoo mzima wewe ndo umeenda safisha macho!
Hata niriporudi bongo niliish fresh. Tu. Maisha lazima upande na lazima ushuke popote ni kawaida
Kwa ushamba wako unadhani utakaa hapo hapo.

Kujenga nyumba kwingine si kuhama wewe fungua akilihizo!

Miaka kumi ijayo unapoona uzunguni patakuwa km uswahilini tu

Kariakoo enzi za mkoloni palikuwa mazogoroni
Punguza ulimbukeni wa kikerewe eti ndo unaona ukanjaaaa!
Tafuta hela dada acha kudanga.


Punguza stress maisha ukiyakosea mwenyewe acha kutufokea ng'ombe wewe.


Umebeba fuvu limejaa matakataka ya jalalani ndio maana huna unalofikiria zaidi ya mipasho.


Tabia zako za uswazi peleka kwa waswazi wenzio na uwe na heshima Nina uwezo wa kukukojoza wewe na danga lako.


Em out!
 
kuna siku mtaani niliwaambia nairobi wametuzidi miundo mbinu i mean ke..wakabishaaa mi niliwaambia kwa kufika kote kote..wao walibisa kwa kuiona tu dsm
 
Wewe nakuona bado mshamba tu pamoja na ulaya yako thamini kwenu, sizani hata kijijini kwenu umejenga zaidi ya ubishoo tu, anza wewe na mikakati kama mpambanaji ndiyo ukosoe ulaya imejengwa toka tukiwa bado tunatawaliwa na sisi tukiwa watu million 12 leo hii tupo zaidi ya million 60
Shalom,

Baada ya kuwa Ulaya kwa miaka zaidi ya minne, hatimaye mwezi wa tisa mwaka 2020 niliamua kurejea nyumbani ili kumjulia hali baba yangu mzazi pamoja na ndugu zangu.

Kwa kawaida mimi napenda sana kutembea, zaidi napenda kufurahia na kujifunza namna miji duniani kote ilivyojengwa. Hivyo nikiwa ulaya mbali na nchi ninayoishi niliamua kutembelea mara kadhaa Brussels, Paris, Berlin, Colon, Dortmund, London, Oslo na miji mingi midogo ya ujerumani. Pia ili kukidhi haja ya moyo wangu nimetembelea karibu miji yote mikubwa na midogo ya nchi ninayoishi. Pia nilibahatika kutembelea tel aviv na jerusalem nchini israel. Kwa ujumla matembezi yangu yameniwezesha kujionea landmarks muhimu karibu yote kwenye nchi nilizotembelea. Pia kwa kuwa, mbali na safari ya London, Oslo na nchini Israel ambapo nilipanda ndege miji yote iliyobaki nilisafiri kwa bus ambapo nilipata furasa ya kuiona ulaya kwa undani zaidi hasa highways. Kwa ufupi ulaya imeunganishwa na barabara nzuri sana na zenye ubora wa hali ya juu kabisa. Kuna raha yake kusafiri nchi za Ulaya kwa kutumia barabara.

Baada ya utangulizi sasa naeleza nilivyoiona tanzania baada ya kutua Dar es Salaam.

1. Kwa kuwa tulitua usiku, haikuwa ajabu sana kuiona Dar es Salaam.mfano wa nyota za angani ambazo huwa hazina mpangilio maalum maana naijua vema na hata kabla sijaondoka kwenda ng'ambo nilitua na kupaa mara kadhaa kwa safari za ndani, nilijua Dar es Salaam. ina mipango miji mibovu inayofanya nyumba kujengwa bila mpangilio na hivyo usiku kuonesha taa zilizozagaa kama nyota angani. Tofauti kabisa na unavyoshuka usiku kwenye miji mingine duniani ambapo utaona namna barabara za mitaa na highways zilivyopangwa, na hata taa za mji kuwa kwenye mpangilio maalum. Tofauti na nilivyouacha uwanja wa ndege. Walau mara hii terminal 3 kwa mbali sana nilikiri inaondoa aibu tuliyokuwa nayo, lakini hata hivyo niliona kama bado ni ndogo sana.

2. Baada ya kutua na kuvuka security control nilitoka nje na kukutana na dereva wa "hotel' niliyofanya booking kwa njia ya simu baada ya kuiona kwenye booking.Com, haiko mbali sana na airport, nikili wazi njia nzima kuelekea hotelini, nikiwa na picha ya miji ya ulaya kichwani, niliona mji kuwa ni masikini na mchafu kupindukia. Hotel yenyewe niliyolipia laki moja ambayo kiukweli ni hela ndogo sana kwa euro niliikuta ni ya hovyo, chumbani nilikuta kuna neti ya mbu hiki nacho kilinistua maana Ulaya sikuwahi kulala na neti, pia nilikuta chumba kimepuliziwa dawa ya mbu. Palinishinda ilibidi nitafute sehemu nyingine ya kulala.

3. Kesho yake asubuhi nilisafiri kuelekea Mwanza. Baada ya kutua nilendelea kuona umasikini kama niliouona Dar es Salaam, nyumba za kimasikini zisizopangiliwa vema. Airport mtu anakubebea mzigo kwa vile vigari mpaka kwenye taxi, lakini baadaye anakuomba hela wakati haukukubaliana naye. Sintoongelea sana Mwanza.

4. Siku zangu zilivyokaribia za kurejea Ulaya, nilirudi Dar es Salaam. siku 2 kabla, lengo likiwa ni kuona mechi ya timu ya taifa. Nakumbuka kulipokucha na baada ya breakfast nilimwambia dereva taxi anizungushe dsm niione kwa ukaribu, hasa miundombinu inayoongelewa sana kwamba imeifanya Dar es Salaam kuwa kama Ulaya. Lengo lilikuwa baada ya kuzunguka mimi na dereva taxi tukaone mechi. Nilikubali kumlipa kwa ujumla. Nilimtaka anipeleke tff maana kulikuwa na dada mmoja nilitaka kukutana naye ili aniuzie jezi za timu ya taifa, Daraja la Mfugale, daraja Ubungo, kisha twende Mlimani City kwa ajili ya chakula, kisha daraja la Selandar, baadaye twende Kigamboni kupitia Daraja la Nyerere.

  • Daraja la Mfugale - sina mengi ila niliona ni kama kituta fulani tu kilichojaa umasikini - hakuna la maana la kupiga kelele nyingi
  • TFF - licha ya hela zote wazipatazo nilisikitika kuikuta kama nilivyoiacha, inatia aibu
  • Daraja la kijazi - hakuna kitu, kampala tu mbali na kuihusisha nairobi tunatia aibu kwa kelele tuzipigazo, maana wenzetu wa east africa wako mbali sana kwenye mambo ya flyovers
  • Mlimani City-licha ya kuwa napafahamu sana, niliona kuna ulazima wa kujenga malls kubwa zaidi kama ilivyo kwa nairobi na miji ya south africa
  • Daraja la baharini Selandar
  • Niliona kama tunajipiga wenyewe, kiukweli sikuona umuhimu wa lile daraja, maana kijiographia niliona kama limelazimishwa, nadhani linalenda kuwarahisishia mabalozi na watu wakubwa wakaao maeneo ya Mbezi Beach, Oysetrbay na kwingineko kufikia ofisi zao kiurahisi.
  • Maeneo yote ya Upanga na hata ikulu niliona ni pa hovyo sana, uchafu ni mwingi mno, pengine nimeathiriwa na kuishi miji ambayo eneo lote la mji limewekewa tiles.
  • Barabara ya Ali Hassan Mwinyi niliona kuna majengo yamechomoka kidogo yaliupendezesha mji, maana kiukweli Watanzania tuko obsessed obssessed sana na maghorofa pengine kuliko miundombinu muhimu ikiwamo maji taka na maji safi na umeme, hivyo kiurefu wa majengo tu, dsm inayazidi majiji yote niliyotembelea, labda kwa uimara yanaweza kuwa chini ya kiwango ila si haba.
  • Hatukubahatika kuliona daraja la nyerere maana muda wa mechi ulikuwa umefika.

Mwisho - siyo kwamba napachukia nyumbani lengo la uzi huu ni kutaka tubadilike na ikiwa tunataka maendeleo ya kweli ya miji yetu ni lazima tukubali kujifunza na kuona wenzetu wanafanyaje. Ili dsm yetu iwe na hadhi ya kidunia ni lazima (ukweli mchungu) kubomolewa upya, labda kuacha maeneo machache sana, na kujengwa upya (ni hasara lakini baada ya kujengwa upya faida yake ni kubwa sana)

Nawaomba viongozi wetu watembee, wajifunze jinsi miji inavyojengwa kuna faida kubwa sana kwa kufanya hivyo
 
Mleta mada mtu ambaye hajatembelea nchi za Europe ,America,Singapore,Dubai... hawezi kukuelewa,
Watu wameichukulia hii thd in a negative way!
 
Umeandika uzi ama andiko kubwa ambalo halina UZALENDO AT ALL ...wewe kama Diaspora was expecting angalau para moja useme umewekeza nini kuleta tofauti......hilo daraja la nfugale na kijazi tunaoishi hapa tuna jua faida zake na imepunguza traffic kwa kiasi gani......ALL THE BEST HOPE UKIJA UTABEHEVE NA KUANDIKA VEMA KAKA KUNA UMUHIMU WA KUANDIKA
 
Aisee nimeishia tu kuguna Yani unavyo ponda Kama sio kwenu ndio Mana katika story zako zako hujazungumzia hata nyumbani kwenu inamana hujafikia kwenu umeishia hotel nilivyo kuelewa Mimi ni kwamba unatusimulia Kama umefika ulaya we tuache na Tanzania yetu kaishi ulaya
one day yes hata roma haikujengwa kwa siku moja
 

Attachments

  • 1615204903286.png
    1615204903286.png
    404.8 KB · Views: 1
Umeandika uzi ama andiko kubwa ambalo halina UZALENDO AT ALL ...wewe kama Diaspora was expecting angalau para moja useme umewekeza nini kuleta tofauti......hilo daraja la nfugale na kijazi tunaoishi hapa tuna jua faida zake na imepunguza traffic kwa kiasi gani......ALL THE BEST HOPE UKIJA UTABEHEVE NA KUANDIKA VEMA KAKA KUNA UMUHIMU WA KUANDIKA
Tathmini ya mtu makini kuhusu maendeleo ni lazima iwe na uhalisia. Ni wazi na ninasema tena kutoka moyoni kabisa japo naipenda nchi yangu, TUNA SAFARI NDEFU. Kama una uwezo, kabla hujafa, na ikiwa hujawahi toka nje ya nchi, jaribu kwenda Nairobi tu kisha uje tujadili hapa. MAJIBU UTAYAPATA MWENYEWE. UTAIONA DSM TAKATAKA, TUNATAKIWA KUUBOMOA MJI NA KUUJENGA UPYA.
 
Kweli wewe ni limbukeni
Huyu jamaa ni fala, zuzu, limbukeni wa maisha na juha kwa pamoja.
Angefahamu hata kiduchu kuhusu historia ya jinsi nchi za ulaya zilivyojitajirisha kwa kuzinyonya nchi za dunia ya tatu, ikiwemo Tanzania, labda mshipa wa aibu ungemshikisha breki.

Na ukimwuliza umemsaidiaje baba yako kwa kumjengea angalau ka ghorofa tu kama kaulaya, ili naye ajisikie ana mtoto anayeishi Ulaya, domo litambaki wazi!
Amemaliza zizi la kuku la mama yake fukara na kumwachia manyoya tu, huku akiendelea kujitoa ufahamu. Boya sana huyu jamaa.
 
Back
Top Bottom